Samuel SITTA Akamatwe na kushitakiwa kwa Uchochezi

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Sitta: Polisi wana ushahidi Mwakyembe kupewa sumu Send to a friend
Tuesday, 31 January 2012 22:05
0diggsdigg

Raymond Kaminyoge
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nohodha kuwa hatapeleka ushahidi wa madai aliyotoa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu kwa kuwa polisi tayari wanao ushahidi.

Amesema wanachotakiwa kufanya Polisi ni kufanya uchunguzi kuhusu madai hayo ya Dk Mwakyembe kulishwa sumu kwa kuwa ushahidi wanao na wasianze kurushiana mpira.Waziri Sitta alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu.

“ Waziri Nahodha anataka ushahidi gani ikiwa taarifa za madaktari zinazomhusu Dk Mwakyembe kuhusu sumu aliyopewa zilishapelekwa polisi, anataka mimi nitoe ushahidi gani,” alisema Waziri Sitta.

Alisema suala hilo la kulishwa sumu ambalo limempata Waziri si la kawaida hivyo Polisi wanatakiwa kufanya uchunguzi ili kupata ukweli.Alisema kuendelea kukaa kimya kwa kisingizio cha ushahidi, kitawatisha Watanzania wengine kuwa wanaweza kufanyiwa chochote na sheria isifuate mkondo wake.

Juzi Waziri Nahodha alimtaka Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa kuwa Dk Mwakyembe alilishwa sumu.
Alisema ushahidi wa suala hilo ukiwasilishwa ndipo uchunguzi unaweza kufanyika.

Kauli hiyo ya Nahodha ilikuja baada ya Jumapili iliyopita, Waziri Sitta akiwa na kundi la makada wenzake wanaojipambanua kuwa wapambanaji wa ufisadi alirejea kauli yake ya awali kuwa Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela alilishwa sumu.

Sitta alisema hayo katika uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Jijini Dar es Salaam.

“ Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu, kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka,” alisema Sitta na kushangiliwa na waumini wa kanisa hilo.

“ Ni vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia lakini baada ya saa moja unarudia tena, kitu hicho si cha kawaida,” alisema.Sitta alisema wamejaribu wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote.

Tangu Dk Mwakyembe arejee nchini Desemba 2011 kutoka katika Hospitali ya Apollo, India alikokuwa akitibiwa maradhi yaliyosababisha ngozi yake iharibike, Jumapili iliyopita ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonekana katika hadhara ya watu.

Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Kahama, James Lembeli, Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Hilda Ngoye, aliyekuwa Mbunge wa Vunjo, Alloyce Kimaro na Mjumbe wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Makonda.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk Mwakyembe aliapa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi.Alisema, “ Nilifika Hospitali Oktoba 10 (mwaka jana) na tangu wakati huo sikuweza kuvaa viatu lakini leo hii naweza kuvaa viatu, kwa hiyo shetani ameshindwa.

 
six anajua sheria hawezi kukurupuka na hawa polis kwanini wasiwakamate wizi wa mali ya uma na ushahidi wanao
 
Sitta hana ushahidi alikuwa anachochea watu kuasi nchi

Huyo Maumba sheria anazotumia alizitunga Sitta, sasa inawezekana vipi mwanafunzi kumfundisha mwalimu????

DC anaropoka tu, ili aonekane naye kaongea kwenye magazeti achukue hizo hatua anazotaka................ Wakituletea za kuleta tunahama chama tunaenda CCK.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wacha Sitta akamatwe kwa sababu ana kiherehere kwani yeye ndio msemaji wa Mwakyembe? Kwani Mwakyembe ni bubu,kwani Mwakyembe ni taahira hajui kuongea? Na hata bora hiyo sumu ingemuua moja kwa moja mbona amekuwa kama mtoto yeye ndiye alikuwa wa kutuambia ukweli ni upi na uongo ni upi hao wanaojikimbiza kutoa taarifa wanabahatisha tu.
 
waifanyie kazi namna gani wakati umeembiwa kuwa DCI ametoa maelezo baada ya timu ya wataalam kufanya uchunguzi na kukosa ushahidi
Wafanyie kazi ripoti ya madaktari na watuambie ukweli
 
waifanyie kazi namna gani wakati umeembiwa kuwa DCI ametoa maelezo baada ya timu ya wataalam kufanya uchunguzi na kukosa ushahidi
Manumba kashindwa sogea scandal za Blandina Nyoni kuwabadili madaktari India kuweka ndugu zao ataweza ya Mwakyembe naona wote mnawaza kutuletea mafisadi wala nchi 6 akisema ukweli kinawauma?????????????
 
Sie kama WALIPA KODI WAAJIRI WA HAWA POLISI

Tutafurahi kusikia ukweli kuhusu

Madai ya Ndugu Reginald Mengi kuhusu mtoto wake kuwekewa madawa ya kulevya
Mauwaji ya raia-----Kesi ya Zombe mpaka leo ni kitendawili

Jeshi la polisi la Tanzania hata mwenda wazimu hawezi kuliamini kwa nukta moja, ni mara ngapi RAIA wema wanasingiziwa kesi za mauwaji??watu wema wanawekewa madawa ya kullevya------hata siku moja hawajawahi kuja clean na kusema ukweli------haihitaji elimu kujua Mwakyembe kawekewa sumu hata Ngumbaro analijua hilo------nawaonea huruma kwani walipa kodi wa leo ambao ndio waajiri wenu kila kukicha wanazidi kufunguka macho-------kama Mwakyembe alikuwa hajawahi kusumbuliwa hata na maleria huo ugonjwa mnaouzungumzia umetoka wapi----na wewe uliyetoa taarifa ni daktari??? nakuonea huruma kwani tunaouwezo wa kuanika taairfa zote za kinachomsumbua mwakyembe hewani mtaficha wapi uso wenu

tambueni kinachomwaongoza katika kazi sio ni maadili na sio msukumo wa kisiasa

walala hoi tumechoka sasa, someni alama za nyakati
 
...yeah, kama sirikali inaamini inachokizungumza imshitaki Sita. Ila nazidi kuwa na mashaka kwa afya za hawa watu. Mapambano yanaendelea.
 
Back
Top Bottom