activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
Nianze waraka huu mfupi kwa kupeleka ujumbe(salamu) wangu kwa vyama halisi vya upinzani CHADEMA,NCCR,CUF na ACT Wazalendo kuhusu yanayojiri Bungeni.Niseme tu kuwa nimekuwa nikifarijika na hoja zenu nzito na za msingi zinazogusa na kuifariji jamii ya watanzania ambao wengi ni masikini.
Niweke wazi kuwa naunga mkono harakati mnazozifanya katika kupigania demokrasia, haki na usawa wa sheria katika taifa hili mkiwa ndani na hata nje ya bunge.Tokea wabunge kadhaa wametolewa na naibu spika, na kupewa adhabu ambazo binafsi zimeniacha mdomo wazi, ninapata shida kuzisaka taarifa zinazoendelea pale bungeni kwani sioni tena jambo jipya litakalozaliwa lenye faida kwa wanyonge.
Lakini ninataka kujua yafuatayo toka kwenu.
1. Mtaendelea kugomea vikao vya Naibu spika hadi lini? Je, kuna jambo lolote mnalolifanya sasa ambalo litakwenda kumuondoa katika kiti hicho ili kuruhusu mrudi na pia hoja zenu za msingi kupenya bungeni?
2. Bunge halionyeshwi, kwa sababu za maajabu, bunge halipo huru, wapinzani mnabanwa kinyume na kanuni na taratibu, mnapewa adhabu za maajabu. Mimi nataka kujua viongozi wa ukawa na Zitto kabwe, mnampango gani juu ya haya? Wahakama zipo, wananchi wapo, hali ya namna hii itaendelea hadi lini? Maisha yanazidi kuwa magumu, bajeti za ajabu zinapitishwa huko bungeni, bunge limekosa nidhamu, wabunge tena vijana wanaongea vitu vya kustaajabisha kabisa. Nauliza hali hii itaendelea hadi lini?
Bunge litaonyeshwa live lini?
Adhabu hizo mlizopewa za kutoshiriki vikao zinatenguliwa lini? Dada anaondoka lini huyu?
Naamini mko na wasomi na watu wa mikakati makini na hamtotuangusha wanyonge. Mmechukua hatua but it's not enough. Njooni na mikakati mipya turudishieni heshima wananchi.
By fikra Huru
activisti@yahoo.com