Samsung Galaxy S5: Hisia za Awali

Samsung Galaxy S5: Hisia za Awali

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
Baada ya kuitia mkononi siku ya awali ambapo Samsung Galaxy S5 imeanza rasmi kuuzwa katika nchi mia na ishirini Ulimwenguni, tutazungumzia mambo mapya baada ya kuitimia kwa muda wa siku mbili. Kimaumbile imezidi ukubwa kidogo kulinganisha na Galaxy S4 na gamba la kufunika sehemu ya nyuma limebadilishwa na kuwa na nakshi za matundu tundu, gamba hili linavutia zaidi kuliko lile la Galaxy S4, hata hivyo Samsung wanaendelea kutumia plastiki katika sehemu ya nyuma ya simu.

Uzuri

√ CPU yenye kasi kubwa (Quadcore 2.5 GHz)
√ Kioo cha Super AMOLED ni chenye ng’aro wa kuvutia
√ Kupunguzwa kwa apps za Samsung na kuwekwa kenye Samsung Apps
√ Kipima mapigo ya moyo na kisoma alama za vidole ni nyongeza nzuri
Mapungufu
x Wengi walikuwa na matarajio makubwa zaidi ya uboreshwaji, hivyo wanahisi haikuboreshwa vya kutosha
x Tofauti na matarajio ya wengi simu hii bado ni yenye gamba la plastiki.
x Inachukua muda kuweza kutumia kwa ufanisi kisoma alama za vidole na kipima mapigo ya moyo.


Umbile
Simu hii ina umbile la kuvutia, ni nyembamba kiasi, ni kubwa zaidi kulinganisha na Galaxy S4, hata skrini yake ni 5.1” kwa wale ambao hawapendezwi na skrini kubwa watachukizwa zaidi, kwetu sisi ukubwa wa skrini ni nyongeza nzuri kwani skrini ndio sehemu halisi ambayo unatumia simu yako. Umbile lake ni la mraba zaidi huku ikiwa na kona za duara, pia ina fremu (bezel) mithili ya Galaxy Note 3. Kiujumla umbile ni la kuvutia ukiondoa suala la plastiki. Gamba la nyuma na nakshi za matundu linavutia zaidi kuliko la Galaxy S4, hata hivyo tunadhani Gamba la Galaxy S5 linapendeza kuliko la Galaxy S5.



Kipima Mapigo Ya Moyo
Baada ya kutumia mara kadhaa, awali ilitupa shida kwa kukataa kutoa matokeo na badala yake kutoa ujumbe “Make sure fingertip is on the centre of the sensor” (hakikisha ncha ya kidole ipo katikati ya sensa. Pia huongeza maneno “Do not press too hard” (usikandamize sana) Baada ya kujirekebisha katika suala la ukandamizaji kidole katika kipima mapigo ya moyo hichi tumeweza kukitumia kwa ufanisi na bila ya matatizo yoyote, ingawa imetuchukua majaribio ya mara kadhaa katika siku mbili hizi tulizoitumia. Hata hivyo ongezo hili halina maana kubwa hasa kwa watumiaji wa Gear fit, Gear Neo au Gear 2, kwa vile saa zote hizi zina kipima mapigo ya moyo, ambapo kwenye saa hizi ni rahisi kutumia kuliko kwenye simu.


Kisoma alama za vidole
Hii hufanya kazi kwa ufanisi mno, tumeweza kusajili vidole vitatu, na vyote hufungua simu bila ya matatizo, ingawa unapojaribu kutumia huwa inakataa mara kwa mara kwkidole kinatakuwa kisilalie upande wowote. Tunadhani utaratibu huu si wa ufanisi ukilinganisha na iPhone 5S. Kama ilivyo kwenye iPhone 5S utaratibu huu umeongeza usalama kwenye simu kwa vile hakuna wawili wenye alama sawa za vidole ulimwenguni. Pia kwenye Samsung unaweza kutumia alama za vidole kufanya manunuzi kwenye duka la Samsung au hata kufanya malipo kwa kutumia Paypal.




Kuzuia maji
Suala jingine katika simu hii ni kuzuia maji, hata hivyo Samsung hawashauri kuogelea nayo simu hii, huweza tu kuhimili maji kama vile unaponyeshewa mvua. Kwenye sehemu ya kuchaji simu Samsung wameiwekea Galaxy S5 kifuniko ambacho kinazuia maji yasiingie kwenye simu. Hili ni ongezo muhimu hasa ukizingatia kwamba wengi miengoni mwetu huenda na simu kila mahala ikiwemo sehemu ambazo tunatumia maji kama vile msalani. Miongoni mwa kivutio kati ya mambo madogo madogo simu hii hutoa ujumbe wa kukumbusha kufunga sehemu ya kuchajia kila unapoichomoa kutoka kwenye chaja au unapoichomoa waya baada ya kuunganisha na kompyuta.


Kamera
Samsung wameongeza pikseli katika kamera ya Galaxy S5 na kuwa na sensa yenye megapikseli 16, ingawa Nokia wameshatoa sensa yenye pikseli 41 kwenye Lumia, sensa ya simu hii ndio ya kiwango cha juu kabisa kwa simu za familia ya Galaxy za Samsung. kamera hii inafanya kazi kwa ufanisi na ina uwezo wa kurekodi video za 4K ikifuata nyayo za Galaxy Note 3. Sensa ya kamera hii ina kasi kiasi cha kutogundua muda wa kusubiri baina ya kubonyeza kifungo cha kupigia picha na picha kupigwa, na picha za awali ni za kuridhisha mno.


Koti la Touch Wiz
Hii ni namna ambayo Samsung wanaibadili Android na kuifanya iwe ya kipekee kwa simu za Galaxy. Samsung inafanya mabadiliko kadhaa katika Touch Wiz UI, ikiwa ni pamoja na kubadili muonekano wa settings ambapo kila setting inawakilishwa na kijiduara mithili ya app. Vile vile watumiaji wanaweza kubadili muonekano wa settings kwa namna tatu tofauti ikiwa ni pamoja na list view, tab view na grid view, tab view ni mtindo uliotumika kwenye Galaxy za kabla ya Galaxy S5. Malalamiko makubwa ya Touch Wiz ni kuwa husababisha simu kupoteza kasi ukilinganisha na Stock Android, hata hivyo baada ya kuitumia mpaka sasa tumeridhishwa na kasi kubwa ya Galaxy S5 na hatukuweza kupatwa na tatizo la kukwama kwama.


Badiliko ambalo linaweza kuwapa tabu watumiaji wa Galaxy S5 iwapo hawatajifunza haraka ni kubadili kifungo cha in app settings na kukifanya kuwa ni cha multi tasking menu. Hata hivyo unapobonyesha na kushikilia kifungo hicho ambacho kipo kushoto kwa home button, utaweza kuingia kwenye in app settings kama kawaida.


Badiliko jingine ambalo samsung wamelifanya ni kuzifanya baadhi ya Touch Wiz Apps au apps za Samsung kuwa ni za kupakua badala ya kuja zikiwa tayari zimewekwa kwenye simu. Miongoni mwa apps hizo ni pamoja na Story Album, Scrapbook, S Note, Group Play na S Apps nyinginezo. Hivyo hii inakupa nafasi ya kuchagua baina ya S apps au Android stock Apps, mfano unaweza kubaki kuwa na Google Keep badala ya kulazimika kuwa na Google keep na S Note kwa wakati mmoja wakati huzitumii zote.


Watoto
Samsung wameingiza kile walichokiita “Kids Mode” ambapo kabla ya kuiweka simu katika mode hiyo unaweza kuchagua apps gani ambazo utamruhusu mtoto kutumia, na hivyo utakapompa mtoto simu yako hataweza kukuharibia mambo muhimu na pia hataweza kutumia apps ambazo usingependa kutumia.


Ingawa simu hii tumekuwa na kwa muda wa kiasi cha masaa arubaini na nane, tumeiona ni simu yenye kuvutia mno tegemea kupata uchambuzi wa kina kutoka wa simu hii kutoka Gajetek katika kipindi kisichozidi wiki mbili.

Chanzo: gajetek habari


 
Back
Top Bottom