Salary slip ya Julai, 2021: Hakuna Tzs 2,500, deni la HESLB halijapungua

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Ndo hivyo, inaonekana sasa!

Niliaminishwa nitakuta deni la HESLB limepungua kutokana na kutolewa ile nyongeza kama alivyoamrisha Mh. Rais; HAKUNA BADILIKO!

Nilisikia kuna kanyongeza ka 2500 ka kupatia mo energy za jero tano kwa ajili ya kuinjoi na familia kila mwisho wa mwezi; HAKUNA KITU.

Dah!
 
ingia kwenye account yako ya HESLB angalia statement, mimi langu limepungua sana tu, ila makato kama tulivyoambiwa yatabaki vile vile.
OK, kwa maana kile kinachoonekana kule ndicho kinachopaswa kulipwa? Km huku kwny slip halitosis haitokuwa raising kupitiliza kweli?!!
 
OK, kwa maana kile kinachoonekana kule ndicho kinachopaswa kulipwa? Km huku kwny slip halitosis haitokuwa raising kupitiliza kweli?!!
Nenda HESLB kachukue statement ukikuta limepungua omba liquidated letter peleka kwa mwajili atalekebisha deni
 
Wakuu naomba kuelekezwa salary slip mbona inagoma kupakuliwa kuna shida gani wajameni?
 
Nenda HESLB kachukue statement ukikuta limepungua omba liquidated letter peleka kwa mwajili atalekebisha deni
Kwa wale wa vijijini wanaenda vipi ofisi za bodi ghafla?

Si walisema watunganisha mfumo wa bodi na hazina ili deni linakuwa linafanana?

Kama waliweza kuwatafuta wadaiwa sugu na kupeleka makato bodi iweje washindwe kuhuisha taarifa hazina?

Wenyewe wakiri tu bodi kuna watumishi hawana uwezo au ni wababaishaji!
 
Nahisi hii imetokea kwa wote ambao wanacheki namba. Yaani salary slip ya mwezi July inaonesha hela imeenda HESLB lakini kwenye akaunti ya HESLB-OLAMS deni haliko updated.

Binafsi naona tuwasubiri bodi mpaka tarehe tano Agost na kuendelea, labda bado hawaja-update kwenye mfumo wao, au bado hazina hawajapeleka hela kwenye akaunti zetu za bodi.

KUWAPONDA BODI;

Kwa nini bodi wanakuwa wababaishaji kuhusu madeni ya wadaiwa. Mwanzoni mwa mwaka huu, walisema wataunganisha mfumo wa bodi na hazina ambapo kila mdaiwa atakuwa anaona deni lake kila anapolipa.

Sasa leo mwezi wa saba bado hawajaunganisha huo mfumo maana yake nini?

Je, hawaoni kwamba wasipounganisha mfumo wa bodi, na hazina mtu anaweza kuwa amemaliza deni lakini anaendelea kukatwa na hazina? Ikumbukwe, baada kuondoa VRF, wadaiwa wengi deni halisi limepungua kwenye akaunti ya OLAMS-HESLB, lakini kwenye salary slip deni ni kubwa! Deni halisi lipo bodi.

Kama bodi walikuwa chapu kupeleka makato kwa waajiri, je, ni kitu gani kinawafanya washindwe kupeleka deni halisi hazina baada ya kuondoa VRF? Yaani wapo shapu kukata ila wamekuwa wazito kuhuisha taarifa hazina!

Je, wataalamu wa TEHAMA hapo bodi hawana uwezo wa kushughulikia hili suala la madeni bila kufika ofisini? Kwa mfano, tangu juni niliomba bank statement ila mpaka leo sijapata! Halafu website yao nzito kweli. Sections ambapo zipo kwenye website ni kama mapambo tu, uki-click hazifunguki. Ukiomba statement unaambiwa subiri. Sasa si wawatafute hata watengeneza blogu wawasaidie kuweka sawa hiyo tovuti!
 
🤣🤣🤣🤣hv kweli me unaniambia unaniongeza mshahara 2500, si utani huu.
Wafanyakazi maserikalini mnapitia magumu sana🙏🙏
 
ingia kwenye account yako ya HESLB angalia statement, mimi langu limepungua sana tu, ila makato kama tulivyoambiwa yatabaki vile vile.
Kwanini makato yabaki yaleyale wakati deni limepungua kwa nusu nzima? Hapo Mtu unashindwa hata kuchukua mkopo kama ilikuwa ni hitaji.

Ila sio mbaya kwasababu deni litaisha mapema
 
Back
Top Bottom