Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Salma Kikwete ameishauri Serikali kutafuta mbadala wa vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks), baada ya kuonekana vinywaji hivyo vinavyotumiwa na vijana wengi nchini vinaharibu vijana hao ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Soma > Serikali yapunguza kodi kwenye vinjwaji aina ya Energy Drink
Salma amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2025/2026 na Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
"Kuna kitu kinaitwa ‘energy’, ni shida, ni tatizo na wanaokunywa ni watoto wadogo na wanakunywa kwa malengo yapi? kama wanaweza sasa hivi wana umri wa miaka 13 ‘kuboost’ wakifika miaka 28 watakuwa katika hali gani? zinaharibu watoto jamani, watoto wanaangamia tutafute mbadala jamani," amesema Salma Kikwete