Salaam kama hizi tafsiri yake nini?

Salaam kama hizi tafsiri yake nini?

kivutio

Member
Joined
Jun 20, 2014
Posts
58
Reaction score
36
Habari wanajamvi?

Kuna demu ambaye ananiita kaka kwa kuwa mimi na yeye ni kabila moja. Na aliniambia kuwa ana boyfriend wake, basi kwa kulijua hilo mimi nimekuwa namchukulia kama dada na nina heshimu kauli yake kuwa yuko na mahusiano na jamaa.

Lakini yapata wiki sasa dada huyu amezua kamtindo ka kunitumia sms usiku za kunitakia usiku mwema na kila asubuhi ananitumia sms kunitakia asubuhi njema.

Sms zake huwa na vionjo vya kuashiria kuwa mm ni mtu wa muhimu sana kwake. Nauliza wanajamvi salaam hizi tafsiri yake nini?
 
hapana tatizo, we kama ni dada yako si ni wa muhimu kwake. Ndo maana ya vionjo kwenye text
 
Mdogo mdogo itakuwa dear kaka, mara kaka angu mpendwa,kaka kipenzi hatimaye kitu na box sweet bro....
 
Anakujali kaka yake ukizingatia hamkai nyumba moja.......
 
Cha kushangaza nini? Si umesema unamchukulia kama dadako, naye anakuchukulia hivyo hivyo. Nifikiriacho ni wewe ndiye uliyeanza kumuangalia kwa jicho la tatu. Kama uko njia panda na wahisi anamaanisha kitu, basi muulize! Humu jamvini hamna mwenye jibu sahihi, yote utakayopata humu ni maoni na mitazamo ya watu. Ajuaye na mwenye jibu kamili ni huyo huyo "dadako"!
 
...asa wewe ndo unapotosha maana,mtu kukuonyesha kuwa wa muhimu kwake sio lazima awe anakutaka kilove...
 
Muulize anaekutumia, atakupa jibu la ukweli.

Hapa tunajaribu tu
 
watu wengine bwana! Huyo "dada" yako umepoteza mawasiliano naye? Kama jibu ni hapana kwanini usimuulize yeye badala yake unauliza humu?
 
sa we ckiliza kwanza akibadlisha salam uje tena
ts too early to conclude... unaeza. ukaitwa kaka na ukala mzigo na ukaitwa bebi ukaishia kuita watu shemejiiiii
 
we ushampenda! dada yako af unataka tena ushauri???? akituma txt yoyote wee mwambie asante dada! ili undugunization mlouanza udumu!
 
Weka vionjo vya msg zake
Mifano 3 ya vionjo hivyo ni:-
1. Mpendwa nikupendaye.....
2. Ni kawaida yangu kumuamsha nimpendaye sana. Asubuhi njema.
3. Chezea mimi wewe, ukinichunia nakusalimia. Ukinichukia nakupenda sana na ukiwa bize nakusumbua.
 
Back
Top Bottom