Sakata la Zitto na wenzake: Viongozi wa CHADEMA, tafadhali badilikeni!

Status
Not open for further replies.
Ww achaujinga m4c ilianzishwa kisiasa kwa maslai ya mtu je ippo wapi na ilishia wapi je walionzisha m4c wamekufa ndani ya cdm jb wapo ile ilikuwa kupata kilewalicho taka wakafanikiwa kwa maslai yao sio ya chama

Ukiulizwa utaje hayo maslahi sidhan kama utakuwa na jibu zaidi ya kubwabwaja tu! wote tunajua m4c ilivyotetemesha magamba hadi yakaamua kuhujumu kwa kutumia dola! tulishuhudia mauaji ya raia ili tu kuihujumu,wote tunakumbuka kuwa zoezi la sensa nalo likatumiwa kisiasa kuhujumu oparesheni na hivyo kuvuruga ratiba yake.m4c bado ipo na makamanda wanapiga kazi kwa kwenda mbele!
 
Mwandishi wa makala hii angemshauri Zitto pia aache kuwazogoa viongozi wenzake hadharani (kwa kutumia mitandao na mikutano). Viongozi wa taasisi wanatakiwa waunde na kutenda kitimu Kama wanataka ushindi au maendeleo. Huwezi kuwa ndani ya timu kwa kujitenga na kuwasema wenzio!
 
Umefafanua vizuri Kilaga. Let us think positively na si kutoa povu tu mdomoni kulalama kama alivyofanya Elli. sehemu kubwa ya waraka ile unazungumzia matatizo halisi ya chama na yanahitaji kutatuliwa.

Kama watu wanashindwa kuwajibika kutokana na nyadhifa zao kuyashauri hayo ndani ya vikao halali vya chama huo ndio unafiki wenyewe! kumbuka wajibu wa kamati kuu ambayo wote walikuwa wajumbe wake ni nini? waliaminiwa katika nyadhifa zao kuwa wanao uwezo wa kukishauri chama ,kukosoa na sio kuandaa waraka wenye matusi kwa viongozi wenzao! ukichunguza pro MM wote wanamawazo kuwa chama kinaongozwa na mtu 1 au 2,hata maamuzi ya kamati kuu wanayapotosha kwa kudhani ni ya mbowe au slaa! wenye akili watajiuliza kama kweli waraka una mambo mazuri,ni kwa nini hawakuwahi kuyasema katika vikao halali? kwa nyadhifa zao tulitegemea watimize wajibu wao kwa kukishauri chama kupitia vikao halali na si kufanya siasa za kuviziana! wamekosa sifa za kuwa viongozi wa cdm,
 
Kama watu wanashindwa kuwajibika kutokana na nyadhifa zao kuyashauri hayo ndani ya vikao halali vya chama huo ndio unafiki wenyewe! kumbuka wajibu wa kamati kuu ambayo wote walikuwa wajumbe wake ni nini? waliaminiwa katika nyadhifa zao kuwa wanao uwezo wa kukishauri chama ,kukosoa na sio kuandaa waraka wenye matusi kwa viongozi wenzao! ukichunguza pro MM wote wanamawazo kuwa chama kinaongozwa na mtu 1 au 2,hata maamuzi ya kamati kuu wanayapotosha kwa kudhani ni ya mbowe au slaa! wenye akili watajiuliza kama kweli waraka una mambo mazuri,ni kwa nini hawakuwahi kuyasema katika vikao halali? kwa nyadhifa zao tulitegemea watimize wajibu wao kwa kukishauri chama kupitia vikao halali na si kufanya siasa za kuviziana! wamekosa sifa za kuwa viongozi wa cdm,

Watu wanashauriwa na majambazi kama lema anajulikana unategemea nn
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe yuko kwenye mgogoro wa kisiasa na Chama Chake.Katika Siasa hili ni jambo la kawaida kabisa,Bahati mbaya chanzo na unakoelekea mgogoro huu ndio kitu kinachosikitisha.

Zitto Kabwe ametuhumiwa based on hearsay kwenye mambo mengi kama ukosefu wa nidhamu, uchonganishi na kushindwa kushiriki kwenye shughuli za Chama.

Ukiyatazama makosa haya utagundua kuwa si makosa yaliyotakiwa kuwekwa wazi kwenye vyombo vya habari,wala kusababisha mgawanyo unaojitokeza kwa hali ya sasa, na kwa kiasi kikubwa pande zote 2 zina makosa ya kutosha kwenye hili. Lakini kubwa zaidi ni jinsi gani Chadema wanashindwa ku-control party cadres wao hasahasa wale wa chini, kina Yericko, Ben na we wengine wanaotumia pseudonyms.

Vijana hawa wamefanya damage kubwa sana kwa Image ya Chadema katika kipindi cha mwezi uliopita. Wanaorodhesha vitu ambavyo ni hearsay halafu wanategemea watu wavikubali kijumla jumla.kwa mimi na wengine tusiofuata upepo,na tusio na maslahi yoyote ya kinachoendelea CDM wala CCM, tunatazama kinachoendelea kwa masikitiko makubwa.

Kutwa kucha vijana hawa kazi yao ni kuorodhesha uzushi, wakishindwa kuelewa kuwa hakumaanishi utaaminisha kwa mamilioni ya watanzania kuwa ZItto anafanya mambo yasiyo na tija na taifa. Kusema chenge ana $1M offshore ni fact, kwa sababu its proven beyond doubt, kusema kuwa Zitto ni mwenyekiti wa PAC iliyosimamia mashirika kadhaa, na mawaziri kadhaa kuwajibishwa, it's proven beyond doubt,hadithi za mwigulu kukutana na zitto "havintishi bar" kuihujumu Chadema ni umbea mabao haujawa proven,kwa mtu mzima kama mimi siwezi kupoteza muda kujadili upuuzi huu.

Tuhuma 11 mlizomtuhumu zito (mbali na kuwa based on hearsay) ziko open kwa kila mwenye macho na masikio-wengi wanakubali hazina weight ya kumua-abuse kiongozi wenu mstaafu kwa level hii.

Mnasema waraka uliowekwa kwenye vyombo vya habari sio wenyewe at the same time mnazunguka nchi nzima kumnanga nao.mnasema kuwa Zitto ame-consipre kumng'oa uenyekiti mbowe kwa waraka alioandika Kitila Mkumbo.

Mbaya zaidi, ukiondoa lugha isiyo ya kistaarabu iliyotumika kwenye waraka 90% ya kilichoandikwa ni matatizo makuu ambayo Chadema kama taasisi inatakiwa iyashughulikie, uitely,sio kupiga kelele kwenye media kila siku.


Kwa wale waliowahi kujibishana na baadhi ya hawa Cadre wa Chadema humu ndani atakubaliana na mimi kuwa Lugha wanazotumia ni Msaliti, mhaini, hafai na majina mengine mengi ambayo si sahihi kumuita aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chama aliyefanya mengi kwa chama hicho.

Ukiwauliza wao wameifanyia nini Chadema hadi kuwa na kifua cha kumrushia mawe Zitto, sidhani kama watakujibu la maana. Nimewajibu baadhi,si kila mtu yuko "naive" kama wao wanavyofikiria, asilimia kubwa (>80%) ya wafuasi wa kambi zote mbili, ZITTO vs SLAA/MBOWE/CHADEMA wana makosa makubwa juu ya kinachoendelea.Si Sahihi kuorodhesha yale ambayo Zitto ameikosea Chadema,kwa lugha za kejeli,Kesho Mbowe akiwaambia Dr. Slaa Hafai ni msaliti, ni Mhaini, mtamsikiliza jumla jumla na kusahau yale mema ambayo mzee huyu ameifanyia Chadema? Kwa mwendo huu sitashangaa.

Kila Binadamu ana mapungufu yake, Chadema wanatakiwa kumhukumu Zitto kwa yale aliyoifanyia CHADEMA sio yale aliyoshindwa kufanya, au yale CHAMA kilidhani angefanya na hakufanya. Kwa wengi wenu kina Ben Saanane, Yericko Nyerere etc, sidhani kama mmeifanyia mengi CHADEMA kuliko yale ambayo Amefanya Zitto, Nyie mnachofanya kila siku ni kusema yale aliyokosea tu, bahati mbaya viongozi wenu vichwa vya moto wanawasikiliza nyie zaidi.

Sijawahi kumuona Mnyika au Slaa akifungua post hata siku moja humu kusema Zitto hajafanya hiki na hiki,na hata baada ya huu mgogoro ni viongozi wachache ambao hata kwa kulazimishwa wanakosa hekima wanaoyasema yale ya uzushi yasiyo na usahidi,Kwenye Mikutano yake Dr. Slaa amesikika akisema huyu Kijana ataadhibiwa( hata mimi naamini anastahili hatua za kinidhamu) kwa kukosa nidhamu, sijaona Dr. Slaa akisema Zitto ameiuza CHADEMA kwa CCM au ZITTO anashirikian ana Mwigulu. Saa nyingine mtu anaweza kufikiria hawa vijana wametumwa kumchokonoa ZItto ili abwabwaje, na kwa kukosa Busara na yeye kaachia breki zote.

Ni jambo lilio wazi GOGORO hili haliwaongezei idadi ya wanachama wala wapiga kura, ila ni jambo liliowazi kuwa mmewapunguza kwa kiasi kikubwa, kama mnabisha subirini wakati wa uchaguzi.uharibifu mlioufanya katika kipindi cha mwezi mmoja ni zaidi ya uharibifu wa aina yoyote ambao Zitto kabwe ameufanya Chadema kwa Miaka 15.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vya Siasa, Mmeipa CCM "clout" ya kusimama majukwaani na Kutoa Ushauri kwa CHADEMA, na jinsi msivyojua maana ya kejeli nyie mnaona CCM wanafanya hivyo kwa kuwa wanampenda sana ZITTO. Ukisikia kubezwa ndio huku. Mnachofanyiwa na CCM hakina Tofauti na Putin kumpa OBAMA somo la Demokrasia,Si wka sababu Urusi ya Putin kuna Demokrasia Kuliko Marekani, hapan ni kwa sababu kwa wanasiasa Nguli kama Putin Kuiacha opportunity y a"snowden" kupita bila kuitumia ni sawasawa na Raul Kukosa goli kwenye 18, au Messi kuacha kupiga chenga, haiwezekani.

Issue ya Snowden inaelezea ni kwa kiasi gani the mighty "USA" has fallen kufikia level ya chini kabisa ya kina Urusi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza. Hakumaanishi Snowden ana Urusi ni marafiki. Kunamaanisha ADUI wa ADUI yako ni Marafiki,CCM pamoja na upuuzi wao wanalifahamu hili kwa kuwa wana "proper" political Stratergists. Msifikiri kuikomboa kusini ya afrika kulihitaji bunduki peke yake,kuna mijamaa mle ndani ni mipanga mbinu mizuri tu, ikiamua kuacha kuhujumu uchumi wetu. Sasa bahati mbaya kwa sababu CHADEMA sasa kumejaa vichwa moto, nyie mnashindwa kuona picha kubwa, mnashindwa kuona jinsi gani mnabezwa, CHADEMA kuwa na wanaharakati ni jambo moja, kuwa na wanasiasa wapanga mikakati ni jambo lengine, hawa wapili hamna na mnawahitaji sana sana sana.


Kinachoendelea CHADEMA Sasa hivi kinaonesha kuwa Wakuu wa Chama hiki wanaamili kuwa wote wanatakiwa kuwa na mtazamo moja katika kila jambo, na kila anayepingana nao ni mnafki,msaliti au mhaini. hii si sahihi,hili si jambo zuri kwa ustawi wa chama chenu.Amkeni na mjitazame upya-Kimya Kimya,sio kutupigia makele kucha kutwa.

Kumzodoa Zitto Hadharani hakuijengi CHADEMA,Mnawapa nafasi wabaya wenu na maadui zenu kutumia udhaifu wenu kuwadhoofisha.
Hivi nyie Ccm, hamna habari za idi ya Zitto? Hivi huyu Zitto ni zaidi ya mawaziri wenu wanne wali ongoza askari wenu kubaka, kuua, kufanyia watu bitu vya kijinga visivyo na nyuma wala mbele???? Ufike muda muonyeshe kuwajali Watanzania na sio kuongea pumba kwa manufaa ya chama mfu badala ya kujadili mustakabali wa Taifa, kama mlimpa Zitto hela aisambaratishe Chadema ni kwamba hela zimeliwa na issue imebuma, tafuteni mbinu nyingine
 
Walimu wana kazi sana

we have a problem in this society, if someone my define chama cha siasa in this context what do you expect

conflicts are happening even in churches and mosques........they are there. It is unique art and heart of leadership skills to resolve them peacefully for the betterment of that particular institution

sikufundishi tena, kajifunze basics

You look to be one of the major funny among that society because you've looked the context in a short run. Let ZZK screw up alone, if he had been serious for what had been standing for " wellfare ya wananchi", he can join and keep on in any part and will get support, rather than weakening the strength that is gained by major opposition part, There is a a back of all this, mind that do u think wale watawala msonge wanataka kutoka madarakani? .
 
Lakini naombeni mnifumbue Macho,hivi Daftari la wapiga kura limerekebishwa,na je M4C INAENDELEA LINI? CCM inawahadaa watu kwa taarifa za kina Lembeli na nyie mnaona ni issue,waacheni wafu wazikane wenyewe,Sisi tunahitaji maambo yafuatayo
1.Marekebisho ya Daftari la kudumulawapia Kura
2.Issue ya Zitto, kamati kuu iitishwe upya na maamuzi yafikiwe upya na yeye Zitto asikosekane .
3.Hatutaki kuonea issue ya Zitto nje ya vikao
4.Slaa andelee na Mapambano tupate katiba bora
5.Tuendelee na kukusanya wanachama zaidi.
 
Kiburi na majigambo yanayoambtana na matusi kwa viongozi wake wa chadeyanachochewa na viongozi hao kusita kumvua uanachama zzk, fukuzeni atakuwa hana ubavu wowote wa kukiathiri chama
 
Hajui tu kuwa anajichimbia kaburi heri angenyamaza kimya angeonekana ana busara zaidi. Nani mfadhili wa mikutano yake? Tafakari
 
Hivi nyi vijana shule mlikwenda kweli hata kuandika tu ni tabu,kama hawa ndo vijana wa chadema bora ccm itawale milele.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom