Sam Mahela, Adui mkubwa wa Ibada si Shetani, bali ni Ria

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
MAHELA......jpg

Naandika haya baada ya kuona picha ya Sam Mahela mtangazaji wa ITV ikimuonesha yupo kanisani katikati dimbwi la maombi huku picha ikionesha hisia zake, unyenyekevu wake na utiifu wake mbele za Mungu. Sijui Sam kwa kuweka ile picha anataka kupeleka ujumbe gani kwa marafiki na mshabiki wake, sitaki kujishughulisha na ujumbe huo bali mimi leo nataka kujishughulisha na adabu za kanisani na katika majumba mengine ya kiibada.

Awali ya yote, maana ya neno "ria" maana yake kufanya jambo kwaajili ya kutaka kusifiwa au kujionesha. Ili "ria" ibaki kuwa adui mkubwa wa ibada na asiwe shetani, ni lazima pasiwepo na pepo la "ria" kama yangalipo mapepo ya urongo, wizi, uzinzi, ukahaba, tamaa, nk

Ria Bw Yesu kaifafanua katika nafundisho yake na waandishi wamemnukuu mara nyingi BwYesu akikemea "ria" na ya kwamba "ria" humtenganisha mtu na utukufu wa Mungu.

Hebu tusome aya hii.

"Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba."

Mathayo 6:5-8

Andiko hilo linakataza katakata tabia ya kufanya ibada kwa lengo la kujionesha kwamba unamcha mungu au kwa kutafuta sifa kusifiwa,

Katika ndiko hilo neno "chumba" halimaanishi chumba chako unacho lala au chumba chochote, bali humaanisha moyo na unyenyekevu mbele za Mungu. Maana ya chumba inafafanuliwa vizuri kwenye aya zifuatazo

".....Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; "
Mathayo 7:7

Kwahivyo hapa wakristo bisheni(piga hodi), katika mlango wa chumba nanyi mtafunguliwa. Hicho chumba ni utukufu wa Mungu na ni eneo makhusi ambapo roho ya mwanadamu inaweza kuongea na Mungu na Mungu akamsikia mwanadamu bila hata ya kutamka. Eneo hilo linafafanuliwa vizuri na andiko hili..

"Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."

Yohana 6:56

Kumbe kubisha hodi, maana yake ni kula mwili wa Yesu na kunywa damu yake(kumkubali kuwa katumwa na Mungu, na hakuna Mungu wa kweli isipokuwa YEHOVA) na ukibisha hodi hiyo utafunguliwa, ukifunguliwa ndio utakuwa uko ndani ya YESU na YESU anakuwa ndani yako, na YESU pia yupo ndani ya Mungu. Hiyo "ndani ya ndani" ndio UTUKUFU au ENEO makhususi ambalo roho husikizana kwa lugha zao.

Kwasababu hiyo hakuna haja kujionesha kuwa mchamungu au haja ya kuomba au kusali kwa kupiga kelele, bali Mungu husikia na hujua kabla hata hujafikiria kuomba. Pia kusali, kuomba, kumsifu Mungu, kutembea, kulala, kuongea, kufanya kazi, zote hizo ni ibada, lakini kuna ibada za kudhihirisha na kuna ibada za siri

Kuna watu wanadhani Yusu kuwa ndani ya Mungu, na watu kuwa ndani ya Yesu ni mambo ya spot spot, hapana, Yesu anaendelea kusisitiza kuwa hili jambo si la mchezomchezo katika aya hii

"Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. "

Yohana 14:20

"siku ile" wachambuzi wote wa biblia bila kukhitalifiana wamekubaliana ni siku ya hukumu, kwa hivyo, huenda sasa watu wakadhani , "Yesu kuwa ndani yao, na Yesu kuwa ndani ya Mungu" ni jambo tu la masihara kama watu wafanyavyo sasa kwa kupiga picha za self, lakini pale Yesu atakapotenganisha mbuzi na kondoo miongoni mwa kundi lote linalo jinasibu kondoo ndipo hapo watajua kuwa jambo hilo halikuwa masihara bali ni haki na kweli!

Nataka niseme kuwa biblia haijazuia au kukataza watu kukusanyika(kanisa) na kufanya ibada kwa pamoja, kinachokatazwa ni ria, wewe unayepiga picha kanisani na kuja kutuonesha huku mtandaoni ili tukuone wewe ndio mchamungu sana naomba jua fika unakosea, tena unakosea sana.

MWISHO.

Kumekuwa na kawaida hasa kwa wakristo hutumia vibaya maandiko katika kuhalalisha tabia za kizushi zilizotungwa na wazushi ili kuchafua au kuharibu imani asili ya kikristo ambayo YESU MWOKOZI ALIIFUNDISHA. Mathalani mtu akikosolewa haraka, atakuletea andiko hili

"Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."
Mathayo 7:1

Kwa makusudi au bila makusudi wakristo wengi hulitumia vibaya andiko hilo kama kinga ya kukataa kukosolewa. Naomba mjue kuna tafauti kati ya "kuhukumu" na "kukosoa"

Kuhukumu ni njia ya kutoa haki kwa mwenye kuistahili na kuadhibu yule aliyekutwa na hatia kwa mujibu wa sheria. Hukumu hutanguliwa na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili, kupitia ushahidi na hatimaye hufanyika maamuzi yenye kubainisha haki na batili, yaani yenye kumbainisha dhalimu na madhulumu.

Kukosoa ni kitendo cha kumwambia mtu makosa yake, lakini nini maana ya makosa?

Makosa ni wingi wa "kosa" pamoja na maana zingine, lakini neno "kosa" ni kufanya kinyume cha taratibu au kufanya vibaya. Anaye fanya vibaya ni sawa kumkosoa ili asiendelee kufanya vibaya au kukosea, na kumkosoa hakuwezi kuwa hukumu kwake bali ni msaada kwake!

Sam Mahela, mimi ndugu yangu sijakuhukumu bali nimekukosoa, kama vile Yesu alivyotuma wanafunzi wake wakatangaze injili ulimwengu mzima, nami nakutangizia leo. Kutangaza Injili ni kazi ya kukosoa MAKOSA ya watu na kazi ya kuwafanya watu wasije kufanya makosa katika siku zao za usoni.

Makala hii ikufunguwe wewe na watakao isoma hata wasifanye makosa.

Ahsante sana
Rafiki Yako katika BWANA.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Cal/whats app 0622845394 Morgoro
 
Duh, selfie mpaka church
Tazama vidole vilivyoshika simu vina rangi wanayopaka wanawake, je Sam mahela naye anapaka rangi? Hiyo picha inaonekana sio selfie ila ni mwanamke alimpiga kwa ukaribu sana, na kama ni yeye basi tukubaliane kwamba na yeye anapaka kucha zake rangi.
 
Duh, selfie mpaka church
Si kila asemaye bwana yesu asifiwe humaanisha kuwa ni mcha mungu kweli. Imeandikwa Mathayo 24 mstari wa 11, 23 na 24.

Siku za mwisho kutakuwepo na manabii wengi wa uongo na makrusto wa uongo. Nao watakuja kwa jina langu na watadanganya wengi, watakuwa na ishara na miujiza. Jihadharini nao. Basi mkiambiwa kristo yuko huku msisadiki na mkiambiwa yuko Jangwani msitoke.
 
Mkuu huwezi kuwamaliza hao walikuwepo hata nyakatiza agano la kale...Fanya yako utaumia kichwa bure.
 
mimi huwa najiuliza mtu unasali kwa uchungu na makelele yenye machozo kikombe kinajaa alafu hapohapo unajiphoto PC ivi hiyo ni ibada au kujionesha?
 
Nafikiri angepiga selfie akiwa bar angepongezwa........... Nilicho jifunza kwenye maisha, ukifanya jema watasema, ukifanya bays watasema. Kwa hiyo kila mmoja afanye kinacho mpendeza, kikubwa tu asivunje katiba ya Nchi.
 
Tazama vidole vilivyoshika simu vina rangi wanayopaka wanawake, je Sam mahela naye anapaka rangi? Hiyo picha inaonekana sio selfie ila ni mwanamke alimpiga kwa ukaribu sana, na kama ni yeye basi tukubaliane kwamba na yeye anapaka kucha zake rangi.
Mkuu hizo ni picha mbili tofaut ambazo mtoa mada amtumia kufikisha ujumbe wa kujipiga picha na kujionyesha...ya kwanza ni mdada kavaa blue shirt kashika simu anajipiga selfie huku akiabudu.. na si sam...ya pili ni sam kavaa suti...yy hajijipiga selfie bali kapigwa na mpiga picha
 
Naona siku hizi ITV wanajitahidi kumbeba, walianza kumuweka kwenye usomaji wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku kila weekend ya jumapili, naona sasa wameanza kumwinua zaidi anasoma mpaka siku za kazi (jumatatu-ijumaa)
Kama jana Jumatano naona ndiye alishikilia Mike na mbwembwe za kutosha.
 
Mkuu hizo ni picha mbili tofaut ambazo mtoa mada amtumia kufikisha ujumbe wa kujipiga picha na kujionyesha...ya kwanza ni mdada kavaa blue shirt kashika simu anajipiga selfie huku akiabudu.. na si sam...ya pili ni sam kavaa suti...yy hajijipiga selfie bali kapigwa na mpiga picha
Mbona hakuna viashiria vinavyoonesha alipiga na si kwamba alipigwa na mtu tena pengine akowa hajijui?
 
Hiyo ya sam mahela inaonyeshwa ilipigwa akiwa hajui....haya makanisa ya kisasa siki hizi wana mafotografa ndani wanapiga picha sijui sababu ni nini...ndio maana hata huyo dada hapo pemben yuko confident kujiselfisha sababu humo ndani inaonyesha makamera ndio mwake[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
View attachment 425299

Naandika haya baada ya kuona picha ya Sam Mahela mtangazaji wa ITV ikimuonesha yupo kanisani katikati dimbwi la maombi huku picha ikionesha hisia zake, unyenyekevu wake na utiifu wake mbele za Mungu. Sijui Sam kwa kuweka ile picha anataka kupeleka ujumbe gani kwa marafiki na mshabiki wake, sitaki kujishughulisha na ujumbe huo bali mimi leo nataka kujishughulisha na adabu za kanisani na katika majumba mengine ya kiibada.

Awali ya yote, maana ya neno "ria" maana yake kufanya jambo kwaajili ya kutaka kusifiwa au kujionesha. Ili "ria" ibaki kuwa adui mkubwa wa ibada na asiwe shetani, ni lazima pasiwepo na pepo la "ria" kama yangalipo mapepo ya urongo, wizi, uzinzi, ukahaba, tamaa, nk

Ria Bw Yesu kaifafanua katika nafundisho yake na waandishi wamemnukuu mara nyingi BwYesu akikemea "ria" na ya kwamba "ria" humtenganisha mtu na utukufu wa Mungu.

Hebu tusome aya hii.

"Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba."

Mathayo 6:5-8

Andiko hilo linakataza katakata tabia ya kufanya ibada kwa lengo la kujionesha kwamba unamcha mungu au kwa kutafuta sifa kusifiwa,

Katika ndiko hilo neno "chumba" halimaanishi chumba chako unacho lala au chumba chochote, bali humaanisha moyo na unyenyekevu mbele za Mungu. Maana ya chumba inafafanuliwa vizuri kwenye aya zifuatazo

".....Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; "
Mathayo 7:7

Kwahivyo hapa wakristo bisheni(piga hodi), katika mlango wa chumba nanyi mtafunguliwa. Hicho chumba ni utukufu wa Mungu na ni eneo makhusi ambapo roho ya mwanadamu inaweza kuongea na Mungu na Mungu akamsikia mwanadamu bila hata ya kutamka. Eneo hilo linafafanuliwa vizuri na andiko hili..

"Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."

Yohana 6:56

Kumbe kubisha hodi, maana yake ni kula mwili wa Yesu na kunywa damu yake(kumkubali kuwa katumwa na Mungu, na hakuna Mungu wa kweli isipokuwa YEHOVA) na ukibisha hodi hiyo utafunguliwa, ukifunguliwa ndio utakuwa uko ndani ya YESU na YESU anakuwa ndani yako, na YESU pia yupo ndani ya Mungu. Hiyo "ndani ya ndani" ndio UTUKUFU au ENEO makhususi ambalo roho husikizana kwa lugha zao.

Kwasababu hiyo hakuna haja kujionesha kuwa mchamungu au haja ya kuomba au kusali kwa kupiga kelele, bali Mungu husikia na hujua kabla hata hujafikiria kuomba. Pia kusali, kuomba, kumsifu Mungu, kutembea, kulala, kuongea, kufanya kazi, zote hizo ni ibada, lakini kuna ibada za kudhihirisha na kuna ibada za siri

Kuna watu wanadhani Yusu kuwa ndani ya Mungu, na watu kuwa ndani ya Yesu ni mambo ya spot spot, hapana, Yesu anaendelea kusisitiza kuwa hili jambo si la mchezomchezo katika aya hii

"Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. "

Yohana 14:20

"siku ile" wachambuzi wote wa biblia bila kukhitalifiana wamekubaliana ni siku ya hukumu, kwa hivyo, huenda sasa watu wakadhani , "Yesu kuwa ndani yao, na Yesu kuwa ndani ya Mungu" ni jambo tu la masihara kama watu wafanyavyo sasa kwa kupiga picha za self, lakini pale Yesu atakapotenganisha mbuzi na kondoo miongoni mwa kundi lote linalo jinasibu kondoo ndipo hapo watajua kuwa jambo hilo halikuwa masihara bali ni haki na kweli!

Nataka niseme kuwa biblia haijazuia au kukataza watu kukusanyika(kanisa) na kufanya ibada kwa pamoja, kinachokatazwa ni ria, wewe unayepiga picha kanisani na kuja kutuonesha huku mtandaoni ili tukuone wewe ndio mchamungu sana naomba jua fika unakosea, tena unakosea sana.

MWISHO.

Kumekuwa na kawaida hasa kwa wakristo hutumia vibaya maandiko katika kuhalalisha tabia za kizushi zilizotungwa na wazushi ili kuchafua au kuharibu imani asili ya kikristo ambayo YESU MWOKOZI ALIIFUNDISHA. Mathalani mtu akikosolewa haraka, atakuletea andiko hili

"Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."
Mathayo 7:1

Kwa makusudi au bila makusudi wakristo wengi hulitumia vibaya andiko hilo kama kinga ya kukataa kukosolewa. Naomba mjue kuna tafauti kati ya "kuhukumu" na "kukosoa"

Kuhukumu ni njia ya kutoa haki kwa mwenye kuistahili na kuadhibu yule aliyekutwa na hatia kwa mujibu wa sheria. Hukumu hutanguliwa na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili, kupitia ushahidi na hatimaye hufanyika maamuzi yenye kubainisha haki na batili, yaani yenye kumbainisha dhalimu na madhulumu.

Kukosoa ni kitendo cha kumwambia mtu makosa yake, lakini nini maana ya makosa?

Makosa ni wingi wa "kosa" pamoja na maana zingine, lakini neno "kosa" ni kufanya kinyume cha taratibu au kufanya vibaya. Anaye fanya vibaya ni sawa kumkosoa ili asiendelee kufanya vibaya au kukosea, na kumkosoa hakuwezi kuwa hukumu kwake bali ni msaada kwake!

Sam Mahela, mimi ndugu yangu sijakuhukumu bali nimekukosoa, kama vile Yesu alivyotuma wanafunzi wake wakatangaze injili ulimwengu mzima, nami nakutangizia leo. Kutangaza Injili ni kazi ya kukosoa MAKOSA ya watu na kazi ya kuwafanya watu wasije kufanya makosa katika siku zao za usoni.

Makala hii ikufunguwe wewe na watakao isoma hata wasifanye makosa.

Ahsante sana
Rafiki Yako katika BWANA.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Cal/whats app 0622845394 Morgoro

Mkuu Dotto
Mimi sijaelewa maana ya uzi huu. Kwanza aliyepiga picha ni huyo mwana mama, Sasa tatizo lipo wapi.
 
Hiyo ya sam mahela inaonyeshwa ilipigwa akiwa hajui....haya makanisa ya kisasa siki hizi wana mafotografa ndani wanapiga picha sijui sababu ni nini...ndio maana hata huyo dada hapo pemben yuko confident kujiselfisha sababu humo ndani inaonyesha makamera ndio mwake[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Anasali kwa gwajima nini?
 
Haya mambo ya imani yamenishinda kabisa! Naona kama watu wanapoteza nguvu na muda wao bure!
 
mahela-jpg.425299

Haya ndo Makanisa ya Upako? Huwa yanaruhusu selfie? Ila Sam atakuwa amepigwa na mtu wala siyo yeye maana yeye kweli yuko kwenye hisia kali sana na hana simu yoyote ambayo kwamba atakuwa amejipiga! Huyu mama kachemsha ile mbaya!!
 
Mhh uzi mreefu kumsema Sam Mahela wkt yeye mwenyewe usikute hajui km amepigwa picha hapo,ungemsema huyo dada hapo sawa aliejiselfisha,au kwasababu Sam maarufu?khaaa
 
View attachment 425299

Naandika haya baada ya kuona picha ya Sam Mahela mtangazaji wa ITV ikimuonesha yupo kanisani katikati dimbwi la maombi huku picha ikionesha hisia zake, unyenyekevu wake na utiifu wake mbele za Mungu. Sijui Sam kwa kuweka ile picha anataka kupeleka ujumbe gani kwa marafiki na mshabiki wake, sitaki kujishughulisha na ujumbe huo bali mimi leo nataka kujishughulisha na adabu za kanisani na katika majumba mengine ya kiibada.

Awali ya yote, maana ya neno "ria" maana yake kufanya jambo kwaajili ya kutaka kusifiwa au kujionesha. Ili "ria" ibaki kuwa adui mkubwa wa ibada na asiwe shetani, ni lazima pasiwepo na pepo la "ria" kama yangalipo mapepo ya urongo, wizi, uzinzi, ukahaba, tamaa, nk

Ria Bw Yesu kaifafanua katika nafundisho yake na waandishi wamemnukuu mara nyingi BwYesu akikemea "ria" na ya kwamba "ria" humtenganisha mtu na utukufu wa Mungu.

Hebu tusome aya hii.

"Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba."

Mathayo 6:5-8

Andiko hilo linakataza katakata tabia ya kufanya ibada kwa lengo la kujionesha kwamba unamcha mungu au kwa kutafuta sifa kusifiwa,

Katika ndiko hilo neno "chumba" halimaanishi chumba chako unacho lala au chumba chochote, bali humaanisha moyo na unyenyekevu mbele za Mungu. Maana ya chumba inafafanuliwa vizuri kwenye aya zifuatazo

".....Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; "
Mathayo 7:7

Kwahivyo hapa wakristo bisheni(piga hodi), katika mlango wa chumba nanyi mtafunguliwa. Hicho chumba ni utukufu wa Mungu na ni eneo makhusi ambapo roho ya mwanadamu inaweza kuongea na Mungu na Mungu akamsikia mwanadamu bila hata ya kutamka. Eneo hilo linafafanuliwa vizuri na andiko hili..

"Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."

Yohana 6:56

Kumbe kubisha hodi, maana yake ni kula mwili wa Yesu na kunywa damu yake(kumkubali kuwa katumwa na Mungu, na hakuna Mungu wa kweli isipokuwa YEHOVA) na ukibisha hodi hiyo utafunguliwa, ukifunguliwa ndio utakuwa uko ndani ya YESU na YESU anakuwa ndani yako, na YESU pia yupo ndani ya Mungu. Hiyo "ndani ya ndani" ndio UTUKUFU au ENEO makhususi ambalo roho husikizana kwa lugha zao.

Kwasababu hiyo hakuna haja kujionesha kuwa mchamungu au haja ya kuomba au kusali kwa kupiga kelele, bali Mungu husikia na hujua kabla hata hujafikiria kuomba. Pia kusali, kuomba, kumsifu Mungu, kutembea, kulala, kuongea, kufanya kazi, zote hizo ni ibada, lakini kuna ibada za kudhihirisha na kuna ibada za siri

Kuna watu wanadhani Yusu kuwa ndani ya Mungu, na watu kuwa ndani ya Yesu ni mambo ya spot spot, hapana, Yesu anaendelea kusisitiza kuwa hili jambo si la mchezomchezo katika aya hii

"Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. "

Yohana 14:20

"siku ile" wachambuzi wote wa biblia bila kukhitalifiana wamekubaliana ni siku ya hukumu, kwa hivyo, huenda sasa watu wakadhani , "Yesu kuwa ndani yao, na Yesu kuwa ndani ya Mungu" ni jambo tu la masihara kama watu wafanyavyo sasa kwa kupiga picha za self, lakini pale Yesu atakapotenganisha mbuzi na kondoo miongoni mwa kundi lote linalo jinasibu kondoo ndipo hapo watajua kuwa jambo hilo halikuwa masihara bali ni haki na kweli!

Nataka niseme kuwa biblia haijazuia au kukataza watu kukusanyika(kanisa) na kufanya ibada kwa pamoja, kinachokatazwa ni ria, wewe unayepiga picha kanisani na kuja kutuonesha huku mtandaoni ili tukuone wewe ndio mchamungu sana naomba jua fika unakosea, tena unakosea sana.

MWISHO.

Kumekuwa na kawaida hasa kwa wakristo hutumia vibaya maandiko katika kuhalalisha tabia za kizushi zilizotungwa na wazushi ili kuchafua au kuharibu imani asili ya kikristo ambayo YESU MWOKOZI ALIIFUNDISHA. Mathalani mtu akikosolewa haraka, atakuletea andiko hili

"Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."
Mathayo 7:1

Kwa makusudi au bila makusudi wakristo wengi hulitumia vibaya andiko hilo kama kinga ya kukataa kukosolewa. Naomba mjue kuna tafauti kati ya "kuhukumu" na "kukosoa"

Kuhukumu ni njia ya kutoa haki kwa mwenye kuistahili na kuadhibu yule aliyekutwa na hatia kwa mujibu wa sheria. Hukumu hutanguliwa na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili, kupitia ushahidi na hatimaye hufanyika maamuzi yenye kubainisha haki na batili, yaani yenye kumbainisha dhalimu na madhulumu.

Kukosoa ni kitendo cha kumwambia mtu makosa yake, lakini nini maana ya makosa?

Makosa ni wingi wa "kosa" pamoja na maana zingine, lakini neno "kosa" ni kufanya kinyume cha taratibu au kufanya vibaya. Anaye fanya vibaya ni sawa kumkosoa ili asiendelee kufanya vibaya au kukosea, na kumkosoa hakuwezi kuwa hukumu kwake bali ni msaada kwake!

Sam Mahela, mimi ndugu yangu sijakuhukumu bali nimekukosoa, kama vile Yesu alivyotuma wanafunzi wake wakatangaze injili ulimwengu mzima, nami nakutangizia leo. Kutangaza Injili ni kazi ya kukosoa MAKOSA ya watu na kazi ya kuwafanya watu wasije kufanya makosa katika siku zao za usoni.

Makala hii ikufunguwe wewe na watakao isoma hata wasifanye makosa.

Ahsante sana
Rafiki Yako katika BWANA.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Cal/whats app 0622845394 Morgoro
ayseee.......tunahitaji walimu km wewe!! UMENIFUNZA JAMBO KUBWA!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom