Sal Davis na Mimi 2006 -2016 (4)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,486
Reaction score
33,036
SAL DAVIS NA MIMI 2006 - 2026

Katika urafiki wangu na Sal Davis nimeweza kumsikiliza akizungumza maisha yake kuanzia kitongoji cha Makadara, Mombasa (Sasa Prof. Ali Mazrui) alikokulia hadi anapelekwa Manchester akiwa kijana mdogo kusoma shule ya msingi hadi anakuwa mwanamuziki wa sifa wa kimataifa, nimeweza kuandika kitabu cha maisha yake kilichochapwa na Amazon.

Jumatano iliyopita baada ya muda mrefu nimekutana na Sal Davis ambae jana yake alikuwa amesheherekea miaka 85 ya kuzaliwa kwake na tukapiga hiyo picha hapo chini mimi nikiwa nimefikisha miaka 74 mwezi Februari.


 

Attachments

  • 1775407306583.png
    1.6 MB · Views: 1
Tanganyika isiyo na Udini inapendeza sana.
Yoda,
Mwalimu Nyerere akiungwa mkono na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Mwalimu Nyerere akienda kwenye madras ya Sheikh Hassan bin Ameir ameongozana
na Abdulwahid Sykes na Waziri Dossa Aziz.

Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi za TANU misikitini.

Hali ilikuwa hivi.
Labda nikuulize huu udini kauleta nani na nini sababu yake?
 
Unazzungumziaje BAKWATA je ni mkonbozi na msimamizi sahihi WA waisilanu na uisliam kwanini WENGI hawakubali baraza hilo
 
Tanganyika isiyo na Udini inapendeza sana.
Kumbukizi ya Wazee wa Vuguvugu la Uhuru wa Tanganyika


Wazee hawa walikuwa sehemu ya msingi ya vuguvugu la kusaka uhuru. Kutoka kulia waliosimama:
1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3 )
2. Nassoro Kalumbanya (Simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.)
4. Mtoro Ally (Muhonda str.)
5. John Rupia (Misheni kota)
6. Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.)
8. Jumbe Tambaza (Upanga)
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
10. Dossa Aziz (Mbaruku/Somali kipande)
11. Mshume Kiyate (Tandamti)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo)
13. Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
14. Rajab Simba (Kiungani str.)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no. 18, Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana (Aggrey/Kongo)
18. Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
19. Sheh Issa Nasir (Bagamoyo)
 
Mzee mwamedi weka andiko si unajua mambo ya record ni RAHISI Kwa text hasa HIZI mb na kizazi kijacho
OgaBoy,
Ngoja nitafute andiko nikilipata nitaliweka hapa.
Jina langu ni ''Mohamed.''

Soma historia ya BAKWATA hapo chini:

 
Nyerere mkatoliki aliufifisha sana udini Tanganyika kwa kuwa mwanachama mzuri wa madrasa na msikitini pamoja na kuvaa baraghashia.
 
Naomba picha ya wazee walioandika katiba ya kwanza ya nchi.
 
Ni muislamu?
 
Nyerere mkatoliki aliufifisha sana udini Tanganyika kwa kuwa mwanachama mzuri wa madrasa na msikitini pamoja na kuvaa baraghashia.
Yoda,
Sasa nani kasababisha udini ikiwa hali ilikuwa hivyo?
 
Naomba picha ya wazee walioandika katiba ya kwanza ya nchi.
Yoda,
Kuna tatizo moja katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuweka mbele wazee kwa mambo ambayo wao hawakuhusika kuyafanya moja kwa moja.

Matatizo yake ndiyo haya siwezi kujibu swali la wazee walioandika katiba ya nchi kwa kuwa hapakuwa na kitu kama hiki.
 
Mulata Huyo mbegu za wakoloni.
Huyu mody kasharudi kulekule udini,udini,udini haaminiki huyu.
Babu...
Udini kwa kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika?

Kwa kuuliza vipi itaandikwa historia ya TANU asitajwe Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Suleiman Takadir?

Au asitajwe Abdulwahid Sykes aliyeishi na Nyerere nyumbani kwake wakati wa kupigania uhuru?

Kadi ya TANU ya Abdul Sykes ni no 3.

Hawatajwi kwenye historia ya uhuru na ukiuliza unaitwa mdini.
 
Unarudi palepale,
Katika harakati kutafuta uhuru ni wote walikuwepo.
Kuna hawa huwataji kabisa wengi tu ni kwasababu mnaita makafiri.
Wamefanya mengi sana,ila wewe ukikaa ukiamka ni Abdul sykes.
Sally Davis kaimba sana Euro pub kule kawe. Umeeleza vizuri historia mwanzo badae mara wazee wa gerezani,kkoo hao.
Hapo unaharibu
 
1 - Je ni akina nani wanaouendeleza udini?
2 - Je ni akina nani wanaonufaufaika na huu udini unaoendelezwa this time around?
3 - Je Nyerere alifanya makosa kutaifisha shule za makanisa na kulazimisha mpaka zikageuzwa kuwa shule za serikali?
4 - Kwanini baadhi ya raia hawataki rais asemwe kwa makosa yake pale anapokuwa ni wa imani yao? Pindi anapokosolewa tu utetezi unakuwa ni kwamba "mnamchukia kwa kuwa nyinyi ni wa upande wa pili" na pale inapokuwa anapingwa na mtu wa imani yake wanadai ni msaliti kwani kumpinga au kumkosoa ni kuisaliti imani?
4 - Kuna baadhi ya Wakristo na baadhi ya Waislamu ambao vichwa vyao vimejaa sumu za udini mpaka wanakosa kuwa na fikra huru, wanakuwa wanajitahidi kuonyesha kuwa dini yao ndiyo imefanya/inafanya makubwa zaidi ya imani nyingine.

- Ujinga mwingi ni kwa kuwa religious people are so brainwashed to the extent that they can't think and analyse situations freely without being influenced by their religious doctrines.

One billion question ni KIPI KIFANYIKE KUZIWEKA AKILI SAWA ZA WATU WALIOJAA UDINI VICHWANI MWAO? WALE AMBAO KILA JAMBO MPAKA WAINGIZE UDINI(religious biasness) NI ULEMAVU WA AKILI.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…