siwazi wa siwazi
Member
- Aug 20, 2016
- 9
- 2
Matumaini yangu kuwa hamjambo na wazima wa afya, binafsi naendelea vizuri alhamdulillah maisha kimtindo yanakwenda japo twazidi kuzisoma namba.
Nimeona nitoe maoni yangu kwenu juu ya masuala yanayoendela ndani ya nchi yetu ya vi-wonder
Nikianza na sakata la Zakaria Hans Pope kwa magari yake kukamatwa, binafsi ningependa kuwapongeza TRA kwa kazi nzuri sana wanayofanya ya kukusanya mapato.
Kwa mujibu wa taarifa zinadai kwamba magari hayo ambayo yamebeba mafuta ya muwako, yamekaa mpakani Tunduma kuanzia Tarehe 19/01/2017 mpaka hii leo, ukipiga hesabu ni takribani miezi miwili.a
Magari yaliyokamatwa ni takribani 16 ambayo yote yapo chini ya mmiliki mmoja ambaye ni Zakaria Hans pope, kama hiyo haitoshi magari hayo yame-pack sambamba kabisa na magari mengine.
Kitendo kinachoelezwa kwamba huenda kikasababisha hatari ya mlipuko, rai yangu kwa serikiali ni kuitaka ifanye kazi kwa ufanisi, uweledi na bila kuingiza visasi au uhasama wa aina yoyote.
Unaambiwa kabla ya hapo, TRA walikwenda kukagua ofisi za malori ya Hans Pope mwishoni mwa mwaka jana na kwa habari zilizochini ya kapeti ni kwamba kipindi MKULU akiwa WAZIRI walipishana kauli na kamanda Z.H.POPE.
KWA UPANDE WA PROF. ASSAD
Kusema ukweli nikijaribu kuangalia mwenendo wa nchi yetu tunapotaka kwenda na mienendo yake ama kwa hakika sipati jibu, nahisi ni kama mchezo wa karata.
Haiwezekana kiranja mkuu wa fedha za serikali (CAG) Prof.Assad akapunguziwa budget ya ofisi yake kwa takribani asilimia 40, mpaka kufikia hatua ya yeye kusema kwamba ukata umeikumba ofisi zake.
Hivi hizi pesa tunazoziita za miradi ya maendeleo ambazo zinatoka kwetu wavuja jasho kwa kubanwa kila kona ya kodi, Ni nani atakayeweza kuzikagua kama zinafanya kazi yake ipasavyo kama sio huyu CAG?
Kitendo cha ofisi ya CAG kufinywa budget yake kinaonyesha wazi kabisa serikali yetu inachokifanya sio kutufikisha kwenye Tanzania tunayoitaka au ambayo tuliahidiwa wakati wa kampeni.
Rai yangu kwa Taifa zima ni kuingia kwenye maombi ya nguvu kwa waumini wa dini zote, kuliombea hili Taifa na kuvunja roho mbaya, za chuki, visasi na kiburi cha hali ya juu kwa viongozi wanaotuongoza.