EmmaGMangwela
Senior Member
- May 11, 2015
- 139
- 54
Baada ya mikutano yangu mitatu ya Kigoma Kaskazini, Kigoma Kusini na Kigoma Mjini, napenda kutumia nafasi hii kuwatakia kila la heri vijana wetu wa Timu ya Taifa Stars kwenye mechi yao ya kwanza ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 watakapokuwa wakiuamana vikali na Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles).
Napenda kuwatia moyo vijana wetu hawa kuwa watambue kwa dhati kabisa kuwa wanabeba matumaini yetu sote kama taifa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inapunguza ile dhana ya kwamba 'kila mmoja anaweza kujifunza kunyoa kupitia kichwa chetu' linapokuja suala la michezo, hususan mpira wa miguu kwa maudhui ya hapa. Ushindi watakaoupata dhidi ya Wanaigeria hao, ni sifa kwa Watanzania wote.
Salaam zangu hizi za kuitakia kila la heri Taifa Stars pia ziende kwa watu wote wanaohusika katika kuwanoa vijana hao kuhakikisha Taifa ndilo linashinda, nikianzia na makocha, madaktari, halikadhalika uongozi wa Shirikisho la Michezo nchini (TFF).
Aidha ningependa kumalizia salaam hizo kwa kuzungumzia suala moja la kisera kuhusu michezo. Watanzania wakinichagua kuwa rais wao hapo Oktoba 25, mwaka huu na Mwenyezi Mungu akaridhia, tunajiandaa kuwa serikali itakayokuwa rafiki wa micehzo na sanaa.
Mojawapo ya masuala ambayo nitayapatia uzito katika eneo hili ni kujenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa.