Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Samia kwenye kampeni zake zote akumtaja na kumeeleza vyema hayati Magufuli kama alivyofanya leo wakati yupo huko Chato!
Unafiki wa kura unaendelea
=======================
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amemkumbuka na kumsifu Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli kama kiongozi mzalendo na mwenye maono ya kimkakati, aliyeliweka Taifa kwenye msingi imara wa maendeleo kupitia miradi mikubwa ya kimkakati.
Akizungumza leo Jumatatu, Oktoba 13, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Chato, mkoani Geita, Samia amesema miradi mingi mikubwa ambayo sasa inawanufaisha Watanzania ni matokeo ya dira na misingi aliyoiacha Magufuli.
“Hayati Magufuli alikuwa kiongozi shupavu, mzalendo na mwenye maono makubwa. Alikuwa mwalimu mzuri na mlezi mahiri ndiyo maana nimeweza kuendeleza kazi tulizoanza awamu ya tano kwa ufanisi,” amesema Samia.