Salum Mwalimu: Tumemaliza wiki Tundu Lissu akipigania uhai wake kitandani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
TUMEMALIZA WIKI TUNDU LISSU AKIPIGANIA UHAI WAKE KITANDANI

Naliona tabasamu lenye kila aina ya dalili ya kujiamini likipamba sura ya mtu anayetambua nini anachokifanya, jasiri, shupavu mwenye kila sifa anayostahili kuwa nayo mpambanaji.

Naiona sura hiyo ilivyojaa bashasha ikipambwa na umbo lililoshiba akitembea kwa kujiamini mikononi akiwa amebeba mkoba uliyosheni vitabu vya kusemea wanyonge kupata haki zao mbele ya vyombo vya kutafsiri sheria.

Naiona taswira hiyo ikitembea kutoka nje ya jengo la mahakama, utitiri wa vyombo vya habari vikisubiri kunasa kauli ya kishujaa na ya haki.

Huyo ni Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Wakili na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika.

Tumemaliza wiki sasa tangu jemedari Lissu akumbwe na shambulio la kihuni lililolenga kukatisha uhai wake nyumbani kwake Mjini Dodoma, akiwa katika majukumu yake ya kutetea wanyonge na nchi yake kupitia sauti yake Bungeni.

Shambulio hili la kihuni lililofanywa na kuratibiwa na watu waoga, waliojaa hofu, wasiojimini limetekelezwa mchana kweupe tena katika makazi yaliyokuwa yakiaminiwa kuwa ni salama kutoka na aina ya watu wanaoishi hapo.

Ni shambulizi la kisiasa dhidi ya mtu aliyejipambanua na kuonesha uthubutu,ujasiri na utayari wa hali ya juu wa kukosoa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais John Magufuli, akiwakosoa pia hadharani wale wasiopenda demokrasia ikue nchini, wasiopenda kusikia ukweli na kuona desturi ya maisha ya kidemokrasia ikishamiri nchini.

Ni wiki sasa Lissu yupo kitandani akipigania uhai wake, hali yake bado hairidhishi, ameumia, amejeruhiwa sana,

Nimesema tangu siku ya kwanza tukio lilipotokea kwamba kamwe haitoiniingia akilini kuamini kwamba eti shambulio dhidi ya Lissu kuwa ni la kijambazi,kigaidi au la kimapenzi, nimekataa na nitaendelea kukataa, shambulio dhidi ya Lissu ni la kisiasa, narudia tena ni la kisiasa.

Tumeanza kuona sarakasi za vyombo vya dola vikihangaika, ni kupoteza wakati na pengine hadaa mbele ya mioyo inayolia machozi ya damu ya mamilioni ya wanadamu dunia nzima ikimlilia mtu wanayempenda sio kwa jina wala vyeo vyake bali kwa sifa zake za kusema kweli na utayari wake wa kutetea haki na demokrsana.

Sintoshangaa hata kidogo kwamba watekelezaj wa jambo hili wakijipa tumaini "mfu" kwamba wakati utapita na kwamba hili la Lissu nalo eti litasahaulika kama yalivyosahaulika au kufifia kwa matukio mengine ikiwemo la mauaji ya kishenzi ya aliyekuwa Mwenyekiti wetu wa Chadema mkoa wa Geita Kamanda Alphonce Mawazo. Huko ni kujidanganya, hili la Lissu halitoisha, halitosahaulika na kamwe halitoachwa hivihivi.

Damu iliyomwagika ya Lissu itatiririka pasi na kukauka kuelekea katika mbegu za mabadiliko katika nchi hii, si ukame wala uharibu wowote wa mazingira utakaokausha mfereji wa damu ya Lissu zilipo mbegu hizo, ni vema watesi wa Lissu wakatambua hilo, haitojalisha utayari wala uhodari wa chombo chochote kile kusimama na kuuelezea umma ukweli juu ya jambo hili, ni wakati pekee ndio utakaaonesha umahiri wa kufichua na kuwaadhibu watesi wa Lissu.

Kwa kuwa walikifanya kitendo hicho kwa kujiamini mno mchana kweupe pengine wakiringia nguvu,kiburi na jeuri (iwe ya kifedha, silaha,madaraka,mtandao nk) nami naamini wakati utawaumbua watesi wa Lissu na maadui wa demokrasia nchini mchana kweupe.

Lissu yupo kitandani, kazi kubwa iliyofanywa na kupewa kipaumbele ni kupigania pumzi yake, tunamshukuru Mungu hilo tumelifanikisha. Lissu yupo katika mikono inayotupa imani kuwa ni salama.

Natambua wapo wanaoomba usiku na mchana kuona Chadema na familia ya Lissu ikiadhirika kwa kushindwa kugharamia matibabu yake nchini Kenya na hivyo maisha yake kuwa hatarini, ni kweli mzigo wa gharama ni mkubwa tena ni mkubwa sana, lakini kwetu fedha si kitu kuzidi thamani ya uhai wa Lissu kwa nchi yetu, tutapigania uhai wake kwa nguvu zetu zote. Dhamira njema tuliyonayo itatupatia ushindi.

Juhudi hizi watanzania na wapenda haki ulimwenguni kote wanaziona na wameziunga mkono, ni imani yangu kwamba kila mmoja atakuwa mshirika muhimu katika kuchangia juhudi za kupigania uhai wa Lissu.

Hali yake bado sio nzuri sana, taarifa zinazohusu matibabu yake hazitoi matumaini kwamba tumtarajie hivi karibuni na atakuwa katika hali gani, huenda matibabu yake yakachukua muda kidogo, hiyo maana yake ni kuendelea kuwepo Hospitalini na hivyo kuhitajika kwa fedha zaidi kugharamia matibabu hayo, kila mmoja ahamasike na kumhamasisha na mwengine kutoa chochote alichonacho kupigania pumzi ya Lissu.

Lissu alipolala kitandani anatudai, alipokuwa mzima mwenye afya yake alisema na kututetea kila mahali kuanzia mahakamani, Bungeni, vijiweni, mitaani na kwengineko, alipaza sauti yake bila woga,kutetea haki ya kila mmoja kuanzia walimu, wanasiasa, wawekezaji, wafanyabiashara, watumishi na wengine hakuwa anapigania haki zake wala za familia yake, alikuwa anapigania haki zetu sisi wanyonge, aliamua kuwa msemaji wa kila mmoja, hakuogopa alitumia rasilimali zake zote, hakutudai malipo, huu ni wakati wetu sisi kupigania haki yake ya kuishi, tujitoe kwa hali na mali ili anyayuke tumpe furaha moyoni mwake na tuzime furaha ya watesi wake.

Namshukuru sana Mungu kwa kuonesha kudura zake kuzikwepesha risasi kukatisha pumzi za Lissu, wote tumemnyanyua mikono kumshukuru, ametenda yake nasi ndugu, jamaa na marafiki wa Lissu tutende yetu.

Huenda jaribio hili pamoja na kulenga kuondoa uhai wake, huenda waliotenda wanadhani kwa kufanya hivyo wangeingiza hofu na woga katika mioyo yetu, kutuziba midomo na kuturudisha nyuma kusudi wazime harakati za kutafuta mabadiliko katika nchi yetu. Huko ni kujidanganya, tukio la kumshambulia Lissu kwa lengo la kumuua limetuongezea nguvu na ujasiri wa mapambano, hatutonyamaza, tutasema,tutakosoa na tutapinga na tunaimani siku za ushindi zimekaribia.

Naisubiri siku Lissu atakayokuwa akirejea nchini, haitojalisha atakuwa akitembelea magongo, kiti cha magurudumu matatu cha wagonjwa(wheel chair) au akitembea kwa miguu yake wima, siku hiyo ndipo watesi wake watakapopata salaam za watanzania.

Mwanadamu huzaliwa siku moja na hufa siku moja, hayupo anaezaliwa siku zaidi ya moja wala kufa siku zaidi ya moja, na hayupo anaetumie roho ya mwenzie kama roho ya ziada.

Aluta Kontinua!
Salum Mwalim,
Naibu Katibu Mkuu
Chadema, Zanzibar.
September 14, 2017.
 
.Damu iliyomwagika ya Lissu itatiririka pasi na kukauka kuelekea katika mbegu za mabadiliko katika nchi hii, si ukame wala uharibu wowote wa mazingira utakaokausha mfereji wa damu ya Lissu zilipo mbegu hizo, ni vema watesi wa Lissu wakatambua hilo, haitojalisha utayari wala uhodari wa chombo chochote kile kusimama na kuuelezea umma ukweli juu ya jambo hili, ni wakati pekee ndio utakaaonesha umahiri wa kufichua na kuwaadhibu watesi wa Lissu.
 
Watu waliufyata na wakapotea kwa Muda kwny Ulingo wa Siasa!
Hujuma dhidi ya Lissu imegeuza Viongozi wote kuwa wasemaji wake kila Mtu Ana post kuelezea Hali ya Afya yake, Hongereni Makamanda
 
.
Amen....

Mungu ni mwema sana, siku zote ni mwema!!

Atatembea kwa miguu yake, na tutalipia matibabu yake kwa sumuni sumuni hizi hizi tutakazochanga...!!
Pia imeibua washahiri, waandishi, wengine wameheuka wacha Mungu.. Mwisho wa siku dhambi ya usaliti wa taifa la wanyonge haijawahi kumuacha mtu salama..
 
Asante kwa maoni yako, karibu tena wakati mwingine...

Hii ndiyo hasa maana ya "freedom of expression"...

Sijui ni kwa nini tu Rais mwoga Bw. John Pombe Magufuli anahofu na watu kama ninyi wakati hamna madhara yoyote....!!

Mr Pombe Magufuli, stop running from your own shadow.... Be bold

People like Sheiza are not to be feared...., let them spit out whatever they have....
 
TUMEMALIZA WIKI TUNDU LISSU AKIPIGANIA UHAI WAKE KITANDANI

Naliona tabasamu lenye kila aina ya dalili ya kujiamini likipamba sura ya mtu anayetambua nini anachokifanya, jasiri, shupavu mwenye kila sifa anayostahili kuwa nayo mpambanaji.

Naiona sura hiyo ilivyojaa bashasha ikipambwa na umbo lililoshiba akitembea kwa kujiamini mikononi akiwa amebeba mkoba uliyosheni vitabu vya kusemea wanyonge kupata haki zao mbele ya vyombo vya kutafsiri sheria.

Naiona taswira hiyo ikitembea kutoka nje ya jengo la mahakama, utitiri wa vyombo vya habari vikisubiri kunasa kauli ya kishujaa na ya haki.

Huyo ni Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Wakili na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika.

Tumemaliza wiki sasa tangu jemedari Lissu akumbwe na shambulio la kihuni lililolenga kukatisha uhai wake nyumbani kwake Mjini Dodoma, akiwa katika majukumu yake ya kutetea wanyonge na nchi yake kupitia sauti yake Bungeni.

Shambulio hili la kihuni lililofanywa na kuratibiwa na watu waoga, waliojaa hofu, wasiojimini limetekelezwa mchana kweupe tena katika makazi yaliyokuwa yakiaminiwa kuwa ni salama kutoka na aina ya watu wanaoishi hapo.

Ni shambulizi la kisiasa dhidi ya mtu aliyejipambanua na kuonesha uthubutu,ujasiri na utayari wa hali ya juu wa kukosoa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais John Magufuli, akiwakosoa pia hadharani wale wasiopenda demokrasia ikue nchini, wasiopenda kusikia ukweli na kuona desturi ya maisha ya kidemokrasia ikishamiri nchini.

Ni wiki sasa Lissu yupo kitandani akipigania uhai wake, hali yake bado hairidhishi, ameumia, amejeruhiwa sana,

Nimesema tangu siku ya kwanza tukio lilipotokea kwamba kamwe haitoiniingia akilini kuamini kwamba eti shambulio dhidi ya Lissu kuwa ni la kijambazi,kigaidi au la kimapenzi, nimekataa na nitaendelea kukataa, shambulio dhidi ya Lissu ni la kisiasa, narudia tena ni la kisiasa.

Tumeanza kuona sarakasi za vyombo vya dola vikihangaika, ni kupoteza wakati na pengine hadaa mbele ya mioyo inayolia machozi ya damu ya mamilioni ya wanadamu dunia nzima ikimlilia mtu wanayempenda sio kwa jina wala vyeo vyake bali kwa sifa zake za kusema kweli na utayari wake wa kutetea haki na demokrsana.

Sintoshangaa hata kidogo kwamba watekelezaj wa jambo hili wakijipa tumaini "mfu" kwamba wakati utapita na kwamba hili la Lissu nalo eti litasahaulika kama yalivyosahaulika au kufifia kwa matukio mengine ikiwemo la mauaji ya kishenzi ya aliyekuwa Mwenyekiti wetu wa Chadema mkoa wa Geita Kamanda Alphonce Mawazo. Huko ni kujidanganya, hili la Lissu halitoisha, halitosahaulika na kamwe halitoachwa hivihivi.

Damu iliyomwagika ya Lissu itatiririka pasi na kukauka kuelekea katika mbegu za mabadiliko katika nchi hii, si ukame wala uharibu wowote wa mazingira utakaokausha mfereji wa damu ya Lissu zilipo mbegu hizo, ni vema watesi wa Lissu wakatambua hilo, haitojalisha utayari wala uhodari wa chombo chochote kile kusimama na kuuelezea umma ukweli juu ya jambo hili, ni wakati pekee ndio utakaaonesha umahiri wa kufichua na kuwaadhibu watesi wa Lissu.

Kwa kuwa walikifanya kitendo hicho kwa kujiamini mno mchana kweupe pengine wakiringia nguvu,kiburi na jeuri (iwe ya kifedha, silaha,madaraka,mtandao nk) nami naamini wakati utawaumbua watesi wa Lissu na maadui wa demokrasia nchini mchana kweupe.

Lissu yupo kitandani, kazi kubwa iliyofanywa na kupewa kipaumbele ni kupigania pumzi yake, tunamshukuru Mungu hilo tumelifanikisha. Lissu yupo katika mikono inayotupa imani kuwa ni salama.

Natambua wapo wanaoomba usiku na mchana kuona Chadema na familia ya Lissu ikiadhirika kwa kushindwa kugharamia matibabu yake nchini Kenya na hivyo maisha yake kuwa hatarini, ni kweli mzigo wa gharama ni mkubwa tena ni mkubwa sana, lakini kwetu fedha si kitu kuzidi thamani ya uhai wa Lissu kwa nchi yetu, tutapigania uhai wake kwa nguvu zetu zote. Dhamira njema tuliyonayo itatupatia ushindi.

Juhudi hizi watanzania na wapenda haki ulimwenguni kote wanaziona na wameziunga mkono, ni imani yangu kwamba kila mmoja atakuwa mshirika muhimu katika kuchangia juhudi za kupigania uhai wa Lissu.

Hali yake bado sio nzuri sana, taarifa zinazohusu matibabu yake hazitoi matumaini kwamba tumtarajie hivi karibuni na atakuwa katika hali gani, huenda matibabu yake yakachukua muda kidogo, hiyo maana yake ni kuendelea kuwepo Hospitalini na hivyo kuhitajika kwa fedha zaidi kugharamia matibabu hayo, kila mmoja ahamasike na kumhamasisha na mwengine kutoa chochote alichonacho kupigania pumzi ya Lissu.

Lissu alipolala kitandani anatudai, alipokuwa mzima mwenye afya yake alisema na kututetea kila mahali kuanzia mahakamani, Bungeni, vijiweni, mitaani na kwengineko, alipaza sauti yake bila woga,kutetea haki ya kila mmoja kuanzia walimu, wanasiasa, wawekezaji, wafanyabiashara, watumishi na wengine hakuwa anapigania haki zake wala za familia yake, alikuwa anapigania haki zetu sisi wanyonge, aliamua kuwa msemaji wa kila mmoja, hakuogopa alitumia rasilimali zake zote, hakutudai malipo, huu ni wakati wetu sisi kupigania haki yake ya kuishi, tujitoe kwa hali na mali ili anyayuke tumpe furaha moyoni mwake na tuzime furaha ya watesi wake.

Namshukuru sana Mungu kwa kuonesha kudura zake kuzikwepesha risasi kukatisha pumzi za Lissu, wote tumemnyanyua mikono kumshukuru, ametenda yake nasi ndugu, jamaa na marafiki wa Lissu tutende yetu.

Huenda jaribio hili pamoja na kulenga kuondoa uhai wake, huenda waliotenda wanadhani kwa kufanya hivyo wangeingiza hofu na woga katika mioyo yetu, kutuziba midomo na kuturudisha nyuma kusudi wazime harakati za kutafuta mabadiliko katika nchi yetu. Huko ni kujidanganya, tukio la kumshambulia Lissu kwa lengo la kumuua limetuongezea nguvu na ujasiri wa mapambano, hatutonyamaza, tutasema,tutakosoa na tutapinga na tunaimani siku za ushindi zimekaribia.

Naisubiri siku Lissu atakayokuwa akirejea nchini, haitojalisha atakuwa akitembelea magongo, kiti cha magurudumu matatu cha wagonjwa(wheel chair) au akitembea kwa miguu yake wima, siku hiyo ndipo watesi wake watakapopata salaam za watanzania.

Mwanadamu huzaliwa siku moja na hufa siku moja, hayupo anaezaliwa siku zaidi ya moja wala kufa siku zaidi ya moja, na hayupo anaetumie roho ya mwenzie kama roho ya ziada.

Aluta Kontinua!
Salum Mwalim,
Naibu Katibu Mkuu
Chadema, Zanzibar.
September 14, 2017.
Mungu mponye lissu ili angalau aonje matunda ya uzalendo ambao ameupigania kwa miaka mingi hapa nchini dhidi ya dhuluma, long live Tundu Lissu
 
Ma
Mungu mpe Lisu uponyaji wa haraka. Amina
Magu kwa weledi wa Tundu Lisu ni hazina ambayo kama nchi zingine za duniani zilizoendelea zingemthamini haijalishi kua upande wa upinzani kwani kwa kukosoa na kushauri upande wa sheria mbalimbali za nchi tungepiga hatua sana.sasa kinyume chake mliona.. wivu hadi kumimina risasi nyingi ili afutike kwenye uso wa dunia hata hivyo mwenyezi mungu muumba amekataa matakwa yenu ameepusha risasi zisimuue je mna la kujifunza hapo?ewe Dab aka makonda nilikuona pale jumba kuu siku ya kuapishwa jaji ulivyokua umekosa amani,na kwa sasa waliowengi wanafahamu sasa uhusiano wako wa karibu na mkubwa kumbe ni kutekeleza mipango ya kueliminate watu wanaosema ukweli kweli mtupu niwaulize sasa je mpo kwa ajili ya wananchi wa tanzania au kwa ajili yenu tu?je katiba inasemaje juu ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni?
 
Sio kifo cha Alphonce Mawazo tu, hata kupotea kwa Ben Saanane, Kifo cha chacha Wangwe, Na majeraha yote aliyoyapata dr.Slaa katika kukijenga chama hiki vyote hatuwezi kuvisahau.
Tukio la fursa limegeuka fursa ya kila kiongozi wa chama kufurukuta ili na yeye aonekane yupo, Msigwa na Lema tuliwasahau kabisa, Kuna watu machoni na midomoni wanaonekana kusononeka lakini kimoyo moyo kutokea kwa hili tatizo wanamshukuru Mungu, Wanasema kufa kufaana. Chadema sio kwamba hamna la kujifunza kutoka kwa chama tawala, kueshimu mamlaka na majukumu ya kila kiongozi ni muhimu kwa chama chochote cha siasa ambacho kina malengo ya kushika dola, kila mmoja amekuwa msemaji, sio mwenyekiti, sio katibu, sio muenezi hiki kweli liaminike la yupi ndio sahihi?
 
Back
Top Bottom