Samaki wa magufuli wasuswa!!

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
broken-heart.jpg


Furaha Kijingo na Festo Polea

TAASISI mbalimbali, vyuo, vituo vya watoto yatima na watu binafsi jana vilikwamisha kazi ya ugawaji wa zaidi tani ya 100 za samaki waliovuliwa kinyume cha sheria katika Bahari ya Hindi eneo la Tanzania kutokana na kushindwa kujitokeza kuitikia wito wa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli.

Kazi hiyo iliyotarajiwa kufanyika katika kiwanda cha Bahari Foods kilichopo Mwenge Jijini Dar es salaam lilitarajiwa kujaza watu wengi baada ya Waziri, Magufuli kutangaza kugawa samaki hao upya.

Lakini kinyume na matarajio ni taasisis moja tu ndiyo iliyojitokeza kuchukua Kg 149 ya samaki hao.

Awali waandishi wa habari walifika katika kiwanda hicho saa tatu asubuhi na kukaa hapo hadi saa sita mchana ambapo walishuhudia taasisi moja ya Salafiya Islamic Centre ilyopo Bunju A ndiyo iliyojitokeza kuchukua samaki hao.

Mmoja wa maafisa waliopo katika kazi ya ugawaji kiwandani hapo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini alisema kazi hiyo imekuwa gumu kwa kuwa taasisi nyingi zilizokusudiwa zilikuwa ni Vyuo vya Elimu ambavyo vingi ndiyo kwanza vimefunguliwa.

"Mimi nafikiri kazi hii inakuwa gumu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya vyuo husika kutofunguliwa na hata wananchi kutokuelewa hatua mpya za uchukuaji wa samaki hao zilizotangazwa jana na Waziri mwenye dhamana ya samaki nchini," alisema.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi John Magufuli alitangaza muda wa siku tatu kuhakikisha samaki wote wanachukuliwa.

Awali, wakati akisaini mkataba wa uvuvi na Chama cha wavuvi kutoka nchini Japan, Waziri Magufuli aliwataka wananchi wote wenye vigezo vikiwemo vya kuwa na taasisi za kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, watoto yatima na vinginevyo kujitokeza kwa wingi kuchukua samaki hao jana.

Waziri Magufuli alisema ameamua kufafanua hivyo baada ya baadhi ya watu kuhusisha kisiasa kushindwa kwa serikali ya Zanzibar kuchukua asilimia 40 za mgawo wa Samaki hao.
Alisema ameamua kuwagawa pamoja na tani 40 zilizokusudiwa kwa Zanzibar baada ya kupokea barua kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira wa Zanzibar, Burhan Saadat kuwa wameshindwa kutokana na kutokuwa na umeme katika visiwa hivyo.
 
Back
Top Bottom