Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza ndugu huyu kwa uwekezaji mkubwa alioufanya huko Arusha kwenye Club inayojulikana kwa jina la Carnival(SunDown) kama sijakosea...
Kwa mwanzoni nilipoifahamu Carnival ilikuwa imechangamka sana kuanzia mazingira,kumbi,club,bar,eneo la michezo ya watoto na hata nyumba za kulala wageni...mazingira ya eneo hili pia yalikuwa yakivutia sana...
Kwa sasa sijui nin kimelikumba eneo hili..Mazingira ni machafu,wateja hakuna,muhudumu kabaki mmoja na mpishi...
Pamoja na kutokujua nin kimetokea ningependa nikushauri haya..
Tafuta Managemet nyingine iweke pale,vinginevyo eneo lile linaamgamia..hata kama pesa za madini zipo au zimekata tizama uwekezaji ule...
Ukishindwa kabisa tafuta mtu upakodishie ili aweze kupaendeleza..
Yangu ni hayo tu,naamin wana arusha watakufikishia ujumbe...