Salum Mkambala wa Magic FM acha kupotosha

Salum Mkambala wa Magic FM acha kupotosha

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,998
Nimekuwa msikilizaji na mfuatiliaji wa muda mrefu kidogo wa kipindi cha KUPAKA RANGI cha Magic FM, ambapo watangazaji wake akina Orest Kawau, Mary Edward, na baadaye alikuja Salum Mkambala, na mmoja ambaye siku hizi hatumsikii, Kibwana Dachi. Hapo nyuma, mchambuzi maalum alikuwa ni Kibwana Dachi, ambaye pamoja na kuwa ana mapungufu yake, lakini kwa kweli ni mtu mwenye taarifa nyingi, mchambuzi, mfuatiliaji, anajenga hoja, ana logic.

Nakumbuka kwamba hapo nyuma kidogo kituo hiki kimewahi kupewa maonyo, kupigwa faini na hata kufungiwa kwa muda fulani, kutokana hasa na mtindo wa serikali ya awamu hii kutokuwa na uvumilivu wa ukosoaji wa aina yoyote ile. Inaonekana kwamba ni kutokana na misukumo hii ya kiserikali, imepelekea Kibwana Dachi kutosikika tena katika kipindi hiki. Naamini hivyo hasa kutokana na ukweli kwamba "mtaalamu" mpya sasa hivi ni SALUM MKAMBALA.

Sasa hata kama Kibwana Dachi alionekana kuwa "mwepesi kuikosoa serikali", basi angalau wangemwacha aendelee hivyo na huyu Mkambala ambaye anaonekana amepata "mafunzo" hivi karibuni na kuna "watafiti" wanaomsaidia katika "role" yake mpya, awepo ili kuleta balance. badala yake sasa tunaye Mkambala ambaye ni wazi kwamba anasimamia msimamo wa CCM na Serikali yake, na kuwaacha akina Kawau na Mary Edward wakionekana kutojiandaa vema kwa mijadala inayoendelea hapo, licha ya mara moja moja kuwa na hoja za msingi lakini hawana data za kutosha ndiyo kinachowagharimu. Na mara nyingi Mtaalamu Mkambala inapokuja hoja nzito ambayo inaihusu serikali, huwa anaishia kusema tu kwamba "tusubiri kitakachoendelea", na uchambuzi mkali unaoikosoa serikali, Mkambala huwa mwepesi kusema "hayo ni maoni yake". Lakini ikiwa ni jambo linaloisifia serikali, basi huwa mwepesi kulipamba lipambike. Mary Edward na Kawau wamebakia ni watangazaji tu na hata wakitoa maoni, yanakuwa hayajafanyiwa utafiti ili kujenga hoja zao.

Leo asubuhi walikuwa wanaongelea hoja ya Mh. Esther Bulaya dhidi ya Mh. Jenista Mhagama. Esther ni Waziri kivuli na Jenista ni Waziri. Nikamsikia Mkambala akidai kwamba "hajisikii vizuri kumuita hadharani Mh. Esther Bulaya kama Waziri kivuli" akadai kwamba hicho cheo hakihusiki nje ya bunge, kimetungwa kwa kanuni "zao" za bunge na haifai kumuita hivyo nje ya bunge. Nilimsikia Kawau akimkosoa kwamba suala siyo "anavyojisikia" bali ni uhalisia ulivyo. Lakini Kawau aliishia kutoa mifano mirefu ya mzunguko bila kupigilia msumari hoja potofu ya Mkambala.

Kimsingi utaratibu wa "Serikali kivuli" ni wa mabunge ya "Westminster" ambao Bunge letu linaufuata. ni kwa utaratibu huo tunaye "Kiongozi wa Upinzani Bungeni" ambaye anatambuliwa rasmi kabisa na anapewa ofisi na usafiri. Haya yalitakiwa kusemwa na aambiwe Mkambala, lakini hakuambiwa na akaendelea tu kubisha lakini mwishowe wote wakafunga mjadala kienyeji na kutupeleka kwenye matangazo ya biashara. Niliamini kabisa kama angekuwepo Kibwana Dachi hayo yasingetokea.

Niwaombe uongozi wa Magic FM wajaribu kuleta mtu mwingine ambaye ataleta balansi ili tusiegemee mno upande wa serikali. Hii itawapunguzia hata biashara zenu. kumbukeni watanzania zaidi ya milioni 6 walipigia kura upinzani. hivyo misimamo yao siyo ya kupuuza eti kisa mnataka ujiko kwa Serikali ya Magufuli.

Angalau Star TV wameanza kutoa nafasi angalau kidogo kwa upande wa upinzani au kuruhusu hoja kinzani kutangazwa. lakini kuondoa kipindi cha JICHO LETU NDANI YA HABARI, ambapo mtaalamu Dotto Bulendu alikuwa anaongoza jopo la wachambuzi ambao kimsingi walikuwa wanaisaidia Serikali, hilo limekuwa pigo kubwa kwa wapenzi wa uchambuzi wa ukweli. kupaumbele sasa ni kwa habari za kusifia serikali tuuu, ambayo inachosha sana kwa wale wanaofikiri vizuri. penye kizuri pasemwe, penye upungufu pasemwe pia. na siyo kusifia mno kama vile unamuongelea malaika. hawa ni binadamu ambao waliomba kazi kwa watanzania, wamepewa kazi, sasa ni jukumu lao kutekeleza ahadi zao. kuwakosoa siyo dhambi na wala haiwazuii kutekeleza ahadi zao na mipango yao bali ndio kuboresha. Hii ni nchi yetu sote.
 
Magic fm hawana ukurasa wa facebook au twitter?
Hope umeelewa dhamira yangu.
 
hahahaha mi nafikiri alikuwa ktk hali ya kuleta matani na kuchamsha kipindi siamini kama hajawahi sikia neno '' shadow minister'' hata ktk bunge la UK hasa ktk kipindi hichi cha brexit
 
Hii ni summary ya kinachoendelea nchi hii.
tapatalk_1542714542899.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahaha mi nafikiri alikuwa ktk hali ya kuleta matani na kuchamsha kipindi siamini kama hajawahi sikia neno '' shadow minister'' hata ktk bunge la UK hasa ktk kipindi hichi cha brexit
Waandishi wengi hawana taarifa nyingi kiasi hicho . Anaweza akawa hajui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuna tofauti gani katika vipindi vya uchambuzi kati yaMagic FM na Clouds
Kwa kweli hakuna tofauti sana kivile, ila Clouds 360 Hassan Ngoma amezidi mno kujikomba. Shida kubwa ya hivi vituo ni wachambuzi ambao hawafanyi utafiti wala hawana uelewa kabisa wa mada. wanabaki kueleza feelings zao tu na hapo ni rahisi kugeuza kuwa vyombo vya propaganda ambazo hata hivyo hazina nguvu sana maana hazivutii hata kusikiliza
 
hahahaha mi nafikiri alikuwa ktk hali ya kuleta matani na kuchamsha kipindi siamini kama hajawahi sikia neno '' shadow minister'' hata ktk bunge la UK hasa ktk kipindi hichi cha brexit
Kama kuleta utani ndio hivyo basi hajui maana ya utani. Lakini seriously, haukuwa utani. alikomaa na walibishana kidogo. Niliona Kawau alikuwa mkali kidogo kutaka kuweka mambo sawa, lakini baadaye naye akaishia porini na kupoteza mwelekeo wa hoja. Ungekuwa utani basi mwishoni angeiweka vizuri
 
Kipindi cha Morning Magic kimepoteza ladha kabisa baada ya kuondoka Kibwana Dachi na kuachiwa huyu bush lawyer kuwa ndiye mchambuzi mkuu. Mkambala anakera sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nine is balalaika sana humu juu ya huyo mkambala sasa hivi nikiwasha redio nikakuta yupo hua nafanya shughuli nyingine.Hugo jamaa in kituko na ueledi wake bado sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi cha Morning Magic kimepoteza ladha kabisa baada ya kuondoka Kibwana Dachi na kuachiwa huyu bush lawyer kuwa ndiye mchambuzi mkuu. Mkambala anakera sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkambala ni mshamba pia ni Bonge la limbukeni Akili zake ni sawa na za Cyprian musiba hana tofauti na Le mutuz yafaa watu waache kusikiliza kipindi chake akose Udhamini ndipo atazinduka na kuacha ufala wake
 
Ni kweli, ndio maana hata mtu akiwa nguli kiasi gani, akishaingia CCM tu basi anakuwa povu tupu

Uzuri watu wa magic FM wengi wapo JF watampelekea ujumbe haraka apate kujua kuwa wasikilizaji wamechoka na umbumbu na ufala wake na asipokuwa makini wataacha kusikiliza kipindi chao.
 
Back
Top Bottom