Punde tu baada ya kubahatika kuona press conference ya Prof. Palamagamba Kabudi, waziri sheria na katiba-Tanzania na mnunuzi wa korosho ndugu Mutembei toka kampuni ya INDO power solutions-Kenya nilifarijika sana. Mununuzi ameweza kununua korosho tani 100,000 kwa Tshs 418 billion.Hii ni sawa na Tshs 4,180 kwa kilo. Ongezeko la bei takribani 33% kwa bei ya korosho ghafi kwa kilo toka mwaka 2009 hadi 2013 kwa wastani wa Tshs 1,372 nchini Tanzania. Lengo la hii mada fupi hapa jamvini nikujaribu kuangalia faida na hasara ambazo tunaweza au tumezipata kutokana na hatua ya serikali kuuza korosho kwa bei ya Tshs4180 kwa kilo nchini Kenya badala ya soko la dunia.
Kwenye press conference, Joseph Kakunda waziri wa viwanda na biashara amesema kwamba “ Wakulima wa korosho wamelipwa Tshs 3,300 kwa kilo bila kukatwa ushuru”. Ukiangalia bei utagunduwa kwamba serikali imepata faida ya takribani Tshs 880(4,180-3,300). Lakini wakati huo huo imepoteza Tshs 495(3,300*0.15)kwa kilo kwenye ushuru. Kawaida wakulima huwa wanakatwa ushuru takribani 15%. Hii inamaana Serikali imeweza kupata faida ya Tshs 385 kwa kilo ambayo ni sawa na takribani 38 billion kwenye sakata zima la korosho. Pia wakulima wamelipwa bei ya juu na msamaha wa kodi takribani 49 billion.
Upande wa pili,Prof. Palamagamba Kabudi, waziri sheria na katiba amesema kwamba “ lengo la raisi John Pombe Makufuli,lilikuwa ni kutafuta masoko ya korosho kimataifa”. Bila shaka lengo la raisi lilikuwa nikutafuta bei nzuri kwenye masoko ya dunia. Ukiangalia bei ya korosho duniani kwa kilo kuanzia mwaka 17 hadi 18, korosho ilikuwa inauzwa kati ya Tshs 9,616($4.22) hadi Tshs 10,596($4.65)3. Lakini sisi tunaweza kuuza $0.60 kwa kilo. Kama Serikali ingeweza kutafuta soko nje ya nchi ingeweza kuuza korosho kwa takribani 1.01 trillion. Zoezi la kuuza korosho Kenya badala ya kwenda kwenye soko la kimataifa, limetupa hasara ya takribani 6 billion pamoja na upungufu wa fedha za kigeni(Dola).
Nakaribisha mjadala
Hatua ya kuuza korosho nchi kenya,Je serikali ya Tanzania imefanya uwamuzi sahihi?