MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Sera za ccm ni kutumia vyombo vya dola kwenye mambo ya kiuchumi? Hiyo 2020 utapima sera wakati vyombo vya dola ndio vitatumika kuhakikisha ccm inatangazwa washindi? Huhitaji kuhubiri sera kwenye nchi ambayo vyombo vya dola vinaratibu matakwa ya watawala.
Unachoshindwa kuelewa ni kuwa wanasiasa wa upinzani wanatakiwa walete sera mbadala tuzipime na hizo "sera za CCM za kutumia vyombo vya dola kwenye uchumi".
Sasa badala ya kutuletea sera zao mbadala ili tuzijadili, wanachofanya ni kutuletea chagizo (slogan) za uchaguzi mkuu tuzijadili. Huoni kama hili tatizo la msingi kwa hawa wanaojiita wapinzani.
Au wewe unadhani wananchi wengi watawapa kura kwa sababu wana slogan nzuri?