GE2025 Samia anachukizwa na shida za wananchi na umaskini lakini hachukizwi na utekaji wa raia unaoendelea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Kibamba Mkoani Dar Es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angellah Kairuki amesema katika kipindi kifupi alichofanya kazi chini ya Rais wa awamu ya sita na Mgombea Urais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa shahidi wa huruma, imani na kujali kwa Dkt. Samia, akimuombea ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

"Mimi ni shuhuda wa dhati wa kazi kubwa alizofanya Dkt. Samia, ni kiongozi wa imani, mtu wa huruma, mtu wa maamuzi ya dhati na mwenye kujali shida na matatizo ya Watanzania. Dkt. Samia anachukizwa na umaskini, anachukizwa na shida za watu na anatamani kuona watu wanakuwa na ustawi na wakati wote katika maelekezo yake katika kazi amekuwa akisisitiza kuwafikiria wananchi na ustawi wao na zaidi mwananchi wa kawaida." Amesisitiza Mhe. Kairuki.

Kairuki ametoa kauli hiyo leo Oktoba 21, 2025 Kinondoni Jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Leaders Club wakati wa muendelezo wa Kampeni za Dkt. Samia Mkoani Dar Es Salaam, akieleza kuwa mara kadhaa amemuona Dkt. Samia akikosa usingizi na kuchukizwa na hali ya umaskini wa Watanzania na kuwasukuma mara zote wasaidizi wake kuwataka wakawatumikie wananchi.

Ameeleza baadhi ya maeneo ya msisitizo kwa Dkt. Samia kuwa ni kuendelea kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi na kusimamia ubora wa huduma za afya, maji, elimu na nishati safi sambamba na kusisitiza uchukuaji wa hatua mbalimbali katika kuwawezedha wananchi kiuchumi.

Akizungumzia Jimbo la Kibamba kwa miaka minne na nusu ya Uongozi wa Rais Samia, Mgombea Ubunge huyo amemshukuru kwa kuwekeza zaidi ya shilingi Bilioni 3.4 kwenye sekta ya afya, Bilioni 6.4 kwenye elimu ya msingi na awali pamoja na uwekezaji wa shilingi Bilioni 14.8 kwaajili ya uendelezaji wa elimu ya sekondari katika Jimbo hilo la Dar es Salaam.
 
🎶"..angeimba nini Sister P asingekuwepo Zay B?.."🎶
 
Atachukiaje kazi yake mwenyewe inayomuweka hapo alipo kwa RAHA ZOTE.
 
Huyu rais wa hovyo hovyo kabisa kabisa kabisa
 
Back
Top Bottom