tatizo sio ccm wala kikwete, sijui kwa nini watanzania hatujui hili
tatizo ni sisi wenyewe watanzania kukosa uzalendo na nchi yetu
kwa tabia zetu hata akija barrack obama ni kazi bure
hata tuletewe malaika watukufu kutoka kwa mungu holaaaa!!!
je wanaouza ARVs feki ni akina nani,tembo wanateketea maporini, nenda mahakamani kunavonuka rushwa
nenda vyuoni rushwa za ngono...
watazame walimu wanavohaha kufaulisha watoto wasiojua kusoma na kuandika
watu tai kubwa maofisini lakini hakuna kinachofanyika,watanzania leo hawapigi kura hadi wapewe kitu kidogo
kwa njia yoyote sisi kama watanzania tujue nchi ni yetu, hata nchi zilizo vurugika ulimwenguni
haikuwa abruptly, but very slowly kama tanzania
we need a person ataeingia madarakani kwa njia tofauti na hizi tulizozizoea
huuu u-chadema, na u-ccm kwa mtazamo wangu si lolote si chochote
ni mtazamo jamani tusitafutane