Samia ni Rais anayesikiliza, lakini "Legasi" yake itakuwa ipi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,684
46,371
Tangu aingie madarakani kuna mageuzi ameyafanya kuirudisha nchi katika ya hali iliyokuwa kabla ya mwaka 2016.

Kelele kubwa ya mwanzo katika utawala wake ilikuwa kesi ya ugaidi ya Mbowe, DPP akaindoa mahakamani baada ya mwaka mmoja.

Watu walipopiga kelele kuhusu Sabaya, aliwekwa pembeni akakamatawa na kufungwa.

Amekutana na wapinzani wake kutoka vyama vya upinzani mkali kama CHADEMA alipokutana na Lissu Ubelgeji na Mbowe mara 2 nyumbani, pia amekutana na vile vyama rafiki kwa serikali kama ACT.

Amepandisha mishahara ya watumishi wa umma baada ya miaka 7 na pia ametaka sheria za pensheni kufanyiwa marekebisho baada ya kelele za muda mrefu.

Tumeumona akikutana na mashirika ya utetezi wa haki za binadamu

Kesi nyingi za uchochezi za wapinzani zimefutwa baada ya kelele nyingi kubwa na za muda mrefu

Vyombo vya habari vimepewa uhuru kiasi japo yeye na Nape wamesema ni "busara tu" zimetumika ila sheria zipo pale pale!

Amerejesha na kuimarisha mahusiano yaliyokuwa yanalega na nchi za magharibi na majirani kama Kenya.

Anakutana na vyombo vya habari mara kwa mara kwa mahojiano na ufafanuzi wa mambo mbalimbali tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa ikifanyika kwenye mikutano ya kuapisha viongozi.

Kila mara amerejea maneno ya kuwaita watu wazungumze.Na pia hasemi ukimshauri unaharibu . Haya ni baadhi ya mambo mazuri aliyoyofanya katika kipindi chake kifupi cha mwaka mmoja lakini "legasi" yake itakuwa ni ipi ukizingatia ?

Anakabiliwa na miradi mengi mikubwa aliyorithi ambayo ilikuwa katika hatua za awali tu wakati anachukua nchi.

Anakabiliwa na wahafidhina wasiotaka mabadiliko ndani ya chama chake na serikalini.

Anakabiliwa na watu waliosahaulika kwa kipindi kifupi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 ambao sasa wanadhani ni wakati wao nao wa "kula"

Kuna wanaoona anachukua muda mrefu sana kufanya mabadiliko, walitaka mambo yaende haraka haraka mfano kwenye suala la kupanda bei za mafuta.

Asipopata jambo moja kubwa la kwake kipekee la kupigia kelele na kuuzika kwa wananchi wengi legasi yake inaweza kutazamwa zaidi katika yale machache makubwa ambayo hatatimiza au hatafanya vizuri kuliko yale mazuri madogo madogo mengi ambayo atayafanya vizuri.
 
Back
Top Bottom