Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Ziara ya ghafla na TBC wapo ! Humdanganyi mtu yeyote ! Halafu badala ya kukagua hivyo viwanda zaidi ya elfu 3 ambamo bila shaka vya mafuta ya kula vimo kwanini anaenda bandarini ?
 
DF344814-B4E1-42C5-8123-B6DC24D145BE.jpeg
Jamaa kamkimbia mzungu kweki lugha ya malkia nomaà
 
Kazi za mawaziri hizo, anaenda Mh Rais, mimi bado nina wasiwasi na watendaji wa hii awamu, sijui kama wanamuelewa Rais. Kwa jinsi ambavyo Rais amekuwa akifuatilia mambo kwa kwenda sehemu husika, nilitegemea kwa kipindi tu hiki cha miaka miwili basi makatibu wakuu, mawaziri wangekuwa wanafuatilia sana mambo haya, lakini toka sakata hili limeanza si waziri wa viwanda, fedha au uchukuzi kuwaona wapo mstari wa mbele kufuatilia hili jambo, sasa leo katoka Rais mwenyewe, na kitu kinarushwa live, jamaani huyu Rais mtaazeesha kwa kufanya kila kazi peke yake!!
MENE MENE TEKELI NA PERESI D.5 25-28
 
Tatizo langu kubwa ni moja. Hata ukiwa nyumbani kwako unaweza kupima mafuta na kujua haya ni crude au refined kwa kigezo cha Free Fatty Acid. Unahitaji Sodium Hydroxide, Ethanol na Indicator(hivi unaunua kwenye maabara ya mtaani tu) na gram 10 za mafuta kufanya neturalization process ambayo kama itachukua muda mrefu sana ni robo saa. Hata mwanafunzi wa darasa la saba akielekezwa anafanya kwa ufanisi mkubwa tu hii kazi. Sasa hiki kilichokuwa kinaendelea kati ya TBS mara TFADA mara mkemia mkuu kwenye maPHD mara waziri yaani naona kizunguzungu.Siku zote hizo wameshindwa kujua kuwa haya mafuta ni crude au refined hadi mgogoro umefika bungeni hadi kwa rais. Kweli mtu akisema yupo frustrated ana haki. Labda niamini kuwa kulitegeshwa upigaji mkubwa. Unless kuna kitu sjaelewa vizuri
 
Jamaa anauliza swali....

Mzungu akianza kuongea na kutolea ufafanuzi yeye anainama chini... akiinuka ananyosha mikono juu... kwa ishara kanakwamba anasema yaishe bhanaa... anashika bega la huyu nashika bega la yule.... yaani !!! Hivi uliyaanza ya nini...

Mwangalie anavokuelezea sasa namna ya kutengeneza mafuta aiseee mda mwingine nikadhani ni Kinyamwanga ndo kinatumika..... aahaahaaaa

Kweli ilikuja na mtumbwi lugha hii

BACK TANGANYIKA
 
Kwani ni nani aliyesema mafuta ya kutoka nje yatozwe kodi kubwa?

Lazima tuwe wap.umbavu kushabikia mambo kama haya. Tunafanywa kuwa hatuna akili. Ni kama mama anamcharaza fimbo mtoto halafu mtoto akianza kulia, anamweleza mwanae asilie.

Mambo ya kijinga kama haya tusishabikie. Unatengeneza tatizo halafu unajifanya unatatua.
 
Nampongeza kaimu Kamishina wa TRA aliyesimama kidete , maana imegundulika haya mafuta siyo CRUDE bali ni mchanganyiko yako Crude yanayotozwa 10% tax , Semi refined 10% na double refined yako Matanki 7 yaliyopaswa kulipiwa 25%. Hongereni TRA kusimamia ukweli huu
 
Ni wendawazimu kusababisha tatizo halafu ujifanye unatatua halafu utegemee kushangiliwa. Lazima uwe mjinga hasa kushangilia mambo kama haya.

Ni miaka mingapi hatujawahi kuwa na tatizo la mafuta wala sukari? Nani aliyesababisha upungufu wa sukari na mafuta?

Aliyeumbwa na uso wa haya, angejitahidi kwenda kimya kimya.
 
Back
Top Bottom