Sakata la Zitto na wenzake: Viongozi wa CHADEMA, tafadhali badilikeni!

Status
Not open for further replies.

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
3,950
Ni ukweli ulio wazi kuwa aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe yuko kwenye mgogoro wa kisiasa na Chama Chake.Katika Siasa hili ni jambo la kawaida kabisa,Bahati mbaya chanzo na unakoelekea mgogoro huu ndio kitu kinachosikitisha.

Zitto Kabwe ametuhumiwa based on hearsay kwenye mambo mengi kama ukosefu wa nidhamu, uchonganishi na kushindwa kushiriki kwenye shughuli za Chama.

Ukiyatazama makosa haya utagundua kuwa si makosa yaliyotakiwa kuwekwa wazi kwenye vyombo vya habari,wala kusababisha mgawanyo unaojitokeza kwa hali ya sasa, na kwa kiasi kikubwa pande zote 2 zina makosa ya kutosha kwenye hili. Lakini kubwa zaidi ni jinsi gani Chadema wanashindwa ku-control party cadres wao hasahasa wale wa chini, kina Yericko, Ben na we wengine wanaotumia pseudonyms.

Vijana hawa wamefanya damage kubwa sana kwa Image ya Chadema katika kipindi cha mwezi uliopita. Wanaorodhesha vitu ambavyo ni hearsay halafu wanategemea watu wavikubali kijumla jumla.kwa mimi na wengine tusiofuata upepo,na tusio na maslahi yoyote ya kinachoendelea CDM wala CCM, tunatazama kinachoendelea kwa masikitiko makubwa.

Kutwa kucha vijana hawa kazi yao ni kuorodhesha uzushi, wakishindwa kuelewa kuwa hakumaanishi utaaminisha kwa mamilioni ya watanzania kuwa ZItto anafanya mambo yasiyo na tija na taifa. Kusema chenge ana $1M offshore ni fact, kwa sababu its proven beyond doubt, kusema kuwa Zitto ni mwenyekiti wa PAC iliyosimamia mashirika kadhaa, na mawaziri kadhaa kuwajibishwa, it's proven beyond doubt,hadithi za mwigulu kukutana na zitto "havintishi bar" kuihujumu Chadema ni umbea mabao haujawa proven,kwa mtu mzima kama mimi siwezi kupoteza muda kujadili upuuzi huu.

Tuhuma 11 mlizomtuhumu zito (mbali na kuwa based on hearsay) ziko open kwa kila mwenye macho na masikio-wengi wanakubali hazina weight ya kumua-abuse kiongozi wenu mstaafu kwa level hii.

Mnasema waraka uliowekwa kwenye vyombo vya habari sio wenyewe at the same time mnazunguka nchi nzima kumnanga nao.mnasema kuwa Zitto ame-consipre kumng'oa uenyekiti mbowe kwa waraka alioandika Kitila Mkumbo.

Mbaya zaidi, ukiondoa lugha isiyo ya kistaarabu iliyotumika kwenye waraka 90% ya kilichoandikwa ni matatizo makuu ambayo Chadema kama taasisi inatakiwa iyashughulikie, uitely,sio kupiga kelele kwenye media kila siku.


Kwa wale waliowahi kujibishana na baadhi ya hawa Cadre wa Chadema humu ndani atakubaliana na mimi kuwa Lugha wanazotumia ni Msaliti, mhaini, hafai na majina mengine mengi ambayo si sahihi kumuita aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chama aliyefanya mengi kwa chama hicho.

Ukiwauliza wao wameifanyia nini Chadema hadi kuwa na kifua cha kumrushia mawe Zitto, sidhani kama watakujibu la maana. Nimewajibu baadhi,si kila mtu yuko "naive" kama wao wanavyofikiria, asilimia kubwa (>80%) ya wafuasi wa kambi zote mbili, ZITTO vs SLAA/MBOWE/CHADEMA wana makosa makubwa juu ya kinachoendelea.Si Sahihi kuorodhesha yale ambayo Zitto ameikosea Chadema,kwa lugha za kejeli,Kesho Mbowe akiwaambia Dr. Slaa Hafai ni msaliti, ni Mhaini, mtamsikiliza jumla jumla na kusahau yale mema ambayo mzee huyu ameifanyia Chadema? Kwa mwendo huu sitashangaa.

Kila Binadamu ana mapungufu yake, Chadema wanatakiwa kumhukumu Zitto kwa yale aliyoifanyia CHADEMA sio yale aliyoshindwa kufanya, au yale CHAMA kilidhani angefanya na hakufanya. Kwa wengi wenu kina Ben Saanane, Yericko Nyerere etc, sidhani kama mmeifanyia mengi CHADEMA kuliko yale ambayo Amefanya Zitto, Nyie mnachofanya kila siku ni kusema yale aliyokosea tu, bahati mbaya viongozi wenu vichwa vya moto wanawasikiliza nyie zaidi.

Sijawahi kumuona Mnyika au Slaa akifungua post hata siku moja humu kusema Zitto hajafanya hiki na hiki,na hata baada ya huu mgogoro ni viongozi wachache ambao hata kwa kulazimishwa wanakosa hekima wanaoyasema yale ya uzushi yasiyo na usahidi,Kwenye Mikutano yake Dr. Slaa amesikika akisema huyu Kijana ataadhibiwa( hata mimi naamini anastahili hatua za kinidhamu) kwa kukosa nidhamu, sijaona Dr. Slaa akisema Zitto ameiuza CHADEMA kwa CCM au ZITTO anashirikian ana Mwigulu. Saa nyingine mtu anaweza kufikiria hawa vijana wametumwa kumchokonoa ZItto ili abwabwaje, na kwa kukosa Busara na yeye kaachia breki zote.

Ni jambo lilio wazi GOGORO hili haliwaongezei idadi ya wanachama wala wapiga kura, ila ni jambo liliowazi kuwa mmewapunguza kwa kiasi kikubwa, kama mnabisha subirini wakati wa uchaguzi.uharibifu mlioufanya katika kipindi cha mwezi mmoja ni zaidi ya uharibifu wa aina yoyote ambao Zitto kabwe ameufanya Chadema kwa Miaka 15.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vya Siasa, Mmeipa CCM "clout" ya kusimama majukwaani na Kutoa Ushauri kwa CHADEMA, na jinsi msivyojua maana ya kejeli nyie mnaona CCM wanafanya hivyo kwa kuwa wanampenda sana ZITTO. Ukisikia kubezwa ndio huku. Mnachofanyiwa na CCM hakina Tofauti na Putin kumpa OBAMA somo la Demokrasia,Si wka sababu Urusi ya Putin kuna Demokrasia Kuliko Marekani, hapan ni kwa sababu kwa wanasiasa Nguli kama Putin Kuiacha opportunity y a"snowden" kupita bila kuitumia ni sawasawa na Raul Kukosa goli kwenye 18, au Messi kuacha kupiga chenga, haiwezekani.

Issue ya Snowden inaelezea ni kwa kiasi gani the mighty "USA" has fallen kufikia level ya chini kabisa ya kina Urusi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza. Hakumaanishi Snowden ana Urusi ni marafiki. Kunamaanisha ADUI wa ADUI yako ni Marafiki,CCM pamoja na upuuzi wao wanalifahamu hili kwa kuwa wana "proper" political Stratergists. Msifikiri kuikomboa kusini ya afrika kulihitaji bunduki peke yake,kuna mijamaa mle ndani ni mipanga mbinu mizuri tu, ikiamua kuacha kuhujumu uchumi wetu. Sasa bahati mbaya kwa sababu CHADEMA sasa kumejaa vichwa moto, nyie mnashindwa kuona picha kubwa, mnashindwa kuona jinsi gani mnabezwa, CHADEMA kuwa na wanaharakati ni jambo moja, kuwa na wanasiasa wapanga mikakati ni jambo lengine, hawa wapili hamna na mnawahitaji sana sana sana.


Kinachoendelea CHADEMA Sasa hivi kinaonesha kuwa Wakuu wa Chama hiki wanaamili kuwa wote wanatakiwa kuwa na mtazamo moja katika kila jambo, na kila anayepingana nao ni mnafki,msaliti au mhaini. hii si sahihi,hili si jambo zuri kwa ustawi wa chama chenu.Amkeni na mjitazame upya-Kimya Kimya,sio kutupigia makele kucha kutwa.

Kumzodoa Zitto Hadharani hakuijengi CHADEMA,Mnawapa nafasi wabaya wenu na maadui zenu kutumia udhaifu wenu kuwadhoofisha.
 
Nasadiki maneno yako 100% CDM tumejisahau kushughulikia matatizo ya chama nakujipa imani eti 2015 magogoni tunaenda kwani kura watapiga watu wa kaskz na Dar kuna mahali mm nimezunguka vijj flan bara hakuna kitu inaitwa Cdm na sehemu kubwa watu wa vjjn ndio wapiga kura.

Wamekaa kupeana posho tu kwenye mitandao kumfitin zzk ambae ana utaifa wakati hata ofisi za chama angalau kila kata hakuna,eti ruzuku ya jimbo inapewa elf 50, na wenyewe kujipangia mishahara minono.

CDM kazi bado tunayo ila nasikitika chama kinapotezwa hvhv na wakora.
 
Mmejipindaaaa ndio mmekuja na huuu uharo..... Eti hearsays! Go to hell nyie sio Chadema na mambo ya CDM hayawahusu. Mwenyewe kakiri halafu Kuna vijitu vinatokea na kupinga! Nyie ni akina nani?
 
Eti Cdm kitadhoofika, ndoto za alinacha hizo wewe. Cdm haiendeshwi na mtu mmoja wewe. Alikikuta chama na alikua na mchango sawa na wanachama wengine tu
 
Mmejipindaaaa ndio mmekuja na huuu uharo..... Eti hearsays! Go to hell nyie sio Chadema na mambo ya CDM hayawahusu. Mwenyewe kakiri halafu Kuna vijitu vinatokea na kupinga! Nyie ni akina nani?

Km hoja ndo hizi kamwe chadema haitapenya vijijin wakati huko wabunge ndo wanakaaga muda mrefu madarakan kuliko mjin.
Jimbo la ubungo,mbeya mjini,mwz,ni rahsi sana kupotea kuliko majimbo ya vjijn,CDM kazi kwenu lakn kwa hili mtaangukia pua msipotumia busara
 
Wasaliti na Wahaini Kazini! Poleni.

This i Expected.Hivi kila atakayekuwa na wazo tofauti hili ndio jina lake?unafahamu maana ya Demokrasia?kwa aina hii ya ufuasi Chama cha siasa si mahala panapotakiwa uwepo,chama cha siasa maana yake ni mkusanyo wa fikra,watu watakuwa na mawazo ya kila aina, ni kazi ya chama kuchagua "agenda of the day".

Mhimili mkuu kabisa wa Demokrasia ya kigiriki tunayoitumia hadi leo ni "respect for minorities".Hivi leo hii CCM wakiamua kusema mtu yoyote anayepingana na Kikwete ni Mhaini, Msaliti italeta maana gani?

Jibu ni Rahisi-UDIKTETA. CHADEMA iwe makini kutokubali kulea vimelea hivi.Nina imani kuu viongozi wako wakuu wa chama, ingawa hawapendi mawazo ya viongozi wenzao, hawako tayari kuhusishwa au kuitwa ma-dikteta.Usiwafanye wakahisiwa kuwa hivyo kwa kauli kama hizi.
 
Zitto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Chadema. Si busara jinsi anavyosemwa vibaya na viongozi kwenye majukwaa na mitandao ya kijamii.

Chadema wajifunze kuheshimu viongozi wastaafu...

Chama cha siasa ni muunganiko wa watu wenye muelekeo na malengo ya aina moja na makusudi walio jiwekea,
Ikitokea mmoja katika kundi hilo haendani na itifaki hiyo na walio wengi kwenye kundi hilo wakakubaliana kwa kauli moja kuwa hawamhitaji, haijalishi amekosea au hajakosea ataondoshwa kwa mjibu wa taratibu walizojiwekea,

Demokrasia imelitambua hilo ndio maana tunaruhusiwa kuwa na vyama vingi ili ikitokea huendani na matakwa ya kundi furani,unaweza kuhamia kundi furani.

Zitto na wenzio demokrasia inawapa ruhusa baada ama kabla ya hitimisho la wengi,
 
Mmejipindaaaa ndio mmekuja na huuu uharo..... Eti hearsays! Go to hell nyie sio Chadema na mambo ya CDM hayawahusu. Mwenyewe kakiri halafu Kuna vijitu vinatokea na kupinga! Nyie ni akina nani?

Paranoia ni kitu kibaya sana, moja ya dalili zake ni kuamini kila mtu ni mbaya kwako.nawashauri vijana wa CHADEMA msilee tabia hii, mkimaliza na Zitto mtakuja na waliobaki, mtamtazama nani haitikii NDIO mwenyekiti kwenye vikao, Baada ya Kudeal na huyo, mtakuja na nani anaitikia kwa sauti ndogo,Mwisho mtajikuta mmefukuzana/mmetibuana wote.
Sifa kuu ya uongozi ni ku-resolve conflicts sio kuzikuza.viongozi wanaokumbukwa na kuheshimiwa na historia ni wale waliotatua matatizo,sio walioyaanzisha au kuyakuza. waanzisha migogoro na waleaji wake Historia haina Hukumu nzuri kwao
 
Namuona zito ALIVYOPANIC na KUANGAIKA.....kwa ujumla MISSION hawakuipanga kwa weledi....walichanganya na vilaza wengi....wakapanic...na mission ilikua immature wao wakawahi kuanza kujisifu na kutaka political result mapema....MTAKOMBUKA HII POST...kwa jinsi mambo yanavyokwende ...IPO SIKU ZITO ATAKUJA KUSEMA kila kitu nani amemtuma na aklipewa shilingi ngapi
 
Chama cha siasa ni muunganiko wa watu wenye muelekeo na malengo ya aina moja na makusudi walio jiwekea,
Ikitokea mmoja katika kundi hilo haendani na itifaki hiyo na walio wengi kwenye kundi hilo wakakubaliana kwa kauli moja kuwa hawamhitaji, haijalishi amekosea au hajakosea ataondoshwa kwa mjibu wa taratibu walizojiwekea,

Demokrasia imelitambua hilo ndio maana tunaruhusiwa kuwa na vyama vingi ili ikitokea huendani na matakwa ya kundi furani,unaweza kuhamia kundi furani.

Zitto na wenzio demokrasia inawapa ruhusa baada ama kabla ya hitimisho la wengi,

Ni kuwa na Mawazo finyu kuamini kuwa Binadamu wenye kuishi pamoja wana kauli moja katika kila jambo,ama kuna asiyefikiria au kuna mfuata mkumbo.sehemu isiyo na mgongano wa mtazamo ni sehemu mfu.haina Msukumo wa wusonga mbele.

Kosa la hawa BAVICHA ni kuamini suluhisho la Matatizo ya CHADEMA ni kumfukuza Zitto, ni mawazo sawa na Zanzibar kuamini umaskini wao utaisha kwa kuvunjika Muungano.Matatizo CHADEMA na ZITTO ni mutually exclusive, NCCR walimfukuza Mrema waliishia wapi?walishindwa kutatua kiini cha matatizo wakatafuta scapegoat.

Kwa tabia za Zitto yeye ni model nzuri ya scapegoat.
 
Namuona zito ALIVYOPANIC na KUANGAIKA.....kwa ujumla MISSION hawakuipanga kwa weledi....walichanganya na vilaza wengi....wakapanic...na mission ilikua immature wao wakawahi kuanza kujisifu na kutaka political result mapema....MTAKOMBUKA HII POST...kwa jinsi mambo yanavyokwende ...IPO SIKU ZITO ATAKUJA KUSEMA kila kitu nani amemtuma na aklipewa shilingi ngapi

Kwa hiyo conclusion yako ni kuwa matatizo ya CHADEMA ni Zitto kutumwa na Kikundi flani ili asababishe matatizo CHADEMA?Unaamini Matatizo ya kiutawala ndani ya CHADEMA yanatatuliwa na Zitto kutokuwepo?

Hii ni contradiction na kauli za kuwa CHADEMA inafuata Katiba na Misingi, sasa mbona hiyo misingi haijatumika kutokuleta hayo matatizo kabla Zitto hajayasasabisha?Je ni misingi ya CHADEMA kuita watu wahaini, wasaliti, wanafki pindi mnapoacha kukubaliana?
Ni misingi ya katiba ya CHADEMA kupeleleza VIONGOZI Wake wakuu kwa kuwaibia au kuwanyang'anya Laptop/simu na vitu binafsi ili kupata siri zao? Sehemu gani ya Katiba ya CHADEMA imeruhusu haya?
 
Huyu jamaa ni Chadema wa kutupwa maana hoja alizozitoa hapa za kiwatengu cdm lakini kwa njinsi ambavyo hawako makini wanamchukulia kama ni mtu aliyetumwa na Zitto hiyari yenu vita vya panzi
 
quote_icon.png
By Kimweri


You and the likes are a hopeless cause, i will not be dragged onto your useless cahoots.


I new exactly the foolishness as haven described several times in your posts in one way or another you could be

inclusive
. The fact is you have failed to provide valid information as to justify ZZK is being discriminated and not treated fairly.

The man who lives abroad Kimweri with all your intelligence please your contribution is highly recommended so that we

fools can find out the truth ..................!!!!!


1. Nataka kukuuliza, posti na mabango kwamfano hapa jf, niaslimia ngapi yanabeba hoja za kweli? (Genuine threads with reliability of at least 90% truth) kukufanya wewe kuamini yatokanayo bila kuwa na mashaka?

2. Nataka pia bila kubahatisha kama utafanya research ndogo hapahapa jf niwachangiaji asilimia ngapi ambao wanachangia hoja za msingi kwa kuweka na kujadili ukweli? Ambao unakufanya wewe unafuatilia kupitia forum kuamini unavyoamini.


3. Je unaamini kwamba wote walio nje ya nchi wanamtazamo kama wako? can you tell the probability of this please at what confidence limit.

Ukinijbu haya tutaendelea na mengine tafadhali, hukujibu umekimbilia huku kufungua uzi mwingine???


Kimweri haya maswali hujayajibu ilikupata muafaka wa mgogoro wa Zito

Mambo ya chama yanajadiliwa kwa mujibu wa katiba, taratibu na kanuni za chama.

1. shutuma na matatizo ya zito yalijadiliwa kichama kupitia wajumbe stahili.
Je katika kufanya maamuzi ya kumsimamisha zito nyazifa zake ilikuweka mambo sawa.

a) Kulikuwa na wajumbe wangapi ndani ya kikao kwa ujumla? unafaham?

b) Ni wajumbe wangapi waliunga mkono hoja ya zito kusimamishwa? (asilimia ngapi?)

c) Niwajumbe wangapi walipinga hoja ya zito kusimamishwa? (asilimia ngapi)

d) ulikuwepo ndani ya kikao ilitufahamu kwamba wewe wa nje unayafahamu ya ndani -yaani katika maamuzi ndani
wajumbe walifuata taratibu? kama hapana fafanua.


Kimweri acha kupika majungu jibu hoja hizi, kisha tupate ukweli badala ya kuzunguuka ukweli.

1. Nikweli mkumbo na mwigamba waliandaa waraka au hapana? kama hapana fafanuwa maana wahusika walikubali kuhusika.


2. Shonza, mwampamba na wengine walifukuzwa cdm au hapana? kama ndiyo tueleze sababu kuu (root cause)

3. Je nikweli Zito anashiriki shughuli zote za kichama na harakati na viongozi wengine wakuu au amekuwa akifanya kivyake? kama siyo eleza vema na kwa mifano.

4. Unatazama kinachoendelea kwa nje, yes je kinachoendelea kwandani unakifahamu? kwa evidence zipi?

5. Siku mwigulu anainnga chadema star tv, zito alikuwepo, niliangalia kipindi chote, kwanini alikaa kimya kabisa bila kuhoji hata kidogo maana ilikuwa tuhuma bado kuthibitishwa na mahakama.

Je hayo ni uzushi fafanua na kanusha kwa evidence please, kukaa nje ya nchi haimaanishi unaufahamu bora.
 
Mmejipindaaaa ndio mmekuja na huuu uharo..... Eti hearsays! Go to hell nyie sio Chadema na mambo ya CDM hayawahusu. Mwenyewe kakiri halafu Kuna vijitu vinatokea na kupinga! Nyie ni akina nani?

Elli, Elli, Elli!!! Nakuomba wakati mwingine jaribu kujipa muda uifikirie Tanzania, na uifikirie Chadema inavyotakiwa kustawi. Don't be static like direct current. Chama kinahitaji kujitafakari, lakini siyo neno CHADEMA ndiyo litajitafakari, bali ni wewe Elli na fulani na fulani. Siyo kila wakati unakuwa UNI...., jitahidi wakati mwingine kuwa BI....!!! Kilichoandikwa ni chachu ya kujenga fikra.
 
Ni kuwa na Mawazo finyu kuamini kuwa Binadamu wenye kuishi pamoja wana kauli moja katika kila jambo,ama kuna asiyefikiria au kuna mfuata mkumbo.sehemu isiyo na mgongano wa mtazamo ni sehemu mfu.haina Msukumo wa wusonga mbele.

Kosa la hawa BAVICHA ni kuamini suluhisho la Matatizo ya CHADEMA ni kumfukuza Zitto, ni mawazo sawa na Zanzibar kuamini umaskini wao utaisha kwa kuvunjika Muungano.Matatizo CHADEMA na ZITTO ni mutually exclusive, NCCR walimfukuza Mrema waliishia wapi?walishindwa kutatua kiini cha matatizo wakatafuta scapegoat.

Kwa tabia za Zitto yeye ni model nzuri ya scapegoat.

Ni opinion yangu kwamba kuna mambo ya msingi ya kujadili ili kuboresha maisha ya wananchi wakawaida ambayo yana zidi kuwa duni siku baada ya siku kukosa huduma bora nk, utawala wa sheria haupo umeyeyuka, na mengine mengi, Zitto amekuwa akipigania yote haya nk, hivyo yuko huru kujiunga na chama chochote ili ayaendeleze hayo, kwani ni lazima awe chadema kuyaendeleza hayo?, Mgogoro wote huo una back up kubwa, na imani ccm hawapendi kutoka madarakani, so u can figure out urself.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom