Sadaka huanza nyumbani nami naanza humu kunyumba JF!
Dada zangu nina salamu kutoka kwa jamaa kutoka Amerika ya kusini. Msishangae! Nilikuwa Balozi wenu wa kutangaza sifa njema moja ya wanadada wa Bongo. Jamaa alishangaa sana kuwa duniani kuna wanadada wenye sifa kama hiyo. Namna alivyovutiwa aliniahidi atakapotaka kuowa basi atawasiliana nami ili aje apate dada yangu mmoja.
Naamini mtaniunga mkono kuwa kweli sifa hiyo dada zangu wanayo!
Huyo jamaa ni mtundu sana! Aliniuliza kipindi cha miezi sita nikiwa masomoni (tulikuwa pamoja nje) mke wangu anapata wapi chukuchuku? Aguwa nilimwambia nini.