Samahani kama itawakwaza

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
pastor: every thing come from above
jamaa: vitu vyote huja juujuu
pastr: when we look today
jamaa: ni lini tutaangalia leo
pastr:we notice everywhere
jamaa: twabandika ilani kila mahali
pastr:it is apparent that
jamaa: hata huyo ni mzazi tu
pastr:things have changed
jamaa: vitu hugeuzwa geuzwa
pastr:remember faith is your pillar
jamaa:kumbuka kuuamini mlingoti wako
pastr:kip it first and above
jamaa: kumbuka kuuweka juu
pastr: let it run deep and strong
jamaa:ndo kisha uukimbize ndani kabisa tena kwa nguvu
pasta anamaliza somo watu wanaguna tu
 
Jamaa kaenda kwa mchungaji kutubu dhambi!
Mchungaji:kiri dhambi zako mwenyewe nikutubishe.
Jamaa:mchungaji mimi nimefanya dhambi ya uzinzi na wanawake wengi kanisani
Mchu:wataje kwa majina ili nao wajue dhambi zao na niwatubishe
Jamaa:naona aibu sana
Mchu:sasa chakufanya ili usione aibu,tutaenda kukaa mbele ya geti wanapoingilia waumini,mda wa mafunzo ya
kwaya ukifika utaona wanaanza kuingia,akikatiza mwanamke ambaye ulizini naye we sema ''pauuuu''
Jamaa:sawa mchungaji.

Anaingia msichana wa kwanza,jamaa anasema ''pau''
mchungaji:umesamehewa
Anakatiza msichana wa pili jamaa anasema ''pauuu'
Mchu:umesamehe
Anakatiza wa tatu jamaa 'pau''
mchungaji:umesamehewa
Anapita wa nne jamaa ''pauuu''
Mchungaji:umesamehewa
Akapita kwaya master jamaa "pauu"
Mchg:umesamehewa
Akakatiza mke wa mchungaji Jamaa ''Pauuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu'''
Mchu;Toka pepo mchafu,kwa hilo''hujasamehewaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa'''
 
demu wako anapita: pauuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
 
Bora mimi napelekaga sala zangu moja kwa moja kwa Mungu,hawa watendaji wa dini wengine mhh
hivi ukiomba msamaha mwenyewe kwa Mungu bila kupita kwa wahusika wa dini Mungu anasikia maombi?
 
hivi ukiomba msamaha mwenyewe kwa Mungu bila kupita kwa wahusika wa dini Mungu anasikia maombi?

naamini hivyo.Hizi ni taratibu za madhehebu tu binadamu walivojipangia na wala sio utaratibu wa Mungu.
Kwa mfano kwa wakatoliki ni mpaka uende ukatubu kwa padri au askofu.
Lakini kwa sisi walokole hamna hiyo hata ukipiga magoti chumbani kwako ukaomba Mungu anasikia vilevile.
 
hapo bado siamini,kuna makanisa ya kilokole unakuta watu mpaka wanatoa unabii kwamba flani umetenda dhambi,
umeshawahi kusikia utaratibu wa kutengwa kwa mda kwenye makanisa ya kilokole?
 
hapo bado siamini,kuna makanisa ya kilokole unakuta watu mpaka wanatoa unabii kwamba flani umetenda dhambi,
umeshawahi kusikia utaratibu wa kutengwa kwa mda kwenye makanisa ya kilokole?

hehe nishawahi kusikia na kushuhudia pia.Acha nikueleze kuna dhambi nyingi mimi naongelea dhambi zangu binafsi,ambazo roho yangu inanisuta kuwa nimemkosea Mungu wangu.Lakini kuna dhambi za jamii zile za kuwagusa direct watu wengine.
Kama kuzini na mke wa mtu, kutukana mtu,na mengineyo hayo ndo mpaka ukae na viongozi muongee,ukiri makosa na uombe msamaha!
Listen,na hapa sio kwamba unaomba wakusaidie kukuombea msamaha kwa Mungu hapana hapa ni kujiwekea uhusiano mzuri baina yako na wewe.Ni kama wewe ukimkosea baba excellent na ukaenda kumuomba msamaha,
Upoo??
 
labda tuseme zile dhambi ambazo huzijui kama umezitenda ,ila unazozijua huwa hata ukijombea msamaha roho inakushitaki
 
Back
Top Bottom