Sakata la ving'amuzi kurusha local channels bure.

Sakata la ving'amuzi kurusha local channels bure.

astranaut

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
1,276
Reaction score
1,024
Naomba anaefahamu ni lini sasa ving'amuzi vya azam,zuku na DSTV vitarejesha channel za bure ukizingatia kwamba channel hizo zimeondolewa kabisa ambapo hata ukilipia kifurushi channel hazifunguliwi,kuoneshwa basi bure kama ambavyo sheria inawataka hazioneshwi.Kweli serikali imeridhia sasa wananchi wanyonge tukose habari jambo ambalo ni razima kwa kila mtanzania?.Mf:king'amuzi cha zuku kifurushi kikiisha wao wanakata hadi TBC ambayo ilikua FTA kwa ving'amuzi vingine sasa mim nashindwa kuelewa hizo leseni ambazo zinawataka kurusha local channels bure kwamba zilitolewa kwa upendeleo?
 
Dstv TBC ni FTA ila channel zingine zote hazipo kabisaa! Nilishaacha kulipia king'amuzi changu cha Dstv kwa mwezi wa pili sasa. Kwa sababu huwa siangalii tbc. Serikali na hizo kampuni wametunishiana misuli na kesi ipo mahakamani....
 
Nadhani umeelewa tofauti ktk sheria za Tz kuhusu FTA.
Walioshinda zabuni ya kurusha FTA ni Startimes, Continetal na mwingine nimemsahau.
Hata DSTV sidhani kama wanarusha tena TBC baada ya kulimwa barua na TCRA.
Lakini nakuomba fuatilia kwa undani zaidi hili sakata. Inawezekana mimi ndo sijaelewa vzri.
 
TCRA wametoa leseni za aina 2 ving'amuzi vya local channel bure kama startimes,tin na continatal na ving'amuzi vya kulipia kama Dstv ,azamtv na zuku
Katika hivi vya local channel bure nafikiri utata umesha isha kifurushi kikikata local channel zinaendelea kuonekana
Utata umebaki hivi vya kulipia kwa nini wananchi wenye hivi ving'amuzi hawaruhusiwi kuona local channel?
Wanasema sheria hairuhusu je hiyo sheria katunga nani mungu au binadamu
Kama katunga binadamu kwa nini hawataki ibadirishwe?
Wao wenyewe waheshimiwa wa TCRA ndio wanajua
 
Serikali iliangalie vizuri na kwaupendo suala hili muhimu kwa wananchi wake. Wengi tumeimia sana kwa haya maamuzi yadiyo na tija. Wangewaruhusu tu warushe local channel kwa sabsbu wao wLiendelea kupata chao nsdi tukienjoy. Matokeo yake sasa wengi hatulipiii tena na matokeo yake twajenga chuki kuangalia TBC pekee. Naamini inawezekana wakubwa wakiamua. Nina cha Azam hapa bata kulipia nimeacha, naangalia TBC tu.
 
Startime Dish ipo Tbc tu hakuna channel za bure zingine.
Awali walikuwa Na decoda za aina 2 Na bei ilkuwa tofauti kimoja kilikuwa kinarusha free local channel Na kingne cha kulipia kama chako. ila kwasasa vyote ni free local channel wakikata bac call them for help
 
Write your reply...Waliweza vyeti feki tu.
 
Nadhani umeelewa tofauti ktk sheria za Tz kuhusu FTA.
Walioshinda zabuni ya kurusha FTA ni Startimes, Continetal na mwingine nimemsahau.
Hata DSTV sidhani kama wanarusha tena TBC baada ya kulimwa barua na TCRA.
Lakini nakuomba fuatilia kwa undani zaidi hili sakata. Inawezekana mimi ndo sijaelewa vzri.
Na makosa hayo mi nafkili yalifanyika mwanzoni kipindi huu mfumo wa kditali unaingizwa nchini,kwanini Serikali haikuainisha mapema vipengere hivyo kwenye mikataba? na kama kweli kwenye mikataba hivyo vipengele vilikuepo serikali kipindi chote ilikua wapi?
 
Nauliza tuu zile channel Zetu bado zipo tusije tukawa tunaua viwanda vya ndan!! Inawezekana mashine za kurushia matangazo na camera havifanani na kiwanda, mi mwenyw sijui kama nauliza au nashangaa
 
Back
Top Bottom