GE2025 Samia: Lengo letu ni kwamba ifikapo miaka mitano ijayo kila Mtanzania awe karibu na maji safi na salama

GE2025 Samia: Lengo letu ni kwamba ifikapo miaka mitano ijayo kila Mtanzania awe karibu na maji safi na salama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Hadi leo bado tunapiga porojo za sera za maji? 🤔 Hii ni aibu kweli! Nchi nyingine wanasonga mbele na teknolojia za kisasa, sisi bado tunajadili kama maji yatamiminika kwenye bomba au kwenye ndoo. Kwa kweli safari yetu ni ndefu kuliko hata msafara wa ngamia jangwani! 🐪
=================
“Lengo letu ni kwamba ifikapo miaka mitano ijayo kila Mtanzania awe karibu na maji safi na salama. Miradi ya maji Nakonde pamoja na ule mkubwa wa kutoa maji Mto Ruvuma kwa ajili ya Mtwara Mjini na Vijijini tutaikamilisha, sambamba na miradi midogo midogo inayotekelezwa maeneo mbalimbali,” amesema Rais Samia.

Mbali na sekta ya maji, mgombea huyo amezungumzia pia mafanikio katika sekta ya elimu ndani ya miaka minne iliyopita, akibainisha kuwa serikali itaendelea kuajiri walimu wapya, kujenga nyumba za walimu na kuimarisha miundombinu ya shule ili kuhakikisha elimu bora inapatikana nchi nzima.

 
Marekani hadi vijijini kuna lami ,ukijenga nyumba serikali inaweka rough ya zege kutoka barabarani hadi kwako koki za maji ya zimamoto yapo states zote hadi vijijini kwa fire emergency(Fire Hydrants)...Kuomba kura hawana ahadi za kujenga barabara wala kuleta maji....Miaka zaidi ya 60 ya uhuru tunahangaika na maji ni upuuzi mtupu.

Serikali imeshindwa kabisa kuwa na mkakati wa kchimba visima na kuweka TANK kubwa kila kata na kujenga mtandao wa maji kwenye kata husika? Mabilioni anayoiba ABDUL si yanaweza kumaliza shida ya maji?
 
Back
Top Bottom