Salam za mwaka mpya

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,014
1,498
Kwenu wakuu Great thinkers:
Kwanza niwatakieni afya njema,amani,kheri,mafanikio na barka za mwaka mpya. Pili ningependa kuzungumzia mafanikio na dosari nilizoziona kutokana na mada na hoja zetu kwa mwaka uliopita ili tuweze kuboresha mtandao wetu pendwa na wenye hadhi ya Great thinkers wa Jamii forum JF.tuna mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo kuelimishana kwa kubadilishana mawazo, kuanzisha mada na kuhoji mambo mbalimbali kwamanufaa yetu na taifa kwa jumla, faida nyingine kubwa ni kuongezeka kwa wanachama, bila kuangalia umri wao maadam wamekidhi vigezo wanastahili heshima.hawa wageni wanaweza kuwa na mapungufu madogomadogo yanayotokana na ugeni wao, iwapo waliowazoefu watawabeza hakutakua na faida yoyote, ila wale waliowazoefu wakijitolea kuwasaidia na wakakomaa kifikra hakika JF itakua chuo na wana JF watastahili kuitwa Great thinkers, bila kuongeza tofauti ya JF na Facebook itaonekana. Iwapo tutaendeleza dharau na kutokujali JF itapoteza heshima yake na wanachama wake kuitwa Great thinkers itakua mzaha uliopitiliza."kwaheri mwaka wa zamani karibu mwaka mpya".
 
Back
Top Bottom