Salome Makamba(Mbunge), ahoji ujenzi uwanja wa ndege Chato, barabara ya Bagamoyo na ununuzi wa ndege

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,724
2,000
P1730908.JPG

Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Salome Makamba amehoji sababu zilizoifanya serikali kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato, ambako ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kuacha kufanya hivyo kwenye maeneo mengine mengi yenye fursa za kiuchumi.

Mhe. Salome ameyasema hayo bungeni wakati akichangia kwenye bajeti ya mwaka huu ambapo amesema sababu kubwa ya kushindwa kutekeleza kwa bajeti iliyopita, ni kwa sababu ya serikali kushindwa kusimamia mambo ya msingi. Bi. Salome ameenda mbele na kutaka kujua ni utaratibu gani umetumika kusimamia gharama za ujenzi wa uwanja huo, sambamba na kutaka kujua kuhusu ununuzi wa ndege uliofanywa na serikali.

Akataka ufafanuzi pia utolewe kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco Jijini Dar es Salaam.

Msikilize hapa anavyotema Cheche.
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,957
2,000
Kama Rais mwenyewe alisema mikataba yote ifike bungeni i hope hakutakuwa na double standard hta hii ya ujenzi wa chato na bombardier zitafika bungeni pia ili sintofaham zote zipate majibu
Kama wanataka kupeleka mikataba yote Bungeni au kama kweli hataki watu fulani wasijadiliwe hadharani basi nafikiri ni bora waunde Reconciliation Commission kama RSA walivyofanya baada ya uhuru ili tuzungumze watu wamalize hasira zao na tuanze upya!!
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,527
2,000
Alichokisema ni sahihi kabisa. Ila wenye Bunge lao wanogopa kabisa kuzungumzia hicho kitu. Hivi wanashindwa kutambua kwamba huo uwanja wa Chato utakuwa ni kituko cha karne?
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,550
2,000
Kama ni kusema tu, hata mimi nishasema sana humu JF. Swali ni je, kajibiwa? Kaungwa mkono na walio wengi? Mbona kimyaaaaa, Tatizo sio kusema, tatizo ujibiwe tu mkuu
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,550
2,000
Alichokisema ni sahihi kabisa. Ila wenye Bunge lao wanogopa kabisa kuzungumzia hicho kitu. Hivi wanashindwa kutambua kwamba huo uwanja wa Chato utakuwa ni kituko cha karne?

Kwa nini mkuu?? Kwani wadhani Chato iko wapi ambapo ndege zitashindwa kufika? Kama zatua Kigali, Entebe hadi Kisumu, Chato ni wapi zisifike?? Wajua kuna madini pale Biharamulo?? Watu watapajua tu
 

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,431
2,000
Mbona hili la uwanja lilishajibiwa kitambo!! Huyu dada aache wivu wa kijinga, hata Chato wanaishi binadamu nao wanahitaji uwanja.

Yeye mbona kapata ubunge viti maalum Shinyanga wakati ni wa Kaskazini? Au kisa chama cha mababy?
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,527
2,000
Kwa nini mkuu?? Kwani wadhani Chato iko wapi ambapo ndege zitashindwa kufika? Kama zatua Kigali, Entebe hadi Kisumu, Chato ni wapi zisifike?? Wajua kuna madini pale Biharamulo?? Watu watapajua tu
Hatukatai kwamba ni sehemu ya Tanzania, lakini je hiyo sehemu ina watumiaji (wasafiri na mizigo) wa kutosha watakaoweza kuufanya huo uwanja usionekane kituko?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom