Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mgombea Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika eneo la Dakawa, Mvomelo, Mkoa wa Morogoro leo, tarehe 30 Agosti 2025, amesema lengo la Serikali ni kuona Tanzania ikijitegemea kiuchumi kufikia mwaka 2050, bila kutegemea mikopo mikubwa kutoka nje, akisisitiza umuhimu wa sera na mikakati endelevu ya maendeleo inayolenga kuimarisha uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi.
"Niwaombe sasa, tusimame pamoja na kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi ili tuendelee na kasi ya kuijenga Tanzania tunayoitaka. Tumesema ikifika 2050, Dira yetu inatuambia tuwe tumefika kwenye Tanzania tunayoitaka- Tanzania ya uchumi wa kipato cha kati lakini cha ngazi ya juu, Tanzania ambayo hakuna atakayelia na huduma za afya wala huduma za elimu wala atakayekosa maji bora na kukosa umeme wa kufanyia kazi zake na kumwangazia pahali alipo. Hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka, Tanzania ambayo uchumi wake utasimama na kujitegemea, Tanzania ambayo hatutaishi wala kufanya shughuli zetu za maendeleo kwa mikopo mikubwa, hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka, ifikapo mwaka 2050, safari yake inaanza miaka mitano inayokuja"