Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Mheshimiwa Rais, mimi ni mpiga kura wako ambaye nimekuwa sifurahishwi na maneno yanayoanza kuzoeleka sasa kama misamiati sahihi ya kuwapa matumaini yasiyokuwepo ama kwa sababu hamna utashi wa kisiasa ama hamna uwezo (ninyi kama wanasiasa) kuyatekeleza na badala yake inakuwa kana vile siye ni midoli yenu ya kujiburudisha nayo.
Naongelea maneno ambayo wewe na wanasiasa wenzako mnapenda kuyatumia kama haya hapa:
n.k., n.k. tatizo langu kubwa ni kwamba kama hizi tuta- zingekuwa tume- au tuna- tungekuwa hatuko kwenye hili janga la umasikini wa kutisha, nashauri ama msitupe matumaini makubwa kuliko uwezo wa serikali yako kwani kufanya hivyo ni kutokutuheshimu sisi wapiga kura wenu kwa kutudaganya vitu ambavyo ama hamfanyi ama hamna uwezo navyo
- Tutawapatia wanafunzi wote wa Tanzania Komputa
- Tutajenga barabara za kupita juu kwenye mji wa Dar es Salaam
- Tutaboresha masilahi ya wafanyakazi
- Tutapeleka maji ya ziwa Viktoria hadi Tabora
- Tutaunganisha kila makao makuu ya mkoa kwa njia ya rami
TUTAFANYA MABADILIKO MAKUBWA NDANI YA CHAMA! Kweli matuta yamekuwa mengi!
hapa nisamehe kabisaaaaaaaaTatizo siyo Mheshimiwa Rais bali watendaji wake kwani Raisi akisema kitu HILO NI AGIZO linalopaswa kufanyiwa kazi. Nimesikia vile vile amesema shule zitaunganishwa kwenye Mkonga wa taifa ili utumike kufundishia; sasa sijui hizo computer zitawashwa kwa Solar au huu umeme wa Tanesco ambao hauna uhakika!!!
Tatizo siyo Mheshimiwa Rais bali watendaji wake kwani Raisi akisema kitu HILO NI AGIZO linalopaswa kufanyiwa kazi. Nimesikia vile vile amesema shule zitaunganishwa kwenye Mkonga wa taifa ili utumike kufundishia; sasa sijui hizo computer zitawashwa kwa Solar au huu umeme wa Tanesco ambao hauna uhakika!!!

Vincent, twende taratibu kwanza. Tatizo sio Raisi? Ni watendaji wake?
Raisi ni nani?
Watendaji ni nani?
Kama agizo lake halijafanyiwa kazi anatoa agizo lingine au anafanyaje?
Tujadili.
Jamani mnanifunja mbavu, hilo agizo analotoa mh. Rais, analitoa akiwa jukwaani ili afurahishe wananchi na wafuasi wake. Je hao watendaji wake amewapa maagizo kimaandishi? Mnadhani watendaji wa serikali wanafanyia kazi hotuba za majukwaani? Rejea maagizo aliyotoa waziri wa afya kuhusu suala la babu Loliondo, mkuu wa mkoa alijibu hafanyii kazi maagizo kupitia Tv.Vincent, twende taratibu kwanza. Tatizo sio Raisi? Ni watendaji wake?
Raisi ni nani?
Watendaji ni nani?
Kama agizo lake halijafanyiwa kazi anatoa agizo lingine au anafanyaje?
Tujadili.
Ha ha haaaaaaa Henge kweli matuta kibao huenda yatakuwa mabampsTUTAFANYA MABADILIKO MAKUBWA NDANI YA CHAMA! Kweli matuta yamekuwa mengi!
ebo kakaa miaka mitano pale, alikuwa anjifunza?Acheni kuwa mlengo usio na mwelekeo tusubiri miaka 4 ndio tufanye tathmini hayakutimia tufanye uamuzi hizi propaganda za ushabiki hazina tija
hapa nisamehe kabisaaaaaaaa
Tatizo namba moja la nchi hii kwa sasa ni JAKAYA KHALFAN MRISHO KIKWETE bila chenga.
Vincent, twende taratibu kwanza. Tatizo sio Raisi? Ni watendaji wake?
Raisi ni nani?
Watendaji ni nani?
Kama agizo lake halijafanyiwa kazi anatoa agizo lingine au anafanyaje?
Tujadili.
Mkuu naomba kutofautiana na wewe, kama hayo maagizo hayatekelezwi na mtoa maagizo hawawajibishi nani wa kulaumiwa? Urais siyo lelemama
There you are Msando....
Udhaifu wa kiongozi huthibitishwa na watendaji walioko chini yake...
Ni sawa na kuwa na paka asiekimbiza panya, panya watacheza na kufanya kila kituko ndani ya nyumba,
Wa kulaumiwa na mwenye nyumba ni paka kwa kule kuacha uhuru....
Tatizo la JK ni Laissaze Affaire na hawezi kufuatilia utendaji wa walio chini yake
Ninachoelewa, kiongozi akitoa tamko watendaji wanatetemeka na kupigana vikumbo kutekeleza, huyo ndie kiongozi imara,
Lakini kiongozi anaetoa tamko then watendaji wanamngoja wampe mgongo wamng'ong'e na kutupilia agizo lake lazima ana upungufu tena ulio wazi mpaka kwa watendaji wake kuwa HANA UBAVU WA KUWACHUKULIA HATUA YOYOTE
Tatizo siyo Mheshimiwa Rais bali watendaji wake kwani Raisi akisema kitu HILO NI AGIZO linalopaswa kufanyiwa kazi. Nimesikia vile vile amesema shule zitaunganishwa kwenye Mkonga wa taifa ili utumike kufundishia; sasa sijui hizo computer zitawashwa kwa Solar au huu umeme wa Tanesco ambao hauna uhakika!!!
Acheni kuwa mlengo usio na mwelekeo tusubiri miaka 4 ndio tufanye tathmini hayakutimia tufanye uamuzi hizi propaganda za ushabiki hazina tija