TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,562
Waziri wa Maliasili Professor Jumanne Maghembe, amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne wa misitu na wanyama pori kwa kuruhusu wanyama kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria. Habari kuhusu Wanyama waliokamatwa fuatilia hii thread=>Raia wa Uholanzi wakamatwa KIA na tumbili 61
Chanzo: ITV
Nukuu za Waziri Maghembe...
Akizungumza na kituo cha ITV Waziri Magembe amesema==> watu wanavuna mazao ya misitu kule kalambo, tukaenda kule tukakutana na magogo mengi sana yako msituni ambayo yanatakiwa yawe yamelipiwa na hayakulipiwa, nimewaondoa hili tuweke uongozi mpya kwa sababu kinachoonekana ni kwamba hawana uwezo wa kuongoza’
Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori Charles Mulokozi, Waziri Magembe amesema ==> Jana usiku tumekamata ndege ambayo ilikuwa inasafirisha nyani, inaonekana ni biashara inayofanywa kwa hiyo amesimamishwa kazi, uchunguzi ufanywe ili tuone hili jambo la kusafirisha wanyama nje ya nchi limefanywa kiasi gani na ni nani anafanya’
Chanzo: ITV
Waziri wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msimamizi wa Wanyamapori, Charles Mulokozi baada ya kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili kwenda Albania.
Sakata hilo limetokea baada ya Jeshi la Polisi kuwakamata raia 2 wa Uholanzi katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa na Tumbili 61 hai wakijaribu kuwasafirisha kwenda nchini Albania.