Salamu toka viwanja vya sabasaba

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
SALAMU TOKA SABASABA
Siku hii imefika tena ambapo kampuni mbali mbali , mashirika na watu
mbali mbali hukusanyika sehemu moja kwa ajili ya kuonyesha biashara
zao , kazi zao na bidhaa zingine mbali mbali kwa watu wa ndani na nje
ya nchi ambao huja kutembelea maonyesho hayo

Haya ndio maonyesho makubwa kabisa ya kibiashara katika Tanzania
ambayo hukutanisha watu wengi zaidi , kampuni , mashirika na watoa
huduma wengi zaidi kuliko maonyesho yote haya ni maonyesho ya
sabasaba


Mimi nimekuwa nikienda katika maonyesho haya huu ukiwa ni mwaka ya 7
karibu zamani kidogo nilikuwa naenda kwa nia ya kuangalia tu na
kufurahi au kununua vitu wakati huo bado nasoma katika shule za
chini .


Muda ulivyozidi kwenda nikajikuta naongia katika Fani ya
ICT ,nikabadilisha mwenendo , sasa nikienda ni kuangalia vitu mbali
mbali vinavyohusu mawasiliano na ICT kwa ujumla mwaka jana ilikuwa ni
hivyo hata mwaka huu imekuwa ni hivyo hivyo .


Nilitembelea maeneo mengi ya sabasaba kwa ujumla nimefadhaika kidogo
kuona kwamba katika maonyesho haya bado kuna bidhaa nyingi sana toka
nchi za watu ,kampuni nyingi zilizo katika maonyesho hayo pia ni za
kigeni ukiacha mashirika machache , kwanini kwa miaka yote hii
serikali pamoja na wadau wengine hawajafikiria kualika zaidi watu
kutoka ndani ya kampuni zao kwa ajili ya kutangaza katika maonyesho
haya makubwa zaidi nchini mwetu
Nilishangaa nilipoona kampuni moja ya Kutoka nchi jirani
inayotengeneza vitu vya kula kama biskuti na keki ,kuwa haina mpinzani
katika maonyesho hayo kampuni hiyo labda ilizidiwa na kampuni ya Azam
ambayo inatengeneza Juice na vyakula vya aina nyingine lakini kampuni
kama Tabisco inayotengeneza biskuti kama hii haikufua dafu wala
kuonekana ikingaa katika maonyesho haya .


Nilipokuja katika masuala ya ICT na mawasiliano kwa Ujumla kuna
Sehemu ya Kampuni kama Agumba computers , nilifika pale kuongea na
Yule dada baada ya kuona katika moja ya vitu wanavyofundisha ni E-
Security na Forensics Dada aliyekuwa hapo kuelezea watu wanaotembelea
Sehemu yao hakuwa anajua chochote kuhusu hiyo ESECURITY NA FORENSICS ,
kampuni kama Power Computers imenifurahisha haswa katika masuala ya
CCTV mtu waliyemweka pale ni mtu anayeelewa vitu anavyofanya .


Nilipita pia Katika Chumba cha COSOTA inayojihusisha na Hati Miliki ,
hawa pia wameshindwa kuweka watu hata wanaojua sheria kidogo kuelezea
wengine waliopenda kujua zaidi , badala yake wanakwambia ukitaka
habari zaidi kupiga simu au kuandika Barua pepe .


Pia nilitembelea kampuni za mawasiliano ya simu TTCL , Tigo , Zain na
Voda kulikuwa na Tatizo kidogo kwenye Upande wa Zantel hata hivyo kwa
huduma nyingi ambazo zinatolewa zantel pia zinatolewa katika kampuni
hizi nyingine na kama nilivyosema watu waliowekwa hawawezi kujieleza
pengine sio wafanyakazi wa kampuni hiyo ni part time ya Sabasaba tu .


Kuna hili suala la Simu feki au zisizokuwa na Viwango kutoka nchi za
Ngambo nimeona suala hili katika Mabanda ya TTCL , TIGO na VODA sasa
inawezekana wanashare vyumba vyao na maduka ya kuuza simu ndio maana
unakuta simu ziko ndani kwenye mabanda yao kama ndio hivyo ni vizuri
waandike matangazo kabisa kwamba maduka hayo na simu zao hazihusiani
kabisa na ZAIN au TIGO na Voda ni maduka binafsi .


Kwenye banda la Kampuni mpya ya Mawasiliano SASATEL nayo nilipita ,
hata hivyo huduma zake nyingi pia ni sawa na kampuni zingine , naona
hajaweza kuleta ushindani kwa kweli na kuwa tofauti na kampuni zingine
kwa kutupa huduma mpya na bora kabisa --- labda huko mbeleni wakati
inasoma soko na kupata wateja wengi zaidi , mfano internet niliona yao
katika computer zao mbili zilizowekwa kama mfano spidi yake ni ndogo
kuliko wanavyotangaza katika Matangazo yao


Ukiacha yote haya na mengine kilichonivutia kingine ni Banda La
Taasisi ya Elimu Tanzania TEA , nilivutiwa sana na jinsi walivyoweza
kuboresha vifaa na elimu kwa watu wenye ulemavu haswa wasioona ,
nilishihudia mwenyewe mlemavu mmoja wa macho akitumia computer yake
bila tatizo lolote , nikajaribu kumuuliza maswali machache ni mtu
anayejua mengi
Huyu mtu ambaye ni mlemavu akaniambia Taasisi ya Elimu pamoja na
Shirika La Sight Savers wako katika mipango kabambe ya kuhakikisha
wanapata walimu wa kutosha na wenye ujuzi ambayo wataweza kwenda
kufundisha watu wenye ulemavu katika utumiaji wa vifaa vya ICT toka
Shule ya msingi sekondari vyuoni mpaka Makazini


Kampuni , Watu binafsi na mashirika mbali mbali yanayowekeza katika
maonyesho ya SABASABA wajue maonyesho yale ni kiioo cha Nchi yetu
katika masuala ya Biashara , sasa wanapoamua kuweka watu wasiojua kitu
katika maduka yao , vibanda na mabanda yao ni hatari sana kwa kampuni
zao , nchi yetu na pia kwa wale waliowekwa pale kuelezea wageni mbali
mbali wanaotembelea maduka hayo .
Ni hayo tu toka saba saba
 
Actually it is rather informative, pray tell it is not copy-pasted.
 
Back
Top Bottom