Zacky20
Member
- Jan 12, 2018
- 24
- 17
*TAMAA YA CHADEMA NA NDUGU SALUM MWALIMU JUMA KINONDONI*
Nimetafakari kwa kina huu uteuzi wa Chadema kumteua Naibu katibu mkuu ndugu Salum Mwalimu Juma kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la kinondoni nimeshawishika na kubaliana na mwenyekiti wa Uvccm kuwa kamati kuu ya Chadema ni kama kamati ya harusi.
Kuna sababu kubwa nne kwa nini mgombea wa Chadema jimbo la kinondoni hawezi kushinda.
*1. Mgombea aliyeteuliwa sio mpiga kura wa kinondoni.*
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Salum mwalimu alijiandikisha kama mpiga kura wa jimbo la kikwajuni Zanzibar na mwaka huohuo alipitishwa na chama chake kugombea ubunge na mpaka leo anapitishwa na chama chake hakuwahi kusema amehamia Dar es salaam rasmi au la!. Huu ni usaliti kwa wakazi wa kikwajuni zanzibar.
Kwa kuwa Salumu alikuwa amejiandikisha Kikwajuni hivyo basi Salumu Mwalimu sio mpiga kura jimbo la kinondoni. Kwa kawaida Unapoteuliwa na chama kugombea nafasi kama ya ubunge jambo la muhimu sana ni kuwa na sifa za kupiga kura katika eneo husika kama mwananchi wa kawaida lakini pia kama mgombea.
Siku zote wananchi hufurahi wanapopata mtu ambaye wanahisi ni mwenzao na anayajua matatizo yao vyema lakini pia ameyaishi. Leo hii hata ukimuuliza Mwalimu kinondoni ina mitaa mingapi hajui je, ni kero gani inawatesa sana wanakinondoni hajui. Sasa Katika mazingira kama haya anashindaje huyu mtu?
Kwanza yeye tu hana uwezo wa kujishindisha kwa kujipigia kura je, unategemea wananchi watamchagua msaka madaraka kama huyu?
Kama ikitokea Mtulia na Salum Mwalimu wakalingana kura basi Salumu hatakuwa na wa kumlaumu isipokuwa kujilaumu mwenyewe kwa kujikosesha ushindi na kukikosesha chama chake usindi.
Kwa mgombea makini angekataa uteuzi wa chama kwa manufaa mapana ya chama. Ccm itatumia sana kete hii kumshtaki kwa wananchi.
Ndio maana nakubaliana na Heri James kuwa kamati kuu ya chadema ni kama kamati ya harusi. Haiwezekani Chama makini kiteue mgombea ambaye ikitokea wapiga kura wote wamesusa yeye mwenyewe hana uwezo wa kujishindisha hata kwa kura moja.
Haya ni makosa makubwa kuwahi kufanywa na kamati kuu ya chadema.Kitendo hiki hakitawaacha salama.
Sasa je, ikitokea ameshindwa 2020 atarudi tena Kikwajuni kuomba ridhaa kwa wananchi au atabaki tena kinondoni? Hizi ndio siasa za chadema huwezi kuwaelewa wanataka nini. Hizi ni siasa za unga wa ngano leo chapati, kesho maandazi na kesho kutwa half cake lakini unga uleule.
*2. Salumu Mwalimu hana ukaribu na wananchi wa kinondoni kama ilivyo kwa mtulia*
Wananchi wengi wa kinondoni wana ukaribu mkubwa na Mtulia kuliko Salum. Sababu kubwa inayojenga ukaribu wao ni ushirikiano wao katika shughuli za maendeleo jimboni.
Mtulia baada ya kuchaguliwa mwaka 2015 amekuwa akionekana kwenye shughuli za maendeleo jimboni huku Salumu akionekana kwenye tv na kwenye mipango ya maandamano.
Kuna uwezekano mkubwa Wananchi wa kinondoni wakapiga kura za kirafiki na kindugu kuliko watu wanavyodhani. Kama hili litatokea itabidi Salumu Mwalimu atunze vzur kitambulisho chake cha kikwajuni zanzibar kwa matumizi ya baadaye.
*3. UTENDAJI WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM*
Tangu rais Magufuli aingie madarakani amekuwa akionyesha kwa vitendo ni jinsi gani alivyo na kiu ya kuifikisha Tanzania katka uchumi wa kati.
Mbali na hilo Mh. Rais ameonyesha uwezo mkubwa katka kupgania rasilimali za watanzania pamoja na kuzisimamia bila kujali ni kwa jinsi gani anahatarisha maisha yake. Kiu kubwa ya rais ni kuona nchi inapiga hatua zaidi.
Hatua ambazo Mh. Rais amekuwa akichukua mathalani kutumbua watendaji wazembe, wabadhirifu wa mali za ummana na wala rushwa zimekuwa zikiwagusa watanzania wa daraja la chini moja kwa moja.
Rais amekuwa shujaa mkubwa sana Kwa watanzania hawa maskini, wanamuona rais kama chaguo sahihi na mtetezi halisi. Kwa mfano hii tumbua tumbua ya watendaji wazembe imemuongezea mh.rais umaarufu mkubwa na kumjengea heshima kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini na kati na wamekuwa wakimpongeza sana. Hawa ndio watanzania ambao rais Magufuli atakwenda kuwaomba wampigie kura mgombea wa ccm.
Hali kadhalika ndugu yangu Paul Makonda amekuwa akifanya kazi kubwa sana katka kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Nadhani kwa sasa huyu ndiye mkuu wa mkoa anayefanya kazi kubwa na nzuri kuliko wote. Hii pia ni kete nzuri kwa ccm katika jimbo la kinondoni.
Hapa Makonda, Hapi, Mwijage, Lusinde, Ummy, mwigulu kule Kangi, Ndasa, Musukuma, Huku Polepole, Makamba na JPM himself unaanzaje kushindwa?
*4. Base ya wapiga kura jimboni*
Ccm ina nafasi kubwa ya kushinda jimbo la kinondoni kwa kutumia kigezo cha idadi ya wanachama. Hakuna ubishi kwamba ccm inawapga kura wengi kinondoni ikifuatiwa na Cuf.
Hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Cuf hakuwa na ubavu wa kushinda isipokuwa alisaidiwa na nguvu ya soda ya chadema jimboni ndipo akaibuka kidedea. Hakuna ubishi bila chadema Cuf angeshika nafasi ya pili na ccm angeibuka mshindi.
This time around Cuf na Chadema wanakwenda kugawana kura zao walizochanga mwaka 2015 na kumuacha Mtulia akirudi mjengoni kiulaini.
Mtulia anakwenda kuweka rekodi ya kushinda ubunge mara mbili katika jimbo moja ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Zakaria[emoji23][emoji23][emoji23]