Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 590
- 706
Soma utaelewa... 🙏🙏Huo ujumbe katumiwa Nan sasa au shumileta wa kizimkazi
Watu wote wenye tabia niliyotaja kwenye nukuu hiyo inawafaa. 😂😂huo ujumbe wako unawafaa G-55
Duh! 😂😂Uaneni tu
Kumbe na wewe ni CHAWA WA MAMA?
Kumbe na wewe ni CHAWA WA MAMA?
Kula block malaya wa kisiasa wewe
This is simple bloody censorship.
Karibu nikufundishe jambo, shuka nayo.This is simple bloody censorship.
Hebu kaa chini nikupe somo.
Katika uongozi kuna kitu kinaitwa collective responsibility. Hii ni kanuni kwamba uongozi unafanyika kwa pamoja, si kwa mtu mmoja mmoja. Maana yake kama kuna pongezi au lawama, zitaenda kwa uongozi wote, si mtu mmoja.
Kwa kanuni hii, mambo hayapitishwi na mtu mmoja, yanapitishwa kwa vikao kujenga consensus, makubaliano.
Sasa inakuwa vipi kama vikao vinaleta ajenda ambazo kiongozi huzitaki, au mambo yanafanyika bila kuletwa kwenye vikao?
Hapo kuna mambo machache ya kufanyika kama mtu hakubaliani na yanayofanyika.
1. Kujenga ushawishi ndani ya uongozi ili mambo hayo yabadilishwe. Kwa njia hii kiongozi anaweza kujenga ushawishi mpaka yale mabaya yakabadilika anavyotaka yeye.
2. La sivyo, kama namba 1 haiwezekani, na mtu bado anataka kuwa kiongozi, na jambo asilolipenda labda kaliona si kubwa sana, anaweza kukubali kubaki katika uongozi bila kulibadilisha hilo. Kufanya hivi kutakuwa kunamfanya yeye awe sehemu ya maamuzi ya jambo hilo hata kama halipendi, na lawama zozote zikitokea atazibeba. Akikubali kubaki katika uongozi, kanuni za collective responsibility zinamkataza kuusema vibaya uongozi kwa maamuzi asiyoyapenda. Kwa sababu na yeye ni sehemu ya uongozi, anaweza kushauri yabadilike kutoka ndani ya uongozi kama nilivyotaja awali kwenye item 1.
3. Mwisho kabisa, kiongozi akiona hili jambo kashindwa kulibadilisha kutoka ndani, na kwa kweli hawezi kusema kuwa hili ni jambo dogo aendelee kuwa kwenye uongozi tu bila ya kulibadilisha, kiongozi ana haki ya kujiuzulu uongozi na kujitenga na mambo fulani, kisha kulikosoa akiwa nje ya uongozi bila kufungwa na kanuni za collective responsibility.
Hizi ni kanuni za uongozi zinazojulikana wazi kabisa.
Sasa, Humpjrey Polepole si mtume, ana maswali mengi sana ya kujibu kuhusu uhusika wake enzi za Magufuli na sababu zake za kweli za kusema aliyoyasema sasa. Hayo sipingi.
Lakini kuna mambo mawili napinga.
Umesema akae kimya. This is simple censorship.
Polepole ana haki ya kikatiba na ya kibinadamu kusema anayotaka kusema. Hafungwi hata na collective responsobility kwa sababu kachagua option 3 hapo juu na kajiuzulu tayari.
Unaziita hizi ni kelele za chuki. Unajiridhishaje kuwa hizi ni kelele za chuki na si mtazamo wa kifalsafa ulio tofauti? Mbona Watanzania wengi sana hawamkubali Samia na uongozi wa sasa kifalsafa tu bila chuki?
Unasema Polepole akae kimya kutunza madhaifu, madhaifu gani? Kwa nini unataka atunze madhaifu na tusiyajue? Yaweke hapa tuyajadili.
Two seemingly opposing things can both be right at the same time. Inawezekana Polepole alikuwa chawa wa Magufuli na kafanya mambo mabaya na akamsema kihalali na kwa ukweli Samia. There is no contradiction there.
Two wrongs do not make a right. Kama Polepole alikosea na kuunga mkono udhalimu huko nyuma, hilo halimaanishi aendelee kuunga mkono udhalimu tu.
Moreover, tusiishie kumuangalia Polepole mtu, tuangalie points alizozitoa. Zina mantiki?
Siasa za Afrika zina tatizo la kuangalia mtu kuliko kuangakia mantiki ya mtu.
Jibu hoja za Poplepole, usimfanyie censorship na ad hominem fallacy attacks.
Hujathibitisha kuwa Polepole kajiuzulu kwa hila ya kisiasa na wala Polepole hajasema kuwa yeye ni mtakatifu, na hahitaji kuwa mtakatifu ili kutumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu kusema.Karibu nikufundishe jambo, shuka nayo.
"Kiongozi anayejiuzulu kwa hila halafu anaanza kutoa kauli kama Nabii wa ukweli, anapaswa kufundishwa kuwa heshima ya uongozi haibebwi kwa mdomo unaolalamika sana, bali kwa uthubutu wa kupambana kutoka ndani mpaka mwisho." – Alloyce, P.R.
Baada ya nukuu hiyo nianze kukujibu kama ifuatavyo:
1. Hoja ya “Collective Responsibility” na Kujiuzulu
Umesema Polepole alitekeleza hatua ya kujiuzulu na sasa yuko huru kuzungumza. Lakini umesahau kwamba kujiuzulu kwa hila na kisiasa hakumfanyi kuwa mtakatifu wa hoja. Kama mtu alikaa kwenye mfumo, akanufaika, akashindwa kusimama ndani ya vikao na kutoa msimamo wake hadharani wakati huo, sasa anaposema aliyoyasema baada ya kuchoka kunufaika, hiyo si falsafa bali ni ujanja wa kisiasa unaovaa joho la busara.
2. Hoja ya “Hii si chuki, bali falsafa tofauti”
Falsafa ni hoja inayojengwa juu ya misingi ya mantiki, tafakuri, na maadili. Lakini Polepole hakutoa hoja za kimaadili au sera bali, alikejeli, na alitumia lugha ya kubeza kama “Serikali haina mwenyewe” na “wamejaa wahuni.”
Hiyo si falsafa, ni kero ya kisiasa. Kama ni falsafa, tupatie kanuni, si matusi.
3. Hoja ya “Tusimjadili Polepole, tudadisi hoja zake”
Hii ni changa la macho. Katika maadili ya siasa za uwajibikaji, **hoja huungwa mkono na tabia ya msemaji. Mtu aliyekuwa sehemu ya ukimya wa mabaya, akafumba macho, sasa hawezi kuwa kipimo cha ukweli hadi ajitathmini kwanza na kutubu hadharani.
Kama hatuwezi kumjadili Polepole, tusijadili hata aliyoyasema, maana ni vigumu kutenganisha sumu kutoka kwenye kikombe kilichojaa makosa yake ya awali.
4. “This is simple bloody censorship”
Hapana. Censorship ni pale ambapo mtu anazuiwa kwa nguvu za kiserikali au za kisheria kuongea. Lakini kukosolewa kwa nguvu na kwa hoja ni sehemu ya uhuru wa maoni pia.
Kama yeye ana haki ya kusema “Serikali imejaa wahuni”, sisi tuna haki kusema “Alikuwa wa kwanza kuwaleta.”
Nimalize na nukuu hii,
"Kama ulikuwa dereva wa basi la hovyo, ukalivuruga njiani, ukashuka kwa hasira, kisha ukarudi kwa abiria na kusema dereva mpya hajui kuendesha, hapo unakuwa huna hoja, una kisasi cha kutoridhika kuachwa kushika usukani." — Alloyce, P.R.
"Kuna watu wanapenda uhuru wa kusema kuliko wajibu wa kuelewa, na wanadhani kubwabwaja ni hekima, kumbe ni kelele za mtu aliyekataa kusoma dakika tano kabla ya kujibu." — Alloyce, P.R.Hujathibitisha kuwa Polepole kajiuzulu kwa hila ya kisiasa na wala Polepole hajasema kuwa yeye ni mtakatifu, na hahitaji kuwa mtakatifu ili kutumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu kusema.
Uhuru wa kujieleza ni haki ya kikatiba na kibinadamu.
Polepole anaitumia haki hiyo.
Huelewi wapi?
Haya, Polepole hajakaa kimya unavyotaka wewe, utamfanya nini?
Utamshitaki mahakamani?
Utamuua?
Utamfanya nini?
Polepole kashasema aliyosema kwa kutumia haki yake ya kibinadamu na kikatiba."Kuna watu wanapenda uhuru wa kusema kuliko wajibu wa kuelewa, na wanadhani kubwabwaja ni hekima, kumbe ni kelele za mtu aliyekataa kusoma dakika tano kabla ya kujibu." — Alloyce, P.R.
Katika hoja ulizoibua nakujibu tena mara nyingine hivi,
1. “Hujathibitisha kuwa Polepole kajiuzulu kwa hila ya kisiasa…”
Kwanza kabisa, hoja ya "kuthibitisha" unaitumia kama mvivu wa hoja anayetaka video ya CCTV ya nia ya mtu.
Kama mtu anaacha madaraka leo, kesho anamkashifu aliyemuamini na kumpa nafasi ya uongozi, unahitaji microscope gani kuelewa hiyo ni hila ya kisiasa?
Polepole wakati akila mkate ulionona alikaa kwenye vikao, akavuta chai na per diem, hakugomea chochote, hakujitenga hadharani. Sasa kaona njia ya kuwa shujaa ni kupitia TikTok ya siasa.
Huo si ujasiri, ni ukumbusho wa mtu aliyepokonywa power bank ya kisiasa.
2. “Hajasema yeye ni mtakatifu…”
Hapana, lakini anaongea kama yule aliyekuja kutufundisha Injili ya demokrasia.
Anaongea kana kwamba hakuwahi kuomba kura akimsifu JPM, kana kwamba hatukumuona akiwabeza waliokuwa wakisema aliyosema leo.
Kama hataki kuitwa mtakatifu, aache kuhubiri kama nabii wa mwisho.
3. “Uhuru wa kujieleza ni haki ya kikatiba…”
Haki ya kusema haimaanishi hatuwezi kukupasulia hoja zako hadharani. Mtu akisema serikali imejaa wahuni, hatumjibu kwa harufu ya maua. Tunampiga kwa hoja, kwa kumbukumbu, kwa mantiki, hadi atafute Google Maps ya akili zake. Uhuru wa kusema ni haki yake, uhuru wa kumcheka ni haki yetu.
4. “Polepole hajakaa kimya, utamfanya nini?”
Huu ni mtindo wa hoja za "kibabe za kihuni."
Tunachofanya ni hiki hapa unachokiona, tunampa darasa, tunamtumbukiza kwenye kisima cha mantiki, halafu tunamweka kwenye jua akaukie.
Hatuhitaji kumshitaki mahakamani, wala kumuua (kama ulivyoandika kwa kihoro cha kishamba).
Tunamtwanga kwa hoja hadi mwenyewe aombe afundishwe somo la “Falsafa ya Aibu kwa Wanasiasa Waliokosa Uaminifu.”
Mwisho, kama anayonia ya dhati arejeshe kodi za wananchi na aombe radhi kwa wananchi.
Wewe jamaa unamtetea Polepole kama kaka yako au baba yako vile 😂😂 mtafute akupe tuzo ya kumtetea ila mfundishane kuwa ulaghai sio mzuri next time wananchi watawapiga mawe.... 'Muwe na weekend njema'🙏🙏🙏Polepole kashasema aliyosema kwa kutumia haki yake ya kibinadamu na kikatiba.
Message sent and delivered. Regardless of all, Watanzania wamemsikia kasimama wapi leo.
Wewe usiyependa aliyosema unayetaka kumnyamazisha, hajakusikiliza, kasema aliyotaka kusema.
Utamfanya nini?
Au umekuwa frustrated tu hajafanya ulivyotaka, huna la kumfanya, umeishia ku vent ujinga wako tu JF kwamba anyamaze, wakati chances are hata hakujui wala kukusoma.
Utamfanya nini?
Mpaka sasa hujaelewa kuwa simtetei Polepole. Nimesema Polepole si msafi hivyo ana contradictions nyingi, nimezitaja hapo juu. Nimezitaja kama critique ya Polepole, na pia nikatoa critique kwa wanaotumia contradictions hizo kama sababu ya kumtaka Polepole asiseme anavyotaka leo.Wewe jamaa unamtetea Polepole kama kaka yako au baba yako vile 😂😂 mtafute akupe tuzo ya kumtetea ila mfundishane kuwa ulaghai sio mzuri next time wananchi watawapiga mawe.... 'Muwe na weekend njema'🙏🙏🙏
Sawa uchwara, wacha chenga 😂😂We jamaa chenga sana na viqoutes vyako uchwara hivi.
Sawa ngumbaru mwenzangu. Siongezi neno😂😂Mpaka sasa hujaelewa kuwa simtetei Polepole. Nimesema Polepole si msafi hivyo ana contradictions nyingi, nimezitaja hapo juu. Nimezitaja kama critique ya Polepole, na pia nikatoa critique kwa wanaotumia contradictions hizo kama sababu ya kumtaka Polepole asiseme anavyotaka leo.
Ila wewe ngumbaru hujui kusoma kwa ufahamu, hujaziona.
Natetea haki ya kikatiba na kibinadamu ya watu kusema wanavyotaka.
Haki ambayo wewe unataka kuiminya kwa kumnyamazisha Polepole kwa censorship.
Huelewi tofauti ya mtu kutetea haki ya kikatiba na kibinadamu na mtu kumtetea Polepole.
Kwa sababu wewe ni ngumbaru huwezi kufanya abstract thought fikra zako fupi zinaishia kumjadili mtu, huwezi kujadili hoja. Ama unajitoa akili tu kutetea watawala.
You are an ignoble imbecile, a calcified cretin.