GE2025 Samia kuumaliza mgogoro wa wakulima na NAFCO

GE2025 Samia kuumaliza mgogoro wa wakulima na NAFCO

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Shirika la Chakula na Kilimo (NAFCO) limetoa hekari 3,000 kutoka katika mashamba yake kwa ajili ya Wakulima wa Namtumbo mkoani Ruvuma ili kuendeleza shughuli za kilimo.

Dkt. Samia alitoa kauli hiyo leo Jumatatu, Septemba 22, 2025, wakati akiendelea na kampeni zake mkoani humo. Amesema hatua hiyo ya NAFCO na serikali inalenga kuhakikisha wakulima wanapata maeneo ya kulima huku shirika hilo likiendelea na jukumu lake la kuzalisha mbegu bora kwa kilimo nchini.

Soma pia: Rais Samia aendelea kuthibitisha kwamba anawajali wakulima, atoa onyo kwa wawekezaji wa zao la chai Rungwe



“Lile shamba ni muhimu kwa sababu ndipo tunapozalisha mbegu. Tumeamua kuzalisha mbegu zetu wenyewe hapa nchini badala ya kuagiza nje, kwani mara nyingine huletwa mbegu zisizo bora au zilizokufa. Hata hivyo, pamoja na umuhimu wake, NAFCO wamekubali kutoa hekari 3,000 kwa ajili ya wakulima,” amesema Dkt. Samia.

Aidha, mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Dkt. Samia ameahidi kuwa akipewa ridhaa ya kuongoza serikali, atajenga barabara ya Mtwara Pachani–Nalasi–Tunduru kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 318 pamoja na madaraja yatakayohusiana na barabara hiyo, akisema ni kiungo muhimu cha kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Ruvuma na mikoa jirani.
 
Back
Top Bottom