Salim Kikeke Vs Shaka Ssali

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,491
2,000
huyu shaka ssali ni level nyingine,labda yakina christina Amanpour (cnn) na Steven sucker (hard talk) kwani huwa anafanya utafiti wa kutosha juu ya mada atakayozungumzia na ndio maana hata wageni waalikwa kwenye kipindi chake huwa wanakutana na maswali magumu ambayo hawakutegemea!!na hata wakati anaanzisha hicho kipindi cha straight talk africa watu walimbeza sana ila walikuja kukubali,na kwa uzoefu wake wa miaka 37 pale VOA,si mchezo.Salim kikeke anajitahidi kiasi chake ila bado hajafikia level ya gwiji hili,hata kwa vicent makoli bado labda ni kutokana na aina ya vipindi,yeye salimu ni taarifa ya habari tu ila hawa jamaa ni waendeshaji wa vipindi vya mahojiano ndio maana wanaonekana wako njema.Sio wakina Gabriel zakaria anaendesha kipindi anarukaruka kwenye kiti kama amekalia msumali!!na maswali yenyewe ni yale mtu anauliza huku anajua jibu!!yeye amebobea kwenye masuali ya visimbusi tu,hapo utampenda.siku moja alikuwa anahojiwa live na cctv (china)juu ya uhamaji wa nyumbu serengeti utamuonea huruma!!kibongo bongo shaka ssali wetu ni jenerali ulimwengu.
 

Mbushuu

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
1,952
2,000
Ha ha haa iyo ya Gabriel zakaria umenichekesha,Generali ulimwengu nae siku hizi naona kiwango kimeshuka sana
 

Scale

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,729
2,000
Salim Kikeke anatangaza BBC (Dira ya dunia usiku) ni kipindi kinachojizolea mashabiki wengi sana wakati Shaka Ssali anatangaza VOA ( straight talk africa) kipindi ni kikongwe kidogo.Sasa naomba tupime ubora wao katika uwasilishaji na uchambuzi katika vipindi vyao,tusi base kwenye lugha mana kipindi kimoja kinaendeshwa kwa lugha ya kigeni wakati kipindi kingine ni cha kiswahili.Naomba kuwasilisha

Usiseme Shaka Ssali sema Dr. Shaka Ssali!
 

Capital

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,349
2,000
Dr Shaka Ssali ni next level, yaani Kikeke hamfikii hata 0.125, yaani moja ya nane. Inaonekana umeanza kuangalia tv mwaka huu. pole kajipange upya
 

Lweye

Senior Member
Apr 15, 2010
139
225
Dr. shaka Ssali ana kiwango cha juu sana, kumlinganisha yeye na Salim kikeke ni sawa na kumlinganisha Messi na Ngassa katika soka! Naamini hata Salim Kikeke akiulizwa anapenda kuwa kama nani katika fani ya utangazaji atasema anapenda awe kama Shaka Ssali!
 

Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,599
2,000
Ni matusi kujaribu kumlinganisha Shaka Ssali na Salim Kikeke now...tusubiri Kikeke afikie level ya Shaka kwanza!
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,770
2,000
ni sawa na kumlinganisha tsyon na cheka.,
too unequal.,
au p.funk na marco,.,
au nyerere na j.k.

Huyo kikeke level zake akina hilary,marin hassan etc.
 

Chen Hu Xiansheng

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
3,046
2,000
Dr.Shaka Ssali yupo juu zaidi, ni jana tu nimetoka kumtazama.
Sema Shaka anatazamwa zaidi na watu ambao hawakukimbia umande na vipindi vyake ni pasua kichwa (kama hapa JF, ningesema JAMII INTELIGENCE) wakati Kikeke anatazamwa na kila mtu (sawa na MMU kwa hapa JF)
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,185
2,000
Kikeke anaelekea huko walikofika hao magwiji akina Shaka Ssali,STEVEN Sucker,Riz Khani,Amanpour,Larry King na wengineo...
 

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,937
2,000
Shaka Ssali anaitwa Veteran Journalist.....Hiyo Straight Talk Africa ipo kwa 10 years!! ameshaongea na viongozi wengi wenye nyadhifa za juu Afrika, Salim Kikeke ana promising future ila kwa sasa hauwezi kumlinganisha na Shaka Ssali.......Remember get better not bitter.
 

dav22

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
1,893
1,225
Dr Shaka Sali ni levo nyingine aisee akiwahoji hawa wanasiasa wetu uchwara hapa bongo wanakimbia kipindi kwanza hawana uwezo wa kuitwa katika kipindi kama kile maana wamezoea kupiga kelele tu bila point yoyote kwahiyo ndugu Dr Shaka Sali huwezi mkompea na chocho kwa Salim Kikeke nadhani salim ndo bado anaibukia na bado ana safari ndefu kumfikia Dr Shaka Sali
 

Scale

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,729
2,000
Emanuel Buhohela wa ITV anakuja vizuri pia! Tatizo ni pale wanapojiingiza kwenye Siasa wanakuwa one sided mind!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom