Sakata la ZITTO, Yaliyoko nyuma ya pazia

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,589
Reaction score
28,754
Wakuu nimesikiliza Breaking News Radio One mida hii na hiki ndicho walichokisema.

Mwandishi wa habari (somebody Mwaifuge)aliyekuwa kwenye kikao cha kamati kuu hapo usiku wa jana anadai Zitto Kabwe na Dr Kitila Nkumbo walikua wameanzisha kundi lao maalumu lililokua likiitwa Mkakati wa Mabadiliko ya 2013(MM-2013) likiwa na viongozi wakuu wanne(Zitto, Nkumbo, Jamaa mmoja aliyejulikana kama MM2 ambaye ni kiongozi mwandamizi makao makuu na Mwigamba), na kamati kuu baada ya kugundua hilo walikaa na kutafakari kwa kina hatua za kuchukua.

Watuhumiwa wawili(Zitto na Kitila Nkumbo) wote waliitwa na kuhojiwa na wakakiri Makosa yao na kuomba msamaha kwa makosa yao, lakini pia waliomba wenyewe wajiuzulu nafasi zao ndani ya chama kwa hiyari yao wenyewe.

Baada ya Kamati kuu kutafakari kwa kina wakaamua kukubali ombi lao la wao kujiuzulu lakini pia wakaamuru waandike barua ndani ya siku 14 kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama.

Juhudi za mwandishi kumfahamu huyu MM2 bado ziligonga mwamba lakini anadai ni kiongozi mwandamizi ndani ya makao makuu ya chama pale Kinondoni.
Lakini pia hajazungumzia hatua zilizochukuliwa kwa MWIGAMBA

Stay tuned

source:Radio One breakingNews saa 9:50 mchana
 
Huyo kiongozi mwingine atakuwa niiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....
 
Ilikuwa ni lazima, chama kimeishi naye kwa shaka muda mrefu lakini urafiki wake na ccm unatiashaka na mambo yalivyo ni bora bila yeye kuliko wingi wa mashaka na hofu kila kukicha
 
Mimi nachotaka kusikia sasa ni kwamba ZITTO anaburuzwa polisi, then mahakamani, akakutane huko na Lissu, then Jela basi.
 
Huo ndiyo mwisho wa kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

Ha ha ha, ukiona mwenzako ananyolewa tia maji kiwchwani
 
Wakuu nimesikiliza Breaking News Radio One mida hii na hiki ndicho walichokisema.

Mwandishi wa habari (somebody Mwaifuge)aliyekuwa kwenye kikao cha kamati kuu hapo usiku wa jana anadai Zitto Kabwe na Dr Kitila Nkumbo walikua wameanzisha kundi lao maalumu lililokua likiitwa Mkakati wa Mabadiliko ya 2013(MM-2013) likiwa na viongozi wakuu wanne(Zitto, Nkumbo, Jamaa mmoja aliyejulikana kama MM2 ambaye ni kiongozi mwandamizi makao makuu na Mwigamba), na kamati kuu baada ya kugundua hilo walikaa na kutafakari kwa kina hatua za kuchukua.

Watuhumiwa wawili(Zitto na Kitila Nkumbo) wote waliitwa na kuhojiwa na wakakiri Makosa yao na kuomba msamaha kwa makosa yao, lakini pia waliomba wenyewe wajiuzulu nafasi zao ndani ya chama kwa hiyari yao wenyewe.

Baada ya Kamati kuu kutafakari kwa kina wakaamua kukubali ombi lao la wao kujiuzulu lakini pia wakaamuru waandike barua ndani ya siku 14 kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama.

Juhudi za mwandishi kumfahamu huyu MM2 bado ziligonga mwamba lakini anadai ni kiongozi mwandamizi ndani ya makao makuu ya chama pale Kinondoni.
Lakini pia hajazungumzia hatua zilizochukuliwa kwa MWIGAMBA

Stay tuned

source:Radio One breakingNews saa 9:50 mchana

Asante kwa taarifa. Ila ungetueleza zaidi kidogo kuhusu lengo na madhumuni ya MM-2013. Au utubandikie kabisa ushahidi wa kuwepo hilo kundi. Hii itasaidia kuondoa upotoshaji na pia kuyaelewa malengo kama yalikuwa kwa nia njema au mbaya
 
sisi tuko live jf wewe unaleta habari za radio 1 hapa ? Hivi kuna radio zaidi ya jf ?
 
Hakuna MM2. Hiyo wameweka reserve tu ili wakitaka kumfukuza mtu mwingine kama Lissu baada ya kumtumia vta kutosha wapate sababu ya kumpachika u MM2.
 
fanya kazi yako ya unesi hapo mvomero ,ndugu zako wanauna huko wakiggea ardhi we uko buzy na jf
 
Tujiulize; je, ule mkakati wa CCM wa kuisambaratisha CDM ifikapo 2014 ndio huo ambao ulibebwa na Zitto wa MM2013? Au bado uko mwingine? Kama ndio huo uliokuwa ukisemwa na Wasirra, basi CCM itakuwa itazikwa rasmi 2015?
 
Lakin jamani chama imara ni kile kinachotoa maamuzi sasa namshauri Zitto akae pembeni awadhihilishie kamati kua sio msaliti kwa matendo kama anaipenda nchi yake na chama, nadhani huu utakua sio wakati wa kulumbana na chama,

Kama ambavyo anafanya lowasa ni ACTION zaidi kuliko kulalama hapo tutajua anatufaa
 
Back
Top Bottom