JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Salum ambaye ni mdau wa Maendeleo na msomi aliyebobea kwenye fani ya uchumi na mfanyabiashara mbobevu amechukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Handeni mjini lengo likiwa ni kuleta mabadiliko chanya na mwanga mpya wa maendeleo ya Jimbo hilo.
Hatua hiyo ya Salum kuingia rasmi katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM imeibua msisimko mpya Kwa wakazi wa Handeni Mjini hasa ukizingatia historia yake ya kiongozi na ufanisi alionyesha katika nyanja mbali mbali za maendeleo katika Jimbo hilo.