Samahani Hasheem Thabit na Flavian Matata

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
Samahani kwa "Celebrities" Hasheem Thabit na F.Matata

Nikiwa kama mwana JF mzoefu,niliyeanza kuperuzi JF mwanzoni mwa mwaka 2008 na baadae kuwa "member" rasmi miaka michache baadae sijawahi kuonywa au kufungiwa kwa uvunjifu wa sheria na taratibu za JF.Mara zote nimekuwa nikiandika kitu kwa umakini bila kuvunja sheria na kumuharibia mtu haiba yake.

Kama Jukwaa la Watu maarufu,siku kadhaa zilizopita nilileta uzi hapa wa picha ya Hasheem na F.Matata,ambayo Matata alikuwa ameweka kama TBT,namna wachangiaji walivyoipokea na kuchangia ilivuka mipaka na kuwadhalilisha wahusika

Hali hii imesababisha maombi ya kuutoa uzi huo kwa "DEFAMATION REASONS",nichukuwe nafasi hii kuwataka rashi hawa watu wawili,lengo langu halikuwa kudhalilisha bali ni ku-share habari na wana JF wenzangu

Napokea "kosa" hili kwa unyenyekevu mkubwa,mimi barafu wa JF ninaomba radhi kwa "usumbufu" wowote uliotikana na maneno ya wachangiaji wa picha ile maana mimi ndio niliileta.

Mwisho nawashukuru @Moderators kwa umakini wao.Tuzidi kuidumisha JamiiForums kwa amani na upendo
 
Pole kwa wahusika walioumizwa na uzi huo... Haina haja ya ku review yaliyochangiwa na wana JF hapa maana itakuwa ni kutibua donda. Maadam umewaomba radhi nadhani watakuwa wemepokea... So far kuna gharama kuwa super star maana your life profile is on air and people will say anything good or bad as long as they talk about you... Poleni Hasheem, Poleni Jokate, Poleni Matata na wengine wote mliozungumziwa kwa namna ya kuumiza mtima...
 
Nasikia na Wakinga wanasema uwaombe msamaha kwa sababu ulisema matajiri wao wanashindia sayona na andazi
Ha ha ha ha ha kumbe unanifuatilia??We ni Mkinga nini!??Asee ile ni ukweli mkuu,Sayona na Juice Cola,ukimix inajaa kindoo cha lita kumi

Hapa unanitafutia ugomvi na jamaa anaitwa Bega kwa Bega na Lusajo11
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom