Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Mdhamini nayezungumzia sio Kama gsm. Mwigulu ana cheo yanga wakati huo huo ni mmiliki wa timu nyingine.
Yeye ndio anasimamia Mali za yanga unategemea kutakuwa na haki yanga ikicheza na Singida black star?
Ana cheo kipi
Sababu wenye vyeo ni wakin engineer, alikamwe, arafati na wengineo mwigulu hayupo

Mwigulu hasimamii mali za Yanga ni uongo yule ni mwanachama tu ambaye hakatazwi kumiliki timu nyingine ni kama wewe kuwa mwanachama wa simba hukatazwi kumiliki timu nyingine

Azam ile timu ni ya bakheresa ila msimamizi wa mambo ya timu ni mtoto wake
 
View attachment 2966280

Moto unawaka SSC! Ni vita kubwa!
Klabu ya Simba ipo katika kipindi kigumu cha vita inayozidi kukomaa kila uchwao baina ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Mhene ‘Try Again’ dhidi ya ‘Rais wa heshima’ wa Simba Mohamed ‘Mo’ Dewj.

Wawili hao walianza kukosa maelewano baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi yake nchini ambapo taarifa za uhakika ni kwamba anaishi Dubai hadi hivi sasa.

Baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi uwekezaji wake Simba ulisuasua, ikitaarifiwa kumuachia mzigo mkubwa wa uendeahaji timu Try Again ambao ulimuelemea!

Try Again alijitahidi kadiri ya uwezo wake baada ya ‘tajiri’ kujitenga ‘kiaiana’, akihaha huku na huko kutafuta namna ya kuinusuru Klabu ya Simba ambayo kwa msimu wa tatu mfululizo imekuwa na matokeo ya kusuasua. Jitihada zake hizo zikizaa matunda kwa kiasi kisichoendana na kipindi ambacho muwekezaji alikuwa ameshikilia usukani.

Try Again adhamiria mapinduzi, amlenga Said Salim Bakhressa!
Baada ya Try again ‘kususiwa’ timu na muwekezaji Mo Dewj, Try Again aliona uwezekano wa kupindua meza, na kama ilivyo ada ya wafanyabiashara wakubwa kuwa na jicho angavu la udhia, S.S Bakhressa hakusita kupenyeza rupia!

Vita kubwa iliyopo hivi sasa ni Try Again aliyeko kwenye mikakati thabiti ya kumpindua Mo Dewj kama muwekezaji kisha nafasi hiyo apewe muwekezaji asiye na ‘mbambamba’ S.S. Bakhressa, huku Mo Dewj nae akiwa katika mipango ya kujidhatiti kushikilia nafasi yake hiyo adhimu ambayo huitumia mara nyingi kama kielelezo cha mali zake (SSC)

Serikali yakoleza vita!
Hivi karibuni, Serikali imetoa agizo la kuanzishwa upya kwa mchakato wa undeshwaji wa kisasa kwa klabu ya Simba. Kama mtakumbuka vyema mchakato huo ulioanza miaka kadhaa nyuma, haukuwahi kukamilika.

Serikali imetoa agizo hilo baada ya kujidhihirisha kuwa mchakato wa awali ulikuwa na makosa mengi, hivyo ulikuwa batili ukikosa uhalali.

Agizo hilo limekuwa chachu kwa Try Again na timu yake, kwani endapo ukifanikiwa kuanza kuna uwezekano mkubwa wa S.S. Bakhressa na wawekezaji wengine kujitokeza na kushika hatamu katika hisa, huku ikielezwa kwamba Mo Dewj atarudishiwa fedha zake alizolipia katika mchakato huo uliohuishwa ambako alijitwalia hisa 49% za umiliki wa klabu ya Simba.

Mo Dewj atupa shilingi mechi ya Yanga!
Hii ni tahadhari kwa Klabu ya Yanga, Hersi na wenzio kama hamjaipata nawapa hii…

Mo Dewj amejipanga kuitumia mechi ya tarehe 20/04/2024 dhidi ya Yanga kama turufu yake ndani ya Simba.

Mo Dewj ambaye inaarifiwa ametenga fungu ‘nono’ kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo, amejipanga sawia na mkakati wake huo ambao tayari ameshaanza utekelezaji.

Mkakati huu wa Mo ni kwamba endapo Simba ikishinda mechi hiyo, atafanikiwa kurudisha imani na mapenzi kwa mashabiki, hivyo kutumia hilo kama zengwe la kuwang’oa Try Again na Mangungu pale Simba.

Kila mmoja ana mpango kazi!
Try Again ambaye hapo awali alitumia ‘janja janja’ kuwang’oa aliyekuwa CEO wa Klabu bibie Barbara na Rweyemamu ambaye alikuwa meneja wa timu kwa ‘kuwachonganisha’ na muewekezaji Mo Dewj, anahaha kulinda maslahi yake kwani endapo Mo Dewj akishinda vita hii (Kwa Simba kushinda dhidi ya Yanga) amepanga kuwarejesha Barbara, Rweyemamu ambaye hivi sasa yupo Kikosi B na aliyekuwa Mkurugenzi wa bodi ya wawekezaji ambaye alijiengua Nkwabi.

Try Again ambaye wameungana na Mangungu kumuhujumu Mo Dewj, nao hawako nyuma. Wanatumia turufu yao ya ‘ujanja wa mjini’ kuhakikisha Mo Dewj anang’oka Simba kwa namna yoyote!

Inaarifiwa hata agizo la kuanza upya kwa mchakato wa uendeshaji wa kisasa wa timu umechagizwa na ‘connection’ za Try Again pamoja na S.S.B na mpaka hivi sasa mpango wao ‘umetiki’.

Je, nani ataibuka mshindi katika vita hii? Ni ‘watoto wa mjini’ Salim Abdallah, Try again au tajiri Mo Dewj?

Ni mimi na chanzo changu nyeti,

Nifah.
Kinadharia, try tena anamuwakilisha Mo kwenye Board na Magungu anawakilisha wanachama so unataka utuambue jaribu tena anataka chukua hisa za MOOO ili amuuzie SSB.?? Juris ignoncia non execusanri
 
Kinadharia, try tena anamuwakilisha Mo kwenye Board na Magungu anawakilisha wanachama so unataka utuambue jaribu tena anataka chukua hisa za MOOO ili amuuzie SSB.?? Juris ignoncia non execusanri
Ni siasa na uongo
Try again ameweka na mo na lisema yeye yuko bize na ana mambo mengi kwa hiyo akamchagua try again
 
Ana cheo kipi
Sababu wenye vyeo ni wakin engineer, alikamwe, arafi na wengineo mwigulu hayupo

Mwigulu hasimamii mali za Yanga ni uongo yule ni mwanachama tu ambaye hakatazwi kumiliki timu nyingine
Unafahamu wajumbe wa baraza la wadhamini yanga na kazi zako

Wako watano Mwigulu akiwemo wengineno Tarimba, Mkuchika, Mama Karume wa mwisho simkumbuki somebody Mwambie.
Unajua kazi zao, ni kusimamia Mali za yanga.
 
Ana cheo kipi
Sababu wenye vyeo ni wakin engineer, alikamwe, arafati na wengineo mwigulu hayupo

Mwigulu hasimamii mali za Yanga ni uongo yule ni mwanachama tu ambaye hakatazwi kumiliki timu nyingine ni kama wewe kuwa mwanachama wa simba hukatazwi kumiliki timu nyingine

Azam ile timu ni ya bakheresa ila msimamizi wa mambo ya timu ni mtoto wake
Ali Kamwe ana cheo gani?
 
Usiamini maneno ya mfanyabiashara Mkuu, akiona fursa katu hawezi kuacha kuitumia.

Simba ni taasisi kubwa, hakuna tajiri anayeweza kuchezea fursa ya kuwekeza pale.
326BB0A7-61D1-4685-8C0A-A11D7D8A97E3.jpeg




2F6E25AE-89B9-4AE4-B795-F82F753D8A4F.jpeg
 
Back
Top Bottom