Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kujenga na kuimarisha umoja wa kitaifa kuelekea mwaka 2026, kufuatia changamoto za kisiasa na kijamii zilizojitokeza nchini mwaka 2025.
Akihutubia Taifa katika salamu za kufunga Mwaka 2025 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2026, tarehe 31 Desemba 2025, kutoka Ikulu Ndogo ya Tunguu Zanzibar, Rais Samia amesema utulivu wa kisiasa pamoja na hali ya amani na usalama ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa.
Amesema mwaka 2025, licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana, Taifa lilipitia pia changamoto na mitihani iliyowagusa Watanzania wengi, hususan katika kipindi cha mwezi Oktoba, ambacho kilihitaji subira, mshikamano na uzalendo wa hali ya juu.
Rais Samia amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wote kwa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa, hatua iliyoiwezesha Tanzania kudhihirisha mbele ya ulimwengu kuwa ni taifa imara, himilivu na lenye uwezo wa kushughulikia changamoto zake kwa misingi ya amani.
Ameeleza kuwa Serikali inapoanza mwaka 2026 imejipanga kujenga upya mshikamano wa kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ambapo maandalizi ya kuunda Tume ya Maridhiano yameanza rasmi.
Kwa mujibu wa Rais Samia, Serikali itahusisha wadau wote katika mchakato wa kukubaliana kuhusu muundo wa tume hiyo, ikiwemo aina ya wajumbe, majukumu yao pamoja na muda wa utekelezaji wa kazi za tume, kwa lengo la kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa Watanzania.