Kama ilivyo ada kwa serikali ya CCM kufumbia macho maslahi ya umma na kuwabeba wawekezaji huku raia wakiachwa na athari za uchimbaji madini Tanzania, UCHIMBAJI UNAOTARAJIWA KUANZA HIVI KARIBUNI WA MADINI YA BAUXITE KIJIJI CHA MAGAMBA WILAYA YA LUSHOTO HALI IMETAJWA KUWA TETE.
Hali hiyo imetokana na kile kinacholalamikiwa na wanakijiji wa kijiji husika, kata na uongozi wa wilaya kudai hawajashirikishwa kwenye mpango huo ulio mbioni kuanza .
Wawekezaji walidai kupata baraka za mkuu wa wilaya lakini walipotakiwa na uongozi wa kijiji kuonesha kibali toka kwa kiongozi huyo kibali hakikuwepo.
Kilio cha wakazi kijijini hapa ni kuona raslimali hiyo inayowazunguka haitawanufaisha kwa lolote licha ya kuachwa na madhara makubwa yatokanayo na uchimbaji huo.
Kesho kutwa jumamosi ya wiki hii kutakuwa na mkutano kujadili juu ya uwekezaji huo na mkuu wa wilaya hiyo atakuwepo kutoa ufafanuzi.
Maeneo yatakayoathirika na uchimbaji huo ni pamoja na eneo la hekta nane linalomilikiwa na chuo kikuu cha Sebestian Kolowa mjini Lushoto.
Uongozi wa chuo pia haujashirikishwa na hayo yameelezwa na makamu mkuu wa chuo hicho Bibi Aneth Munga saa chache leo asubuhi wakati akiongea na wanachuo wa mwaka wa kwanza chuoni hapo.
BAUXITE EXPLOITATATION itaua mali asili za northen pick ikiwa ni pamoja na aina tofauti za mimea zaidi ya 684 zinazozunguka milima Usambara ambazo ni urithi mkubwa kwa mtanzania kwa faida ya wawekezaji.