Salad ya maharage machanga, viazi mviringo na nyanya

Kijini

Member
Aug 17, 2007
36
6
Mahitaji: Viazi mviringo nusu kilo- vichemshe na maji mengi yenye chumvi bila kuvimenya
Maharage machanga nusu kilo- yachemshe na maji mengi pia yenye chumvi
Mwaga maji ya kuchemshia toa maganda ya viazi. Hifadhi viazi na maharage kwa kutenganisha katika jokofu.
Nyanya 4/5 -zilizomenywa na kutolewa mbegu, zikate vipande vya wastani
giligilani ya majani kodogo
Dressing: chumvi 1/2 kijiko cha chai, ndimu vijiko 4 , mafuta ya mzaituni vijiko 4, pilipili manga ya kusagwa

Kata vipande vya wastani viazi, maharage, nyanya na uvichanganye katika bakuli kubwa, mailizia kwa kuweka giligilani
Changanya chumvi, ndimu, mafuta ya mzaituni na pilipili manga katika bakuli ndogo pembeni, hii utaweka katika sahani yako ukiwa mezani. Unaweza tunza saladi yako kwa siku 2-3 katika jokofu, waweza ichangamsha zaidi kwa kuongezea yai la kuchemsha.
DSC_0031.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom