Same: Mwanafunzi asombwa na maji ya mvua

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,272
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali, Mwanafunzi anayedhaniwa kuwa wa sekondari , mkazi wa eneo la stesheni wilayani Same amesombwa na maji ya mvua usiku huu akiwa anavuka korongo wakati akielekea mtaani kwake.

Mashuhuda ambao ni wanafunzi wenzake wamedai walikubaliana kuvuka kwa zamu na mwanafunzi mwenzao alipoanza kuvuka maji hayo yalimsomba.

Hadi muda huu wananchi mbalimbali wako eneo la tukio wakishirikiana kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo.

Poleni familia ya mwanafunzi.
 
Heading kama una kichwa kichafu ukisoma haraka haraka dah inaleta neno jengine kabisa...

btw tuombee apatikane akiwa mzima.
 
allah (t.w) ajaalie apatikane akiwa hai in shaa allah.

Mpaka muda huu ni ngumu kumpata akiwa hai. Lisaa lizima lishaisha halafu inaonekana amepelekwa mbali mnoo. Tuombe asifikishwe mto ruvu maana mvua bado inanyesha
 
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali, Mwanafunzi anayedhaniwa kuwa wa sekondari , mkazi wa eneo la stesheni wilayani Same amesombwa na maji ya mvua usiku huu akiwa anavuka korongo wakati akielekea mtaani kwake. Mashuhuda ambao ni wanafunzi wenzake wamedai walikubaliana kuvuka kwa zamu na mwanafunzi mwenzao alipoanza kuvuka maji hayo yalimsomba. Hadi muda huu wananchi mbalimbali wako eneo la tukio wakishirikiana kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo.

Poleni familia ya mwanafunzi.
Stesheni Makanya?
 
Ameokotwa akiwa ameshakufa tayari. Ni mwanafunzi wa kike anayeishi stesheni ya same mjini
Nimesoma Same sec enzi hizo,Tulikua tunaenda station kuchota maji.Weekend tunaenda Kwa Katengu mjini kuangalia movie afu napita kwa babu mahuu kula Diet.
 
Aisee umesahau masandare kweny vimbuzi..
Nimesoma Same sec enzi hizo,Tulikua tunaenda station kuchota maji.Weekend tunaenda Kwa Katengu mjini kuangalia movie afu napita kwa babu mahuu kula Diet.
 
Back
Top Bottom