Samoa washinda rugby Dubai Sevens

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Messages
404
Points
225

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2012
404 225
Timu ya rugby ya Samoa ya wachezaji saba kila upande imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Dubai Sevens baada ya kuwafunga New Zealand kwa pointi 26-15 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika nchini humo.
Ubingwa huo ni wa kwanza kwa timu hiyo ya Samoa kwenye michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya ndege ya Emirates.
Wawakilishi wenye nguvu toka Afrika, Kenya walifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuwafunga Ufaransa kwa pointi 15-12. Mapema siku hiyo, Kenya walipoteza mchezo dhidi ya New Zealand kwa pointi 27-7 kwenye nusu fainali za michuano hiyo.
 

Forum statistics

Threads 1,392,810
Members 528,696
Posts 34,118,623
Top