Salamu kwa ndugu yangu Dar Es Salaam


Makiri Unguluma

Makiri Unguluma

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2011
Messages
993
Likes
113
Points
60
Makiri Unguluma

Makiri Unguluma

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2011
993 113 60
Nimependa nikusalime ndugu yangu maana tangu siku zile za zamani mimi nilipopewa hadhi ya kuwa makao makuu umekuwa ukinibania. Ndugu yangu wewe hukukubali kunipatia haki zaidi ya kuruhusu tu waheshimiwa waje kufanya mikutano kwangu.

Kwa roho nyeupe kabisa nafurahi sana kwa sasa undugu wetu utapendeza zaidi maana nimesikia kuwa huwezi kubeba watu tena na hivyo uko tayari kuruhusu hadhi yangu nipewe.

Mimi nitakupenda tu ndugu yangu hata kama hilo halitatokea maana wewe utabaki kuwa mkubwa kibiashara kwa muda mpaka baadaye wakati wadogo zetu wengine Mtwara na Tanga watakapokua wakubwa.

Waambie Tanga na Mtwara wawe watulivu kama mimi nilivyokuwa mtulivu kwa muda mrefu

Ni mimi nduguyo wa kufa na kuzikana
Dodoma
 

Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044