Samahani mke wangu

Samahani mke wangu

Nime-like halafu baadaye nikakumbuka ... KAHABA ANAPOMSHAURI KAHABA MWENZIE...


Ni ukweli usiopingika ni nadra sana kumkuta mwanaume hana mchepuko, cha msingi wanaume tuhangaike lakini mkeo ndiyo kila kitu
 
Mfano mzuri ni wewe mwenyewe Zogoo, mama watoto kuonyesha kutojali mambo yako na kutaka kuondoka, si umeona nusra uchanganyikiwe. Na alivyokusamehe umefurahi mpaka husikii hata njaa...lol
Hahaha chezea kusamehewa
 
  • Thanks
Reactions: kui
Yani huyo mke ningempa na haka ka Zawadi
1471154302666.jpg
 
Mke wangu Samahani

Niliamka asubuhi nikamkuta mke wangu akisali, nilimsikia akiniombea na mimi, nilimtazama kwa mshangao sana!


Ni muda mrefu umepita tangu nimuone akisali. Katika kipindi cha miezi michache iliyopita tumekuwa tukibishana, na jana usiku tuligombana sana, nilitoka chumbani na kushuka ngazi haraka kwenda jikoni kujiandalia kifungua kinywa (chai) kwani kwa siku kadhaa huduma hiyo ilishasitishwa. Nilistaajabu na kupatwa na mshangao kukuta chai tayari imetengwa mezani, nilikunywa na kurejea chumbani ili nikaoge, Mke wangu alitoka bafuni na kusema “Habari ya asubuhi, uwe na siku iliyobarikiwa” huku akijishughulisha pale chumbani, nilienda bafuni kuoga, baada ya kuoga na kujiandaa kwenda kazini nilimkuta Mke wangu akinywa chai kwa Amani huku akitazama video za vichekesho na kucheka sana. Nilimtazama mke wangu kisha nikaelekea mlangoni na kuondoka kwenda kazini.


Muonekano wa mwisho aliokuwa nao mke wangu kabla sijaondoka ulikuwa wa mtu mwenye Amani, Muonekano huo ulinisumbua sana. Hivyo sivyo anavyopaswa kuwa. Hivi sivyo alivyokuwa hivi karibuni. Nilikuwa nikimuumiza sana, Mke wangu aligundua kuwa nina mahusiano na wanawake wengine, na nilitumia fedha iliyokusudiwa kwa ajili ya familia kutumia na wanawake hao, Alipaswa kufura kwa hasira, Utulivu wake, ulinisumbua sana siku nzima, Ikawa jioni nilirudi nyumbani na kukutana na mke wangu aliyekuwa na Amani, alikuwa anapika na kucheka na watoto wetu , yeye alirejea masaa mawili kabla yangu toka kazini. Chakula cha usiku tulikifurahia sana, Chakula kilikuwa kizuri na kitamu, Mke wangu aliongea kwa furaha na watoto. Nikiwa Baba na Mume nilihisi nimetengwa, Mke na Watoto wangu walionekana wenye furaha sana licha ya mimi kuwaumiza,


Usiku ule baada ya chakula, Mke wangu akiosha vyombo na watoto wakienda kulala nilimfuata na kumuuliza”uko sawa”? Ni Zaidi ya sawa nimebarikiwa” alijibu, Hujanikasirikia? Hata baada ya yote niliyoyafanya na niliyokukosea? Nilihoji, Aliweka sahani iliyooshwa katika chanja kisha akanitazama na kusema “Nilijiuliza, ni upi uhusiano muhimu katika maisha yangu? Uhusiano nilionao na wewe au nilionao na Mungu?”Nikatambua ni ule uhusiano nilionao na Mungu, Ninaishi kwa ajili ya Mungu sio kwa ajili yako, kuoana na wewe ilikuwa Baraka lakini siyo kila kitu kilichopo katika maisha, Mungu amenibariki kwa kunipa maisha na sitoyatumia bure kwa kulialia sababu ya maumivu unayonisababishia”.


Mke wangu alichukua glasi chafu na kuanza kuiosha, aliendelea”Nilikuja kugundua kuwa nimekupa nguvu nyingi, Ndio wewe ni Mume wangu, binadamu uliye karibu sana nami maishani mwangu na ninayekupenda sana, ila wewe siyo Mungu, Umeniangusha ila Mungu kamwe haniangushi, sitoruhusu uniharibie furaha, Amani na maendeleao yangu, Vunja tu ndoa yetu iwapo unataka, ila mimi nitamshika Mungu,nitakapomshika Mungu nitakuwa mwenye furaha tele licha ya yale unayonifanyia “ alisema huku akisuuza glasi, alinitazama usoni na kuendelea kuongea “Uliponiumiza na kunidhalilisha niligundua nilikuwa ninafanya mambo kama Mwanamke asiyekuwa na Yesu! Nilikasirika na kutukana, nilitaka kulipiza kisasi na nikaruhusu univuruge siku hadi siku, utendaji wangu kazini ulishuka, niliongea kidogo sana na watoto wetu, nikawa mkali sana kwa watoto, nikajihurumia, nikapata vidonda vya tumbo.


Ndipo nilipotambua nina Mungu, sitakiwi kuishi kama mtu asiyekuwa na uhusiano na Mungu Kwa nini nisiwe na tumaini wakati Mungu yupo pamoja nami? Nilikuwa nimetoa kipaumbele kikubwa sana kwako hata nikasahau kuhusu Mungu, Uliponifahamu kwa mara ya kwanza, nilikuwa na Mungu, ulinichumbia na tukaoana na nikaacha kila jambo kwa sababu nilitaka ndoa yetu ifanikiwe, Ndoa yetu ikawa Mungu ninayemuabudu badala ya Baraka niliyonayo katika Mungu, Ndoa yetu inavunjika kwa sababu yako ila uhusiano wangu na Mungu bado ni imara” alisugua sufuria kisha akaongeza “Umechagua kuitelekeza ndoa yetu ila hilo halimaanishi dunia yote imesambaratika nitaendelea kuwa mama mzuri kwa watoto wetu, hawatosema kamwe kuwa matatizo kati ya mama na baba yalimbadili mama kuwa kiumbe katili, wewe fanya upendavyo na hao wanawake wengine mimi nitawakuza watoto wetu,” alinitazama usoni na kuniambia “je ninakuchukia? Hapana itakuwa uwongo nikisema ninakuchukia, Wewe ndiye mwanaume niliyeolewa naye, niliyeweka naye nadhiri za ndoa, ninayekupenda” machozi yalitiririka mashavuni mwake, aliyafuta na kuendelea “Siwezi kufuta miaka yote tuliyoishi pamoja, Biblia inatutaka tuwapende hata adui zako, Iwapo ninaweza kuwapenda adui zangu, hakika ninaweza kuendelea kukupenda licha ya yote uliyofanya. Nina hasira na nimevunjika moyo, ila nimerejesha nguvu yangu. Ninaishi kwa ajili ya Mungu aliyenibariki sana, siyo kwa ajili yako na maumivu unayonisababishia” alikausha mikono yake na kuniambia “Katika Amani yangu ninapanga ni mahali gani mimi na watoto tutahamia, kwa sababu umeamua kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine, umetuonyesha wazi kuwa hautuhitaji, hivyo hatutoyafanya maisha yako magumu/mabaya kwa kukulazimisha uishi nasi, inabidi uwe na uhuru wa kumleta mwanamke huyo katika nyumba yako. Nilikuwa katika nyumba hii kwa Amani na nitaondoka kwa Amani, hutoua tabasamu langu na nuru yangu” ndivyo alivyohitimisha na kwenda chumbani. Uuuuwi Mungu wangu nipe nguvu. Nilimfuata chumbani nilimkuta ameshaanza kusinzia nilimuamsha na kumwangukia mke wangu na kusema “tafadhali mke wangu nisamehe sana wewe na wanangu nimewakosea, nimewatenda, nikawa chukizo mbele yenu, tafadhali msiondoke, msihame, sitokuumiza tena, sikuwa na uhusiano tena nje ya ndoa, siko sawa nahitaji Amani uliyonayo.


UPENDO UNA NGUVU HATA KUNYENYEKESHA MIOYO INAYOJIVUNA SANA

Ila kuwa mwangalifu mkuu hao wanabadillka Kama taa za barabarani Kama unajua saikolojia hatokusumbua lakini,Tukisungumzia wife material huyo ndiyo mfano
 
...si mchezo dia mbele ya kumkosa mama watoto, teh!
Teh si wanajifanyaga wao michepuko ni nature yao, angehamia kwa mcheps sasa. Chezea mke wa viwango wewe, unajirudi mwenyewe yamekushuka shuuu
 
  • Thanks
Reactions: kui
Dah, kaka hongera kwa mkeo kuwa na madhabahu ya maombi na yenye kumtegemea Mungu. Hongera na pongezi kama umeomba msamaha wa dhati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom