Samatta Ampa Big Up Ismail Aden Rage

Rio Tinto

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
777
451
Mchezaji Bora wa Ndani Barani Afrika na mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Ally Samatta amemtaja Mwenyekiti wa Zamani.wa Simba Ismail Aden Rage kama mmoja wa watu muhimu waliochangia mafanikio yake.
Samatta anafunguka kwa kusema kama sio uamuzi mgumu wa Mwenyekiti huyo wa Zamani wa Simba kusafiri mpaka Lubumbashi kukutana na Mmiliki wa TP Mazembe ili kukamilisha usajili wake basi ingekua ngumu kwake kupata platform ambayo klabu yake hiyo yenye makao yake Lubumbushi inampatia na kujulikana Afrika nzima...
Ikumbukwe pia Rage alihakikisha kwenye mkataba wa kumuuza Samatta basi kunawekwa kipengele kitachoinufaisha klabu ya Simba ikiwa Mchezaji huyo atauzwa kwenda klabu kubwa hapa Afrika ama Duniani.

Samatta anasema Mwenyekiti huyo wa Zamani alikua ana imani kubwa juu yake ndio maana alishinikiza kuwekwa kipingele hicho..

Swali kwa utawala wa Evans Aveva unaacha legacy gani kwenye klabu yetu maana kila siku hadhi ya Simba inashuka..
 
Kiukweli ukiondoa mapungufu yake ya kibinadamu, Ismail Aden Rage alikua ni kiongozi mwenye maono zaidi kuliko Evance Aveva!
Ni kipindi cha uongozi wa Rage Mbwana Samatta aliuzwa Tp Mazembe, Okwi aliuzwa Etoille du Sahel ingawa dili ilibuma kutokana na ukunguru wa mchezaji husika, na pia tulishuhudia timu ikimiliki eneo lake la uwanja kule Bunju huku Aveva akishindwa kuendeleza eneo lile hadi sasa! Kiujumla hizi timu mbili kongwe nchini za Simba na Yanga ifikie tu wakati zimilikiwe na watu binafsi (matajiri) ili ziweze kutoka hapo zilipo badala ya kuwategemea wanachama na wachumia tumbo!
 
so far Rage alifanya walau machache kwa samba...hata pale timu ilipoyumba ilikuwa ni kwa sababu ya hawa kina kaburu na kina aveva....

Hawa wa sasa hata Ubingwa wa Ligi samba haitakaa ichukue hata siku moja
 
...hawa jamaa wakiendelea kuwepo,Simba ikijitahidi sn itaishia nafasi ya tatu.
 
Kumsifia Rage ni kujishushia hadhi,Yule ni mpigaji hatari.Ili tumheshimu samata akae tu kimya
 
Back
Top Bottom