Samaki wa Magufuri wagawiwa bure

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Serikali imetangaza kuwa samaki waliokamatwa wakivuliwa eneo la Tanzania mwezi machi mwaka huu, kuwa itawagawa bure,

Waziri wa uvuvi Mh Maghufuri ametangaza hayo sasa hivi huko Dodoma, kuwa tani 290 zote zitagawiwa bure mashuleni, vyuoni vituo vya mayatima na makambini tu

Sijui hii ni huruma kwa wananchi au ni sehemu ya kampeini ya 2010?
 
Hivi kunauhakika gani kama bado hao samaki ni salama? au wameishakuwa na madhara ndo wanaamua kuwagawa
 
Serikali imetangaza kuwa samaki waliokamatwa wakivuliwa eneo la Tanzania mwezi machi mwaka huu, kuwa itawagawa bure,

Waziri wa uvuvi Mh Maghufuri ametangaza hayo sasa hivi huko Dodoma, kuwa tani 290 zote zitagawiwa bure mashuleni, vyuoni vituo vya mayatima na makambini tu

Sijui hii ni huruma kwa wananchi au ni sehemu ya kampeini ya 2010?

"wewe samaki zimekosa watu wa kuzinunua ni bei ghari mno samaki mmoja"
 
Asante sana Kaitaba nimekupa thanks. ni jana tu nilikuwa nawawazia hawa samaki wameishia wapi kumbe bado wapo.....
 
Asante sana Kaitaba nimekupa thanks. ni jana tu nilikuwa nawawazia hawa samaki wameishia wapi kumbe bado wapo.....
Nakushukuru sana, ni vyema tukapeana habari zinazotokea kila mahali kwani dunia sasa hivi ni kama kitongoji tu,

We unaonaje uhamuzi huu.
 
Kwa vile wameitia hasara serikali, hata kuwauza haitasaidia. Bora wagawiwe kwa wananchi wapate kitoweo.
Lengo ni kuwafunga midomo watu waliokuwa wameanza kuchonga kuwa samaki hawa wametia hasara taifa
 
Lakini kwa muda waliokaa kwenye barafu, kweli watakuwa bado wanafaa kwa matumizi ya binadamu, isije ikawa wateja wamekosekana ndo wakaamua kuwauza, baada ya miezi kadhaa magonjwa ya ajabu yanaibuka,
 
samaki hao....watakuwa tasteless....lakini wanafaa kuliwa.....kama walikuwa frozen -1.8 kila siku....
 
Lakini kwa muda waliokaa kwenye barafu, kweli watakuwa bado wanafaa kwa matumizi ya binadamu, isije ikawa wateja wamekosekana ndo wakaamua kuwauza, baada ya miezi kadhaa magonjwa ya ajabu yanaibuka,

Wamehifadhiwa kwenye joto la below minus 18 degrees centigrade na kwa temperature hiyo they can be stored for over 24 months. Hivyo shelf life zao ni 2 years under the above conditions
 
Katika hili nivyema wataalamu wa afya wakawapima kabla ya kuwagawa.
pamoja na hilo pesa zetu kwanza tunaficha madhambi kwa kugawa bure! hapana jamani! pesa za kuifadhia hao samaki nani analipa? kama siyo kodi zetu tu mbona viongozi wetu wametuona matutusa sana? kwanini hawkuzigawa mwanzo kabla hazijaleta hasara? mi sijui bwana wa tz wenyewe ndo hao wanipenda CCM kama nini!
icon8.gif
 
kama wanafaa kwa matumizi ya binadamu kwanini wasiuzwe kwa gharama nafuu????????? au takrima, na kama wakigawa bure ujue kwenye kampeni zijazo utasikia tu Ndugu wananchi HAMJALA SAMAKI? Tumekulaaaaaaaaaaa ipeni kuLA CCM
 
Serikali imetangaza kuwa samaki waliokamatwa wakivuliwa eneo la Tanzania mwezi machi mwaka huu, kuwa itawagawa bure,

Waziri wa uvuvi Mh Maghufuri ametangaza hayo sasa hivi huko Dodoma, kuwa tani 290 zote zitagawiwa bure mashuleni, vyuoni vituo vya mayatima na makambini tu

Sijui hii ni huruma kwa wananchi au ni sehemu ya kampeini ya 2010?

Chondechonde angalieni wanafunzi na watoto wetu wasije wakaanza kupata mafua ya samaki
 
kama wanafaa kwa matumizi ya binadamu kwanini wasiuzwe kwa gharama nafuu????????? au takrima, na kama wakigawa bure ujue kwenye kampeni zijazo utasikia tu Ndugu wananchi HAMJALA SAMAKI? Tumekulaaaaaaaaaaa ipeni kuLA CCM

Jamani waziri ameamua samaki waliwe na wananchi, ninyi mnaleta maneno mengi.
Hivi angeamua kuchukua 10% yake toka kwa hao wavuvi haramu na akawacha waendelee zao ingekuwa faida ya nani?

Na wangeliwaje wakati kesi ilikuwa bado inashughulikiwa kujua uhalali wa hao wavuvi waliovamia maji yetu.

Mwacheni afanye kazi yake. Sidhani kama Magufuli anaweza kuwauwa wananchi wake kwa kuwapa chakula kibaya. Kama kilihifadhiwa vyema haina shida.

Mbona mnaletewa expired food/bidhaa toka nche ya nchi na zimejaa madukani kibao na hamsemi?? sembuse samaki wetu??? Ama kweli huwazi kumfurahisha binadamu.
 
hakuna cha kampeni 2010 wanajaribu kuficha ujinga wao baada kuona gharama walizotumia kuhifadhi samaki mpaka leo ni kubwa kuliko mauzo ya hao samaki wenyewe kama wakitaka kuuza leo.wameona bora wagawe kwa wananchi itasaidia kuficha ujinga wao wakushindwa kufikiria mambo kabla ya kutenda.
 
Serikali imetangaza kuwa samaki waliokamatwa wakivuliwa eneo la Tanzania mwezi machi mwaka huu, kuwa itawagawa bure,

Waziri wa uvuvi Mh Maghufuri ametangaza hayo sasa hivi huko Dodoma, kuwa tani 290 zote zitagawiwa bure mashuleni, vyuoni vituo vya mayatima na makambini tu

Sijui hii ni huruma kwa wananchi au ni sehemu ya kampeini ya 2010?

Mambo mazito. Kwanza kesi yenyewe bado kumalizika maana ile ni exhibit na haitaweza kugawiwa bila kesi kumalizika. Itabidi wa speed up ili wawahi takrima ya 2010. Kama kweli si takrima basi na wapeleke mashuleni ambapo kuna under 18 (Primary na O-level in many cases) ambao not eligible for votting!!!!! Kazi ipo.
 
Jamani waziri ameamua samaki waliwe na wananchi, ninyi mnaleta maneno mengi. .

Kwa hiyo Waziri wa afya akisema Matumizi ya kondom yamepitwa na wakati msitumie inatakiwa tukubali tu sababu waziri kasema, makada bana we utakuwa umenyweshwa maji ya bendera tena iliyopauka. Nilichosema Kuwa Wataalam wa afya wauthibitishie umma kuwa wako salama kwani hata hizo bidhaa fake ulizosema tunazijuaje si mpaka tbs wazipitie non sense
 
Jamani waziri ameamua samaki waliwe na wananchi, ninyi mnaleta maneno mengi. .

Kwa hiyo Waziri wa afya akisema Matumizi ya kondom yamepitwa na wakati msitumie inatakiwa tukubali tu sababu waziri kasema, makada bana we utakuwa umenyweshwa maji ya bendera tena iliyopauka. Nilichosema Kuwa Wataalam wa misosi wachek na wauthibitishie umma kuwa wako salama kwani hata hizo bidhaa fake ulizosema tunazijuaje si mpaka tbs na taasisi zinazohusika wazipitie.......... non sense
 
Wasiwasi wangu ni kwamba labda wanasumu, tutajuaje kama walivuliwa katika njia salama?. NIONAVYO MIMI wachomwe moto. najua huko mashuleni na kwingineko kuna problem itatikea tu. harafu tutatafuta mchawi. Mimi nimetabiri hivyo.
 
Back
Top Bottom